Kampuni ya simu za mkononi, TECNO
inayofanya kazi chini ya TRANSSION HOLDINGs imezidi kutanuwa wigo wa soko la simu nchini kwa kufungua duka
jipya maarufu “Experience Center’’ Dar
es salaam, Samora, jumamosi 24/03/2018,
uzinduzi huo ulihudhuriwa na naibu waziri mawasiliano na uchukuzi mheshimiwa Atashasta
Nditiye, watu maarufu, wageni waalikwa,
wadau wa TECNO kutoka mtandaoni na nyanja mbalimbali nchini.
Mgeni rasmi Naibu waziri mawasiliano
na uchukuzi Mheshimiwa Atashasta Nditiye alishiriki zoezi la kukata utepe
pamoja na mkurugenzi mkuu wa TECNO Bwana Xu pamoja na meneja wa Clouds media
group Ruge Mutahaba
Mheshimiwa pia aliweza kuzunguka sehemu mbalimbali za duka hilo kujionea
huduma mbalimbali zinazopatikana,ni wazi TECNO imekua chachu ya kukuza
Teknolojia na mawasiliano ambapo aslimia 94 ya wananchi wana mawasiliano
nchini, lakini napongeza kitendo cha watumiaji kupewa elimu ya namna ya kutumia
simu janja kuepuka uhalifu, nawapongeza sana TECNO ”alisema Naibu waziri
Nditiye.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkurugenzi wa TECNO nchini, Daniel Xu alisema “Ni furaha
kujumuika nanyi katika uzinduzi wa duka la TECNO “Experience Center”, wateja
watapata fursa ya kununua bidhaa, kupewa elimu ya bure kuhusiana na
matumizi,sifa na mifumo mbalimbali ya simu, lakini pia huduma ya matengezo
“after sales service” kupatikana papo hapo dukani.
Uzinduzi huu unatoa fursa nyingine ya
ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuwainua kiuchumi, ambapo zaidi ya vijana
500 wa kitanzania wameshaajiliwa kwenye kampuni ya TECNO,Mkurugenzi Xu alimaliza.
Pia sherehe hzio zilipata ugeni
kutoka kwa wanamuziki na mastaa tofauti tofauti ikiwemo mchekeshaji almaarufu
kama JayMondy, ambapo alijuimika na wadau wa TECNOkupitia kurasa zake za
mtandaoni. Kulikua na michezo, elimu na burudani kabambe na bahati nasibu.
Naibu waziri Nditiye akiendesha zoezi
la bahati nasibu,na baadaye alikabidhi zawadi kwa wateja waliojishindia zawadi kabambe
kupitia droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa kwa hisani ya TECNO.
Naibu waziri Mh. A. Nditiye,
Mkurugenzi wa TECNO na meneja masoko Franck Luo, wakiwa na baadhi ya washindi
wa bahati nasibu.
Kampuni ya TECNO inawakaribisha
katika duka lao jipya linalopatikana Samora, Posta.
No comments:
Post a Comment