Thursday, March 1, 2018

MZEE JORAM MOLLEL MAARUFU KAMA "BABU" APATA NAMBA YAKE YA KUSHIRIKI TIGO KILI HALF MARATHON 2018

Mzee Joram Mollel maarufu BABU mwenye umri zaidi ya miaka 90 akijisajili kushiriki mbio za kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Mtoa huduma wa Tigo, Mohammed Ally akiwasajili Aghata Philii na Poling Nikesa raia wa Zambia kushiriki mbio za Tigo Kili Half Marathon kwenye viwanja vya Kibo Palace Arusha juzi. Mbio zinatarajiwa kutimua vumbi jumapili ya wiki hii Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akimkabidhi Babu Molell  NAMBA ya ushiriki wa mbio za  kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo akifurahi mara baada ya kumkabidhi  Babu Molell  NAMBA ya ushiriki wa mbio za  kilomita 21 Tigo Kili Half Marathon zitakazotimua vumbi siku ya jumapili wiki hii mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

No comments: