Anaandika @exaud_msaka_habari1
MWANDISHI WA HABARI NI NANI
Mwandishi wa habari ni mtu ambaye ameamua kuwa Daraja kwa wananchi, mtu ambaye ameamua kufanya kazi ya kuwasikiliza watu ambao hawasikilizwi na kuwaweka mbele ili wasikike
Anaruhusiwa kusifia sana pale ambapo panahitaji sifa na anaruhusiwa kukosoa pale ambapo kunahitajika kukosoa, huku akifuata sheria za nchi na taaluma yake pamoja na miongozo ya taaluma husika
Mwandishi huyu anaendeshwa na ukweli, heshima kwa wengine na weledi mkubwa huku akitakiwa kutomuonea mtu kwa sababu ya kalamu au Mic yake
Katika kila analofanya huyu bwana anatakiwa asahau kabisa kuhusu maslahi yake, wala hatakiwi kujiuliza anapata nini, swali muhimu anatakiwa ajiulize jamii inapata nini, wananchi watasikika wanachotaka ?
MWANASIASA NI NANI ?
Mwanasiasa ni mtu ambaye anatumia ushawishi wake wa maneno, vitendo na vitu vingine kupendwa na wananchi ili wampe madaraka
Anaweza kushawishi kwa kuwaletea maendeleo (Kitu ambacho ni sahihi) anaweza kushawishi kwa kuwapa maneno ya matumaini (inaruhisiwa) na wasio weledi wanaweza kutumia pesa (Rushwa)
Baadhi ya wanasiasa kazi yao inawalazimu kutumia maneno ya uongo ili kufanikisha malengo yao
Mwanasiasa yupo tayari afanye jambo lolote, aseme lolote ili kulinda nafasi yake, kwa sababu kwenye siasa kupoteza cheo inaonekana kama ni kupoteza nusu ya maisha
Tofauti na taaluma ya habari, mwanasiasa haendeshwi na Kanuni za taaluma yake (siasa sio taaluma) hana miongozo mingi sana na kipimo chake ni wananchi wakimpenda kwa njia yoyote
HITIMISHO
Ukisoma hadi hapo utagundua fani hizi mbili haziwezi kukaa kwenye kichwa cha mtu mmoja na zikafanikiwa
Yani mwanasiasa ambaye analalamikiwa na wananchi ndio awe daraja kati ya wananchi na mwanasiasa yani awe mwandishi wa habari ? Atasema nini kwenye Mic pale ambapo upande wake wa siasa unahitaji kukosolewa, yani ajikosoe ?
Taaluma ya habari ni eneo ambao halitakiwi kuchanganywa na kitu kingine chochote......

No comments:
Post a Comment