Saturday, March 5, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 6,2016 YAKO HAPA


Maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar.

Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Kisonge Zanzibar. katika Viwanja vya Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Zanzibar michezani Kisonge akiongozana na Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation Ndg Masaud Maftah, katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Maonesho ya Wajasiriamali wa Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Informal Sector Foundation Ndg Masaud Maftaha na  Mwenyekiti wa Zanzibar Informal Sector Foundali Bi Nuru Mohammed Ahmeid, wakati wa hafla hiyo ya Maonesho ya Biashara za Wajasiriamali Wanawake Zanzibar katika maonesho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Mkurugenzi Mkuu wac Banki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi, akizungumza wakati wa maonesho hayo ya Wajasiriamali Wanawake kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani yaliofanyika katika viwanja vya Mnara wac Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar Michezani Kisonge.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Banki ya Posta Tanzania Ndg Sabasaba Moshingi baada ya kusoma risara yake wa maonesho hayo na kukabidhi hundi kwa ajili ya kuchangia Maonesho hayo.  
Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea mfano wa hundi ya shilingi miliono kumi na tano ikiwa mchango wa Benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya kufanikisha Maonesho hayo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kutoka Mkurugenzi Mkuu wa TPB. Ndg. Sabasaba Moshingi,   
Makamu wa Pili wac Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipokea mfano wa hundi ya shilingi miliono kumi na tano ikiwa mchango wa Benki ya Posta Tanzania kwa ajili ya kufanikisha Maonesho hayo ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kutoka Mkurugenzi Mkuu wa TPB. Ndg. Sabasaba Moshingi,

ACT WAZALENDO WAPANGA SAFU MPYA YA UONGOZI


WENYEVITI NA MAKATIBU WA KAMATI ZA KITAIFA WA CHAMA CHA WAZALENDO (ACT-WAZALENDO)

Kamati Kuu ya Chama cha Wazalendo (ACT-Wazalendo) imeidhinisha uteuzi wa Wenyeviti na Makatibu wa Kamati za Kitaifa. Wanachama walioteuliwa na wasifu wao ni kama ifuatavyo:

TFF YAPIGA MARUFUKU MICHEZO YA KUBAHATISHA (BETTING)


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa mshtuko taarifa za kuwepo makundi ya watu na makampuni wanaochezesha michezo ya kubahatisha inayohusu mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na kusimamiwa na TFF (betting).

TFF inauthibitishia umma wa watanzania kuwa Shirikisho halihusiki wala halijawahi kutoa kibali chochote cha kuhusisha mashindano yake na michezo ya kubahatisha.
Kwa kuwa baadhi ya wahusika wa matendo hayo ni makampuni ya nje ya nchi hivyo TFF imechukua hatua zifuatazo:
1.TFF imeandika barua kwenye Shirika la Bahati Nasibu ya Taifa ili kupata mwongozo wa kisera na kisheria kuhusu haki na majukumu ya Shirika hilo  katika kudhibiti na kusimamia  jambo hilo.
2.TFF imeandika barua kwa kitengo cha sheria cha FIFA ili kupata mwongozo na ushauri wa namna ya kudhibiti makampuni ya nje yanayoshiriki mchezo huu.
TFF inawaomba wadau wa mpira wa miguu na washiriki wa michezo ya kubahatisha wajiepushe kushiriki michezo ya kubahatisha inayohushu michezo yote inayoandaliwa na TFF.

Mahafali ya Nne ya Chuo cha Zenith Learning Center Kwa Kushirikiana Travelport Tanzania.Kinachotoa Mafunzo ya Ukataji wa Tiketi za Ndege Kwa Njia ya Kieletronic (Galileo Resevation Systeam)

Mwalimu wa Chuo cha Zenith Learning Center Ali Mussa Mohammed, akizungumza kabla ya kuaza Mahafali ya Nne ya Chuo hicho yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho Majestik Zanzibar jengo la Zanlink,Jumla ya Wahitimu 28 wametunikiwa Vyeti vyao na Mwenyekiti wa Bodi ya Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dr Ahmada Khatib.
Mkuu wa Mafunzo wa Chuo cha Zenith Learning Center Mundhir Nassor akitowa maelezo ya Kozi zinazotolewa na Chuo hicho kwa mgeni Rasmin kabla ya kuzungumza na wahitimu na kuwakabidhi vyeti vyao, Chuo hicho kinatowa Kozi ya Kimataifa ya Ukataji wa Tiketi za Ndege kwa Njia ya Kielectoniki
 (GALILEO  RESERVATION SYSTEM) 

Friday, March 4, 2016

BOA Yawajengea Uwezo wa Kibiashara Wadau na Wafanyabiashara wa Zanzibar katika Mpango wa Biashara


Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Bwa. Ammish Owusu Amoah akitowa maelezo kwa Washiriki wa Warasha ya Siku Mbili ya Kuwajengea Uwezo Wafanyabiashara kuibua Mipango ya Biashara iliowashirikisha Wadau mbalimbali katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Ammishi Owusu-Amoah akisisitiza jambo wakati wa ufungaji wa Warsha hiyo ya Siku mbili ilioandaliwa na Bank Of Africa kwa ajili ya wafanyabiashara na wadau kuweza kuweza kufanya Mpango wa Biashara.  
Mtaalam wa Banking Tanzania Bwa,Michael Alcorn akitowa maelezo wakati wa Warsha hiyo ya Siku mbili kwa Wafanyabiashara wa Zanzibar ilioandaliwa na Bank Of Africa Tanzania iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Washiriki wa Warsha hiyo wakifuatilia Mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika Mafunzo hayo.

Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Azinduzi wa Tawi la Bank Of Africa Mlandege Zanzibar

Tawi Jipya la Bank Of Africa lililofunguliwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee likiwa Tawi la 22 Bank Of Afrika Nchini Tanzania, linalotowa huduma za Kibenki.
Wajumbe wa Bank Of Africa wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bank Of Africa Nchini Tanzania Bwa. Ammish Owusu-Amoah, katikati wakizungumza wakimsubiri Mgeni rasmin Waziri wa Fedha Zanzibar.
Mwenyekiti wa Bodi ya Bank Of Africa Tanzania Balozi Mwanaidi Maajar akisalimiana na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe Omar Yussuf Mzee alipowasili katika viwanja vya Bank hiyo hapo mlandege kwa ajili ya Uzinduzi wa Bank hiyo.

MAGAZETINI LEO JUMAMOSI MARCH 5,2016 YAPO HAPA

TIGO YATOA UDHAMIN WA MILIONI 11 KAMPENI YA ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA”

 Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa Tigo wa kiasi cha Shilingi Milioni 11 katika kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  ambayo inatarajiwa kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye  “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 saa 12 asubuhi, katikati Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi na kushoto  ni Rais wa  (TWA,) Irene Kiwia   ambao ndio waandaaji wa matembezi hayo, kwenye mkutano uliofanyika mapema jana  jijini Dar es salaam.
Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) Irene Kiwia  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu udhamini wa Tigo katika  kampeni ya kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, inatarajiwa kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye  “Uwanja wa Farasi ”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 kwenye mkutano uliofanyika mapema jana  jijini Dar es salaam. 

MWIGULU NCHEMBA APASUA JIPU HUKO MIKUMI,AANZA ZIARA NCHI NZIMA KUFUFUA VITUO VYA UTAFITI NA UZALISHAJI MBEGU



Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa aghala la mbegu za ASA(Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.
Mh.Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani morogoro.
Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi wa ASA(Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo,Kubwa alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.
Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu malisho ya ng’ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo -Morogoro(LITA).
Mh:Waziri akiangalia baadhi ya ndama wa Ng”ombe waliopo kwenye shamba la Utafiti kwenye kituo cha LITA-Morogoro
.
Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu Mkuu wa chuo za SUA(Sokoine University of Agriculture) alipofika kwaajili ya kukutana na wataalam,na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea maoni yao kuelekea kilimo,ufugaji na uvuvi wa kisasa. “Transformation of Agriculture”.
Katika kikao hicho,Wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Akiwa njiani kuelekea Ifakara,Mwigulu Nchemba anaamua kufanya mkutao Jimbo la Mikumi kijiji cha Tungu kwaajiliya kusikiliza kero za wananchi dhidi ya uongozi wa miwa wilaya,Mkoa na Taifa,mahusiano mabaya ya kibiashara kati ya wakulima wa miwana kiwanda cha ilovo,Lakini utitiri wa vyama vya wakulima kwa eneo lakilombero.
Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mbunge wa Mikumi Mh.Joseph Haule(Prof.Jay) wakati wa mkutano huo
Baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi na kusoma baadhi ya ripoti za serikali ya wilaya na mkoa na zile za Tume mbalimbali zilizounda kujua kiini cha matatizo ya wakulima wa miwa-Kilombero,Mwigulu Nchemba akiwa ndiye waziri mwenye dhamana na kilimoa akaamua kufuta uongozi wote kwa wakulima wa miwa kuanzia ngazi ya wilaya ya Mikumi hadi Taifa kwa kosa la ubadhilifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa mbegu za Mpunga-Kilombero.Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa mfumo wa kutegemea mvua ilimimea kupata maji na kukua kwa wakati.
Mwigulu Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya Utafiti na uzalishaji wa mbegu nchi nzima,lakini wakati huo huo atatembelea mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Picha/maelezo na festo Sanga Jr

SERIKALI YAMKABIDHI CHEKA CHETI CHA PONGEZI KUTOKANA NA USHINDI WAKE.

che1
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(kulia) akiwa ameambatana na Bondia Francis Cheka (wapili kulia) alipotembelea Wizarani leo jijini Dar es Salaam na Serikali imemkabidhi  Cheti cha pongezi. Kushoto ni Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh).
che2
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi kutokana na ushindi Bondia Francis Cheka (kushoto) leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge.
che4
Bondia Francis Cheka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  wakati wa zoezi la kupokea Cheti cha pongezi kutoka kwa Serikali leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye,Rais wa Chama cha ngumi Tanzania (TPBO) Yassin Adballah (Ustadh) na Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
che5
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wapili kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa BMT Mohamed Kiganja (aliyesimama) akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la kumkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka (kushoto) kutokana na ushindi wa Mkanda wa Uzito wa Super Middle wa Mabara wa WBF leo jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge
che6
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi Cheti cha pongezi Bondia Francis Cheka kutokana na ushindi alioupata katika pambano baina yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
che7
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) na Bondi Francis Cheka wakiwaonyesha waandishi wa Habari Mkanda wa uzito wa Super Middle wa Mabara ambao Cheka ameunyakuwa baada ya kushinda pambano la tarehe 27 Februari baina yake na Bondia Mserbia anayeishi Uingereza Geard Ajetovic (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bondia huyo Chifu Ndambile Juma Ntinginya.
Picha na Frank Shija, WHUSM

JAMII FORUM WALIVYOJITOSA MAHAKAMANI KUHUSU SHERIA YA MTANDAO

Septemba Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.
Leo March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com naFikrapevu.com imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza unaolindwa kwa mujibu wa katiba ya Nchi.

TAARIFA RASMI KUHUSU HABARI ZA KUTENGWA KWA ZITTO KABWE ACT ZANZIBAR


TAMKO LA CHAMA KUHUSU ACT PEMBA WAMTENGA ZITTO KABWE


Chama cha ACT Wazalendo kimesikitishwa na na kinalaani taarifa ilichapiswa na iliyosambazwa leo tarehe 03 Machi, 2016  na Gazeti la Raia Tanzania kwamba wanachama watano (5) na waliokuwa wagombea wa uwakilishi kwa tiketi ACT Wazalendo Pemba wakimuhusisha Kiongozi wa Chama ndugu Zitto Zubeir Kambwe kwamba amefuata msimamo wa CUF katika kufikia uamuzi wa kutoshiriki Uchaguzi wa marudio Zanzibar tarehe 20 machi, 2016.