Wednesday, October 4, 2017

MBUNGE CHUMI AZIPIGA TAFU TIMU ZA JIMBONI KWAKE KWA KUZIPA VIFAA VYA MICHEZO NA FEDHA

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akitoa maelezo wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akipeana mkono na viongozi wa timu ya Mafinga veterani wakati wa kugawa vifaa vya michezo kwa timu za mafinga mjini pamoja na kuisaidia timu ta Mufindi United kiasi cha shilingi laki Tano


 Na fredy Mgunda, Mafinga

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi amezipiga tafu timu zinazoshiriki ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Iringa kwa kuzipatia jozi moja moja ya jezi kwa kila timu lakini pia ameichangia timu ya Mufindi United inayoshiriki lingi daraja la kwanza Tanzania bara kiasi cha shilingi laki tano kwa lengo la kuisaidia katika harakati zake za kupanda daraja.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa na pesa hizo Chumi alisema kuwa ameguswa kufanya hivyo kwa kuwa anapenda michezo na anacheza mpira wa miguu kufanya hivyo kutaendelea kuzipa morali timu za jimbo la Mafinga Mji kufanya vizuri kwenye mashindano wanayoshiriki.
  

"Leo nimekabidhi jezi kwa timu zinazoshiriki daraja la tatu ngazi ya mkoa na timu hizo ni Bajaji Fc,Mabo Fc (Boda Boda) na Kinyanambo United nimefanya hivyo kuzifanya timu hizi kuzihamasisha kufanya vizuri kwenye ligi hiyo" alisema Chumi


Chumi aliwataka wananchi na wadau wanaoipenda timu ya Mufindi United kuendelea kuisaidia katika haraka za kupanda daraja kwa kuwa kuendesha timu ni gharama kubwa hivyo tuungane kwa pamoja kufanikisha lengo letu ili kupata timu itayokuwa ligi kuu Tanzania Bara msimu ujao.


“Jamani kushiriki ligi daraja la kwanza ni gharama sana na ligi ya mwaka huu ni ngumu hivyo tunahitaji kuwa na pesa nyingi kufanikisha lengo letu la kuwa na timu ya ligi kuu wenzetu wengine wamejipanga sana na wanapesa hivyo timu yetu ikiwa na njaa itatuwia vigumu kuipandisha” alisema Chumi


Aidha Chumi hakusita kuwapongeza viongozi wa timu ya Mufindi United pamoja na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri William kwa kuendelea kuisadia timu kushiriki lingi hivyo kwa michango na mawazo yao.


“Mimi nilijua mwaka huu tunashushwa daraja maana hali ilikuwa ngumu wakati wa usajili lakini viongozi hawa walipigana kufa na kupona wakahakikisha timu inasajili na inacheza ligi hiyo” alisema Chumi



TECNO SMART HUB KUBWA ZAIDI KUZINDULIWA JUMAMOSI.

TECNO imeeendelea kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora Zaidi kuwahi kutokea katika biashara simu kwa kutengeneza duka jipya la kisasa zaidi.
 TECNO SMART HUB ndio jina  sahihi la maduka haya mapya yanayofunguliwa na kampuni hii, duka hili jipya la kisasa linatarajiwa kufunguliwa eneo la Mlimani city , jengo jipya ambapo kutakua na  watu maarufu mbalimbali walioalikwa , wadau wa kampuni ya TECNO pamoja na mashabiki wa TECNO mitandaoni.

 Duka hili kubwa linalotarajiwa kufunguliwa siku ya jumamosi maaraufu kama TECNO SMART HUB litakua linatoa huduma bora zadi ya maduka mengine ya kawaida  ya simu. Huduma zinazotarajiwa kutolewa katika TECNO SMART HUB ni pamoja na mauzo, huduma baada ya mauzo na kikubwa katika maduka haya elimu mahsusi juu ya matumizi ya simu janja  “smartphone” itakua inatolewa na wabobezi wa simu hizo watakao kua dukani muda wote, lakini pia wateja watkaohudumiwa katika duka hili  wataapta nasafi ya kupumzika na kupata vivywaji huku wakipata huduma bora.


TECNO SMART HUB itazinduliwa siku ya jumamosi tarehe 7 ambapo watu 200 wa kwanza kuingia dukani watapata zawadi za bure wakati kwa wanunuaji wa simu siku hiyo watakua na nafasi za kupata zawadi mbili kwa mpigo, furaha Zaidi ni pale ambapo wateja wote wataweza kuingia katika bahati  nasibu ya kushinda televishen ya inchi 32 mbili pamoja na zawadi zingine kama feni, power bank na majagi ya umeme.
Wakati wa uzinduzi wa duka hilo jipya, vinywaji baridi  vitakua vinatolewa kwa wateja  wa bidhaa mbalimbali zikiwemo hata vifaa vya simu  pamoja na siu zenyewe, kadi maalumu za matengenezo ya simu zitatolewa pia kwa  wateja “VIP card”, huku burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali zikitawala eneo hilo kuhakikisha TECNO SMARH HUB linakua sehemu ya kisasa Zaidi.

TECNO inawaalika  wateja wote kwenda kununua simu kattika  duka hili jipya la kisasa ili kujishindia zawadi mbalimbali na kuingia katika familia ya TECNO kupitia bidhaa zilizopo katika SMART HUB.

WANAHARAKATI WA GDSS WAZIJADILI CHNGAMOTO NA FAIDA ZA TEHAMA

Wanaharakati wa semina za jinsia na maendeleo GDSS wamekutana mapema wiki hii lengo likiwa ni  kujadili faida na changamoto mbalimbali za matumizi ya teknolojia ya habari na mwawasiliano (TEHAMA).
Akiongoza semina hiyo muwezeshaji kutoka Mtandao wa jinsia(TGNP) Bi. Veronica Magayane alisema kuwa wanaharakati wanajukumu kubwa la kuleta usawa na haki katika jamii hivyo ni vema kutumia Tehama katika harakati zao na kujiletea maendeleo kama wajasiliamali wadogo.

Wakitoa maoni mbalimbali kuhusu matumizai ya Tehama wanaharakati hao walisema kuwa mfumo wa elimu yetu siyo rafiki kwa matumizi ya Tehama kwani serikali ilitakiwa kuweka mfumo huu kuanzia shule ya msingi na secondary ili wanafunzi waweze kuelewa vizuri kitu hiki, na waweze kukitumia kwa faida yao ya sasa na baadae na siyo kusubiri mpaka wafike chuo ndipo waanze kujifunza.

Lakini pia ni kwa wazazi kukosa uelewa wa kutosha kuhusu teknolojia hii kwamba mzazi anasema awezi kumnunulia kompyuta mtoto wake anaesoma kwa kudai hana fedha wakati huo huo anachangia harusi zaidi ya laki mbili wakati ni kiwango ambacho unaweza kuipata hiyo kompyuta, lakini pia kwa kuhisi atajifunza vitu vingi vibaya ambavyo ni utamaduni wa nje ya taifa letu na kuhisi ataharibikiwa wakati angefanya hivyo ingekuwa ni njia nzuri ya kumuandaa mtoto kufahamu Tehama ambayo ingemsaidia kwa maisha yake ya baadae.
Na jambo lingine wanaharakati walisema kuwa kwa watu wazima wengi wanahisi wao hawastahili kutumia Tehama kwani ni mambo ya vijana wakati ni njia nzuri ambayo ingewasaidia katika kutimiza majukumu yao na ingeweza kuwaletea faida katika ujasiliamali wao kwani mtu unaweza kutumia Watsaap, ama Instagram kutangaza biashara yako na ukapata wateja wengi kuliko kukaa sehemu moja kusubiri mteja ambae hujui atakuja saa ngapi.

Aidha wanaharakati waliendelea kusema kuwa njia hii endapo itatumiwa vibaya basi inaweza kuleta matokeo mabaya katika biashara zao, mfano ukuwa unauza nguo na ukapiga picha lakini ukaongezea rangi kupitia instagram mtu akihitaji nguo ile ukampelekea inawezekana yeye alipenda ile rangi ilivyokolea lakini akaona tofauti na uliyomletea itakuwa umempoteza mteja na atawaambia wengine hivyo hutapata wateja tena watakao nunua bidhaa zako.

Lakini pia mtu mwingine atakwambia amependa bidhaa yako na kwa kuwa umeweka na mwasiliano atakupigia umpelekee hivyo katika hilo vingi hutokea unaweza kuvamiwa, kupigwa na kuibiwa ulivyonavyo kama simu na hizo baidhaa ulizoendanazo kumpelekea mtu huyo.
Na jambo lingine kuna wale watu ambao wezi wa kurasa za watu(account/page) wanaweza kuiba kurasa yako na kuitumia vibaya na wakati wewe ulikuwa ukiitumia kwa mambo ya kibiashara tu, lakini wao wakaweka vitu vingine tofauti au wakaamua kukuchafua wewe na biashara yako na hata muda mwingine kukutaka utoe pesa illi waweze kukuachia kurasa yako ya biashara.

Lakini pia wanaharakati wameshauri ili kuweza kupata maendeleo kupitia Tehama ni vyema kutumia vizuri teknolojia hii kwa kutoa taarifa za ukweli ili unachokitangaza kiendane kweli na ubora wa bidhaa yako ili kujitengenezea mazingira mazuri kwa wateja wako.

Serikali kwa kushirikiana na vikundi vya wanaharakati  kama GDSS kusaidia kusambaza elimu hii  ya matumizi bora ya Tehama na kwa kiasi gani inaweza kutumiwa na wajasiliamali ili kujiletea maendeleo wao na vizazi vya vya sasa na vijavyo.


Tuesday, October 3, 2017

Ushirikina : MZOGA WA KUKU ALIYEFUNGWA SANDA WAZUA GUMZO GEITA

Mzoga wa kuku aliyefungwa na sanda uliokutwa nje ya nyumba ya Emmanuel Kabodi.
Mama Mwenye nyumba Bi,Scolastica Nicodemo akizungumza na mmmoja wa viongozi wa dini waliofika kushuhudia mzoga huo
Wananchi wakishangaa
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye nyumba hiyo.
Wananchi wakiendela kushangaa tukio hilo

*****
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita wamepigwa butwaa baada ya kukuta mzoga wa kuku ukiwa umevishwa sanda kwenye familia ya Emmanuel Kabodi.


Mama wa familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa wakati akifanya usafi aliona kuna kitu kimefungwa na shuka jeupe nyuma ya geti na alipojaribu kukiangalia aligundua ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.

Askofu wa kanisa la TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda ameiasa jamii kuachana na masuala yanasosadikiwa kuwa ni ya kishirikina kwani vitendo hivyo havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .


Mjumbe wa Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata amesema hii ni mara ya pili kutokea kwa tukio hilo kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la kufukuliwa kwa mtoto na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya vitendo hivyo kuachana navyo mara moja kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo hawataweza kumvumilia.

Wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho kinachohusishwa na imani za kishirikina.

Mtaa wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na vitendo vinavyosadikiwa ni vya imani za kishirikiana vya mara kwa mara na kusababisha hofu kubwa kwa watu ambao wanaishi maeneo hayo.
Imeandaliwa na Joel Maduka - Maduka 
online

Tigo yasherekea wiki ya huduma kwa Mteja katika duka la Mlimani City

Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akisaidiana na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti kutoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana.

  1. Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti wakifurahi jambo na mteja wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yameanza jana.


Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola (kushoto) akitoa huduma kwa Happiness Muthali wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Maadhimisho hayo yamefanyika jana katika duka la Tigo Mlimani City jijini Dar.

 Meneja Mawasiliano wa Tigo Tanzania, Woinde Chisel  akijadiliana jambo na Meneja huduma kwa wateja kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Tigo Mwangaza Matotola na msimamizi wa duka la Tigo Mlimani City Joseph Umoti (katikati mapema jana katika duka la Mlimani city.

wateja wakiendelea kupata huduma.

MSANII IZZO BIZNESS WA TANZANIA NA AVRIL WA KENYA WAPAMBA ONYESHO LA COKE STUDIO

Wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wanaendelea kupata burudani ya muziki kutoka wasanii nguli kutoka nchi za Afrika kupitia onyesho la Coke Studio kupitia luninga ya clouds ambapo mwishoni mwa wiki Kolabo ya mwanamuziki kutoka nchini Izzo Business na Avril kutoka Kenya imeacha gumzo kubwa. Wanamuziki wengine waliopagawisha washabiki wa muziki katika onyesho hilo ni Mafizikolo kutoka Afrika ya Kusini kwa kushirikiana na msanii Nyashinski kutoka nchini Kenya na wasanii waalikwa Bill Nas (Tanzania),Sheebab (Uganda) na Asgeg Ashko (Ethiopia). Akiongea juu ya kolabo hili,Izzo Business alisema amefurahi kushirikiana na Avril kimuziki hususani wimbo walioimba pamoja unaojulikana kama 'Kanyonyi Kanja' na 'mabata mabata yanaogelea' ambao umeimbwa kwa lugha ya Kiswahili ukiwa na vionjo vya muziki wa bongofleva. Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca Cola muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika na linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50. Wasanii wa Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness, Nandy na mtengenezaji wa muziki wa studio nguli Nahreel. Wakitoa maoni yao kuhusiana na onyesho hili,baadhi ya wapenzi wa muziki kutoka mikoa mbalimbali wanaolifuatilia walisema kuwa burudani za Coke Studio msimu huu ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa kolabo za wanamuziki zimetengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba zikionyeshwa zinaleta furaha na kumfanya mtazamaji kujiona anaangalia onyesho la wanamuziki hao mubashara (Live).
Mbali na wasanii wa Tanzania,wasanii msimu huu wa tano wa Coke Studio unawajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon Baadhi ya wasanii hao ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya), Sami Dan (Ethiopia), Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda ( Uganda). Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius, Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana. Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.

Monday, October 2, 2017

TAMASHA LA TIGO FIESTA LATIKISA KIGOMA WIKIENDI HII



Wasanii Ben Pol na Jux wakiimba pamoja wimbo wao walioshirikiana ‘Nakuchana’ kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma usiku wa kuamkia jumatatu


Aslay akiburudisha wakazi wa Kigoma





Msanii Chege na Nandy wakiimba pamoja wimbo wao walioshirikiana ‘kelele za chura’kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani  Kigoma usiku wa kuamkia jumatatu.


Darasa akiburudisha wakazi wa Kigoma 


Wasanii Stamina na Maua sama wakiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma

Mr blue akipagawisha umati  wa wakazi wa kigoma 




Msanii wa Bongo flea Ommy Dimpoz akiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma

Roma Mkatoliki akiimba kwenye tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma

Roma mkatoliki akiburudisha umati wa wanakigoma waliojitokeza katika viwanja vya Lake Tanganyika.

Young D akiimba kwa hisia katika jukwaa la Tigo fiesta

Wasanii wa Tigo fiesta watembelea duka la Tigo Tabora


Msanii Ommy Dimpoz akimkabidhi zawadi mteja wa Tigo mkoani, Elizabeth Mremba mkazi wa Kariakoo Kijiweni mkoani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika ofisi za Tigo Tabora baada ya wasanii watakaopanda jukwaa la Tigo Fiesta kutembelea duka hilo mapema wiki iliyopita.

Mfanyakazi wa Tigo, Joyce Maweda akipiga picha 'selfie'na wasanii.
Wasanii wakipiga picha ya pamoja nje ya duka.

MAKONDAKTA NA WAPIGA DEBE MWANZA WAVUNJA UKIMYA

...Mwenyekiti wa umoja huo Mrimi Juma pamoja na Katibu wake Erick Felishian, wanasema umoja umedhamiria kuwa mfano bora katika jamii na kwamba umeanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa baadhi ya Makondakta na Wapiga Debe wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kuwapeleka polisi...
Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza, John Mwakalasya (kushoto) akipokea rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Jijini Mwanza, Mrimi Juma (kulia), kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Nyamagana aliyefiwa na baba yake
Kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza, John Mwakalasya (kushoto) akipokea rambirambi kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Jijini Mwanza, Mrimi Juma (kulia), kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Nyamagana aliyefiwa na baba yake. Wanaoshuhudia ni wanachama wa umoja huo.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Jijini Mwanza wakifanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba kwenye barabara ya Pamba na mitaa mbalimbali ya Jiji hilo
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Jijini Mwanza wakifanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba kwenye barabara ya Pamba na mitaa mbalimbali ya Jiji hilo
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Jijini Mwanza wakifanya usafi jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba kwenye Mnara wa Nyerere na mitaa mbalimbali ya Jiji hilo
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akisalimiana na mmoja wa wapiga debe Jijini Mwanza.
BMG Habari, Pamoja Daima!