Friday, October 6, 2017

Makachero wamtia mbaroni mtoto wa Mbunge huyu

POLISI mkoani Rukwa inamshikilia Bakari Kessy ambaye ni mmiliki wa gari aina ya Fuso lililopinduka na kusababisha vifo vya watu 15 na wengine tisa kujeruhiwa.

Mmiliki huyo wa gari hilo lenye namba za usajili T 425 BFF, ni mtoto wa kiume wa mwanasiasa machachari, Ally Kessy (CCM) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini katika Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Lori hilo lilikuwa limebeba magunia ya nafaka yakiwemo mahindi, lilipinduka na kuua watu 15, wakiwamo wanawake 10 na wanaume watano huku mwenye umri mdogo akiwa mtoto mwenye umri wa wiki mbili na mwenye umri mkubwa akiwa na miaka 84.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema wanamshikilia mmiliki wa gari hilo kwa kuwa dereva wake amekimbia, hivyo ni jukumu lake kueleza alipo, na akishindwa atafikishwa mahakamani kwa kosa la uzembe wa kutotunza kumbukumbu za dereva wake.

Inasemekana devera wa gari hilo anayetafutwa na polisi baada ya kubaini kuwa gari limemshinda, aliruka kupitia dirishani na kulicha likiwa na abiria likienda kwa mwendo kasi na kugonga mwamba kisha kupinduka.

“Kweli tunamshikilia mmiliki wa gari lililosababisha ajali Bakari Kessy ili atuoneshe alipo dereva kwa kuwa yeye ndiye anayetunza kumbukumbu zake akishindwa basi tutamfikiza mahakamani,” alieleza Kamanda Kyando.

Aidha, alieleza kuwa maiti 14 kati ya 15 zimetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya maandalizi ya maziko yao isipokuwa mwili wa marehemu Abuu Amani (37) mkazi wa mkoani Kigoma haujachukuliwa na ndugu zake.
Makachero wamtia mbaroni mtoto wa Mbunge huyu
Miili iliyotambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao ni Domona Tenganamba (41), Emmanuel Rashid (84), Restuta Sunga (35), Salula Revana (64), Felisia Tenganamba (1), Prisca Madeni (45), mwalimu wa shule Richard Chikwangara (24), Yusta Somamabuto (36), Grace Ramadhan (24), Odetha Madirisha (46), Megi Nalunguli (52), Nyandindi Batrahamu (35) na mtoto mwenye umri wa wiki mbili ambaye alikuwa hajapewa jina.

Kwa mujibu wa Kamanda Kyando, ajali hiyo ilitokea Oktoba 3, saa tisa alasiri na gari hilo lilikuwa likitokea Sumbawanga Mjini kwenda Kijiji cha Wapembe wilayani humo. Alisema dereva huyo ambaye jina lake halikufahamika amekimbia kusikojulikana muda mfupi baada ya ajali hiyo, huku chanzo kikielezwa kuwa ni mwendokasi.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amepiga marufuku magari ya mizigo kubeba abiria huku akimwagiza Kamanda wa Polisi kufuatilia kwa karibu. Alishauri kuwa kama tatizo ni uhaba wa magari ya abiria, basi magari maarufu kama “chai maharage” yaanze kutoa huduma za kusafirisha abiria vijijini

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MANJI KESI YA DAWA ZA KULEVYA

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam imemwachia huru mfanyabiashara, Yusuf Manji katika kesi ya dawa za kulevya iliyokuwa inamkabili.

Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha amesema upande wa mashitaka ameshindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi yake.

Taarifa muhimu ya TCU kwa wanafunzi waliokosa vyuo

TAARIFA KWA UMMA
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inautangazia  Umma kuwa  awamu ya kwanza ya Udahili wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo ya shahada za awali ulimalizika tarehe 30 Agosti 2017. 

Tume inawaarifu kuwa imekamilisha zoezi la uhakiki wa majina ya waombaji wote walioomba kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo wa 2017/18.
 
Hata hivyo kutokana na  waombaji wengi  kutochaguliwa  kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 4 hadi 10 Octoba 2017 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili:
  
•  Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza;
•  Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika  awamu ya kwanza;
•  Waombaji wenye vigezo vya Stashahada  walioshindwa kupata Namba ya Uhakiki wa Tuzo (AVN);
•  Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge”  mwaka 2017 na matokeo yao yameshatoka; na
•  Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitsho toka vyuo vyao vya awali.
  
Aidha Tume inapenda kusisitiza kuwa utaritibu wa kutuma 
maombi ni ule ule uliotumika katika awamu ya kwanza ya Udahili. 
  
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni 
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
4 Oktoba 2017  

COCA-COLA YAJA NA PROMOSHENI YA ‘MCHONGO CHINI YA KIZIBO’

Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi (katikati),akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo.Wengine pichani ni Maofisa Waandamizi wa kampuni hiyo
 Kikosi kazi cha timu ya mauzo ya Nyanza Bottlers katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Mchongo chini ya kizibo
Msafara wa magari ya kampuni ya Nyanza Bottlers yakipita mitaani katika mji wa Mwanza wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo
Kampuni ya Coca-Cola, imezindua kampeni kubwa ya wiki 10 kwa wateja wake inayojulikana kama ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ ambayo itawawezesha wateja wake wa mikoa ya kanda ya ziwa na jirani kujishindia zawadi nono za fedha taslimu zaidi ya milioni 400,bodabado 100,televisheni 60 aina ya SONY LED zenye inchi 32,T-shirts , kofia na soda za bure. Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kiwanda cha Nyanza Bottlers, Japhet Kisusi, alisema lengo la promosheni hii ni kuleta msisimko zaidi kwa wateja wanywaji wa soda zote zinazozalishwa na kampuni ya Coca-Cola waliopo mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, na mikoa mingine jirani ya kanda ya ziwa. “Kampuni yetu ya Coca-Cola katika kutoa shukrani kwa wateja wetu wanaotuunga mkono tumekuwa tukifanya promosheni mbalimbali zenye lengo la kuleta furaha na kubadilisha maisha yao kupitia Coca-Cola na promosheni ya ‘Mchongo Chini ya Kizibo’ tunayoizindua leo. Kwa kunywa soda aina yoyote inayozalishwa na kampuni ya Coca-Cola wataweza kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu, bodabado, televisheni aina ya SONY LED zenye inchi 32, T-shirts , kofia na soda za bure.” Alisema Kisusi. Alisema ili mteja kujishindia zawadi atabandua kiambatanisho laini kilichopo chini ya kizibo cha soda. Kwa upande wa fedha taslimu kuna zawadi za shilingi 5,000/-, 10,000/- na 100,000 na zaidi ya shilingi milioni 400/- zimetengwa kwa ajili ya kushindaniwa na wateja, ambapo kwa upande wa zawadi ya bodaboda anachotakiwa kufanya mteja ni kukusanya vizibo vitatu vyenye picha zinazokamilisha picha ya bodaboda – kuonyesha upande wa Nyuma, Katikati na Mbele. Kisusi aliongeza kuwa pia zawadi nyinginezo za Televisheni, kofia, T-shirt na soda za bure zinapatikana chini ya kiambatanisho laini chini ya kizibo kama zilizvyo zawadi kubwa. “Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia promosheni hii ili waendelee kuburudika na soda zinazotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola sambamba na kunufaika kwa zawadi za kuleta furaha na kuboresha maisha yao, familia zao na wapendwa wao.” Kuhusu jinsi ya kupata zawadi alisema kuwa zawadi zote kwa washindi zitatolewa bila urasimu wa aina yoyote kuanzia kwenye maduka ya rejareja, mawakala maalumu wa kusambaza vinywaji vya kampuni ya Coca-Cola na kwenye kiwanda cha Nyanza Bottlers. Soda za kampuni ya Coca-Cola ambazo zitakuwa na zawadi kwenye ganda la vizibo ni Coca-Cola, Fanta, Sprite, Tangawizi, Sparleta na Novida.

WADAU WA ELIMU WAKUTANISHWA KUJADILI MAZINGIRA YA MWALIMU SHULENI.

Mtandao wa Elimu (TEN/MET)  kwa kushirikiana na Action Aid Tanzania wawakutanisha walimu kutoka mikoa yote ya Tanzania ili kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto zinazorudisha nyuma au kukwamisha jitihada zao za kutoa elimu bora nchini.

Meneja Miradi wa Mtandao huo, Mwalimu  Alistidia Kamugisha (wa kwanza kulia) Akizungumza na waandishi wa habari juu ya Kongamano hilo.
Akizungumza wakati wa utambulisho na lengo la kongamano hilo maalumu katika siku ya Mwalimu duniani, Afisa  miradi ya  mtandao huo Mwl. Alestidia Kamgisha alisema walimu wanachangamoto nyingi ambazo zisipotatuliwa zitaendelea kushusha ubora wa elimu kutokana na kuporomoka kwa hali ya mwalimu kufundisha.

“kukutana  kwao kwa pamoja kutasaidia kila mmoja kusikia changamoto na mafanikio ya mwalimu mwenzake kutoka mkoa mwingine lakini pia kujifunza kwa walimu wengine waliofanikiwa wakiwa ndani ya changamoto hizo”, alisema Kamugisha.


Pia Afisa  Miradi huyo wa mtandao wa elimu Tanzania aliongeza kuwa mawazo ya pamoja kutoka kwa wadau hao yatasaidia katika kubuni mbinu za pamoja kama wadau ili kusaidia kutatua chaangamoto hizo  na kurudisha nguvu ya mwalimu katika kufundisha na kufaulisha.


Aidha akieleza hali ya shule yake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura  alisema kuwa shule yake inawalimu watano tu lakini inazaidi ya wanafunzi 1000 idadi ambayo ni kubwa sana kwenye uwiano kati ya mwalimu mmoja na mwanafunzi.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyandira mwalimu Atulinda Musebura.


“hali hii inatulazimu kufundisha kwakuelekeza nguvu kwa darasa la saba ili kuwawezesha wanafunzi hao kufaulu mitihani yao ya mwisho na wanapoondoka nguvu zetu tunazielekeza kwa darasa la nne ambao nao wanakuwa na mtihani wa Taifa, 

 Hali hiyo inawanyima wanafunzi wengine kwenye nyakati Fulani kukosa masomo na hata kuwatesa walimu hao kwa kufanya kazi kupita uwezo wao na mwalimu anapopata dharura hali huwa mbaya zaidi kwani walimu hao kila mmoja anavipindi zaidi ya 67 kwa wiki badala ya 40”,alisema Musebura.


Kwa upande wake muwezeshaji kwenye kongamano hilo bwana Zelote Loilang’akaki alisema mkakati wa serikali kutoa elimu bure umesaidia kuwepo kwa ongezeko kubwa la wanafunzi mashuleni  lakini swala la ongezeko la walimu halikuzingatiwa hivyo kuwafanya walimu kuzidiwa na mzigo wa  kazi ya ufundishaji.
Muwezeshaji wa kongamano hilo Bwana Zelote Loilang’akaki akizungumza na washirki hao 


“Changamoto ya upungufu wa walimu umekuwa mkubwa kwa shule za msingi wakati wa idadi ya walimu wa Sayansi ikibaki kuwa ndogo kwenye shule za secondary  kwamfano kuna upungufu wa walimu wa Sayansi 64 sekondari wakati msingi kunaupungufu wa walimu 614 kwa mujibu wa ripoti za TEN/MENT kwa wilaya ya Mvomero pekee”, alisema Loilang’akaki.

Pia alibainisha kuwa kwa mujibu wa serikali idadi ya walimu imeongezeka  kufika 165,856 mwaka 2010 hadi 2011 hadi kufika 190,957 mwaka 2014 hadi 2015. 

Taarifa za chama cha walimu Tanzania (CWT) zinaonyesha nchi inaupungufu wa walimu 100,000 kwa shule za msingi 500,000 shule za sekondari ambapo walimu wa Sayansi 30,000 na sanaa 20,000 huku taarifa za elimu ya msingi (BEST 2016) zinaonyesha upungufu ni walimu 7291 wa hesabu 5118 Biology 5375 kemia 6873 walimu wa fizikia.

Siku ya walimu duniania mwaka 2017 imebeba ujumbe usemao “mwalimu anastahili mazingira bora na huru ya kufundishia: kodi anayolipa itumike kwaajili ya kumjengea uwezo na kuboresha mazingira yake”.  

Bwana Prosper Lubuva Mkuu wa Idara ya Elimu na Mafunzo (CWT) akiwasilisha mada juu ya mapendekezo ya Shirika la kazi duniani na ILO na UNESCO kuhusu hali ya walimu ya mwaka 1966.

 
Mwalimu akiwa amefungwa kitambaa na kuagizwa kitu ukumbinu hapo ikiwa ishara ya kuona changamoto na vikwazo anavyokutana  navyo Mwalimu kwenye kufikia malengo yake ya kufundisha na kufaulisha.




 
Wadau hao wakifuatilia mada ya mapendekezo ya hali ya mwalimu duniani.


  
Baadhi ya wadau hao wa Elimu wakifuatilia kongamano hilo.

Thursday, October 5, 2017

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, yatoa msaada wa vifaa vya intaneti kwa shule za mkoa wa Njombe leo

Mkurugenzi wa Tigo Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga (kushoto) Mkuu wa wilaya Wanging'ombe Ally Kasinge Katikati) Mkuu wa shule ya Sekondari Njombe Benard William  wakikata utepe kufungua kufungua  darasa la kusomea wanafunzi kwa njia ya mtandao. Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Ally Kasinge (kulia) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe akipokea kifaa cha kupokelea mawimbi ya intaneti kutoka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga,   msaada huo umtolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa ajili ya Shule ya sekondari Njombe.

Mkuu wa Wilaya Wanging'ombe Ally Kassinge (wa pili kushoto) akipata maelekezo ya matumizi ya kompyuta zinazo tumia mtandao wa Intanet toka kwa mkurugenzi wa Tigo kanda ya Nyanda za juu kusini Jackson Kiswaga katika Darasa la wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe, Msaada huo umetolewa jana na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo mkoani Njombe.

ZIJUE SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA SARATANI YA MATITI

Na Jumia Travel Tanzania

Saratani ya matiti ni miongoni mwa saratani inayomkumba zaidi mwanamke duniani na ndiyo inayoongoza kwa vifo vinavyotokana na saratani katika nchi zinazoendelea, ambapo watu takribani milioni 1.7 mwaka 2012 waligundulika kuwa na ugonjwa huo (kwa mujibu wa taarifa zilizopo hivi sasa). Viwango vya saratani duniani kwa ujumla vinatarajiwa kuongezeka kutoka milioni 14 mwaka 2012 na kufikia milioni 20 ndani ya miongo miwili ijayo, na kuifanya saratani kuwa ugonjwa unaotakiwa kuchukuliwa tahadhari zaidi.      

Mwezi Oktoba wa kila mwaka dunia huwa imeutenga mahususi katika kukuza uhamasishaji wa kupambana na ugonjwa wa saratani ya matiti duniani. Kampeni hizo huungwa mkono na serikali, taasisi na mashirika mbalimbali duniani kwa kuangazia umuhimu wa kuhamasisha juu ya saratani ya matiti, kutoa elimu na kufanya tafiti. Miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika mwezi huu ni pamoja na kukuza hamasa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo na kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanyia tafiti toauti za ugonjwa huo.

KAMANDA MAMBO SASA ANENA HAYA KUTOKANA NA TUKIO LA WATU 10 KUFA BAADA YA KUNYWA GONGO ENEO LA KIMARA

Watanzania wameshauriwa kutumia vinywaji vilivyothibitishwa na shirika la viwango Tanzania (TBS) ili kuepukana na matatizo yanayopatikana katika vinywaji hivyo kwa kuwekwa vitu kama sumu na hata madawa mengine yasiyofaa kwa bidamu katika utengenezaji wa vinywaji hivyo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam ndugu Lazaro Mambosasa alipokuwa akitoa ripoti ya watu kumi waliofariki baada ya kunywa kinywaji aina ya gongo maeneo ya kimara jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda Mambosasa alisema kuwa upelelezi wa awali unaonyesha kuwa waliofariki ni 10 na siyo 19 kama vyombo vya habari vilivyoripoti jana na eneo la tukio ni Kimara stop over na muuzaji alikuwa ni marehemu mama Anoza na katika eneo la tukio zilikutwa chupa 3 za ujazo wa lita moja moja inayodhaniwa ni pombe ya moshi(gongo).

Aidha kamanda huyo alieleza kuwa watu hao waliofariki ni Maleo Ramadhani mwenye umri wa miaka 45 ambae alifariki baada ya kupelekwa mwananyamra hospitali na alipopata nafuu alirudi nyumbani na ndipo umauti ulipomkuta , na wapili ni mmasai aliyefahamika kwa jina moja la Yona anayekadiliwa kuwa na miaka 20 hadi 30 alikuwa mlinzi wa getini kwa jamaa aliyeitwa Paula Kisanga mkazi wa Kimara stop over.
Na taarifa nyingine zilizopatikana zinaonyesha kuwa kuna watu wengine nane waliofariki dunia kwa kunywa pombe hiyo na miili yao ipo Mwananyamara na  hospitali ya Tumbi Kibaha Mohamedi Issa miaka 67 mkazi wa Kiamra Saranga, Kabugi Rashid miaka 64 mkazi wa Saranga, Stanslaus Joseph miaka 58 Kimara Saranga, Stephen Isaya miaka 61 Kimara Saranga, Monica Rugaillukamu miaka 42 mkazi wa Kimara Saranga, Alex Madega miaka 41 mkazi wa Kimara Korogwe, Hamisi Mbala miaka 35 mkazi wa Kimara Golani, Eksoni Nyoni miaka 28 mkazi wa Kimara stop over,


Lakini pia vielelezo vyote vinapelekwa kwa mkeamia mkuu ikiwa ni chupa na miili ya marehemu hao ili kufanyiwa uchunguzi na kubaini chanzo halisi cha vifo hivyo, na huku jeshi la polisi likifanya msako mkali kumbaini aliyewauzia pombe watu hao,

WATU WASIOJULIKANA WATEKELEZA MAUAJI KWA MTOTO MDOGO SOMA HAPA KUJUA ZAIDI

Mtoto mwenye umri wa miezi kumi Arman Hassan Mohamedi, ameuawa na watu wasiojulikana katika eneo la Fuoni lililopo mkoa wa Mjini Magharibi Unguja visiwani Zanzibar, na kisha kumtumia ujumbe mama mzazi wa mtoto huyo.
Wasiojulikana waua tena
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Maghari Unguja, Hassan Nasir, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 3, ambapo mtoto huyo aliuawa na kisha kutumbukizwa kwenye dumu la maji la lita 60, na kulitelekeza nyumbani kwao.

“Upelelezi wa awali unaonyesha aliuawa na mtu ambaye hajafahamika bado, tunasema ameuwawa kwa sababu alikuwa alikuwa nje na watoto wenzake wakicheza, baada ya muda akatoweka, akatafutwa sehemu mbali mbali hadi vituo vya polisi, lakini kwenye saa moja na nusu akaonekana akiwa kwenye dumu la maji la lita 60 akiwa ndani amekufa, lakini kuna message alitumiwa mama wa mtoto kwamba mtoto wako atapatikana akiwa maiti, na nyingine ikimpa pole kwa msiba”, amesema Kamanda Nassir.

Kamanda Nassir amesema Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea kuchunguza kwa kufuatilia messgae hizo ili kuwabaini waliofanya mauaji hayo, aliyoyaita ya kikatili na kuwachukulia sheria stahiki

SIMBANET KUTANGAZA FURSA KWA VIJANA WATANZANIA

TANZANIA ikiwa  kwenye mapinduzi ya kiteknolojia ilhali  inadaiwa kuwepo kwa changamoto ya ajira ambapo mapunduzi hayo yanaweza kutoa fursa zaidi.

Fursa hizo zimeelezwa kuwa zipo kwenye teknoljia endapo vijana hao watajitambua kwa kufanya kazi vizuri katika kuitumia mitandao ya kijamii kwa ufanisi.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa  Operesheni  kwenye mtandao wa Simba Net wa Tanzania Kenya na Uganda, Hussein Kitambi, amesema kuwa Simba Net itawakutanisha vijana  100 watakao funguliwa fikra ya jinsi Teknolojia inavyoweza kuwasaidia kujipatia ajira,
 
Amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika kesho jijini Dar es Salaam katika  Ofisi za  Umoja wa Mataifa ambapo Simba Net ikishirikiana na wadau mbalimbali wa Teknolojia.

Wednesday, October 4, 2017

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA UDSM 2017/18

Home 

LIST OF APPLICANTS SELECTED TO UNDERTAKE POSTGRADUATE STUDIES FOR 2017/2018 ACADEMIC YEAR – FIRST AND SECOND BATCH



For more information click HERE

SHIRIKA LA WOTESWA LAWANOA WAANDISHI WA HABARI JIJINI MWANZA.



Amesema hatua hiyo itasaidia kuwanusuru watoto wafanyakazi wa majumbani na ukatili ikiwemo wa kingono pamoja na kiuchumi ambapo baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi bila malipo ama kwa malipo kidogo.

Aidha ametoa rai kwa serikali kuboresha sera, mikakati na sheria zinazomlinda mtoto ili kuondoa mkanganyiko uliopo ambao unashindwa kutambua bayana umri wa mtoto anayepaswa kuajiriwa kwani baadhi hutaja umri wa miaka 14 huku nyingine ikitaja umri wa miaka 18.

Nyangasi amebainisha kwamba mwaka jana shirika la WoteSawa lilifanya utafiti katika Kata nne za Jiji la Mwanza ambazo ni Igogo, Mkuyuni, Butimba na Capriont na kubaini kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na utumikishwaji na ili kupambana na hali hiyo shirika hilo lilianzisha mkakati wa kuwafikia watoto waajiriwa, waajiri wao pamoja na viongozi wa serikali za mitaa na kuwaelimisha.

Nao waandishi wa habari, Moses Mathew kutoka gazeti la Daily News pamoja na Rhoby Magira kutoka Redio Afya wamebainisha kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuandika habari na makala zinazoielimisha jamii ili kuondokana na mazoea ya kuwatumikisha watoto kupitia ajira za majumbani.

Itakumbuka kwamba mtoto mfanyakazi wa nyumbani analindwa na sheria kadhaa ikiwemo sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009, sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, waraka wa mishahara wa mwaka 2013 pamoja na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa upande wa waraka wa mishahara wa mwaka 2013, mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni ingwa waraka huo hautaji mwajiriwa huyo anapaswa asiwe mtoto.

Mkufunzi Dotto Bulendu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augostino cha Jijini Mwanza, akisisitiza wanahabari kuungana pamoja katika kuibua na kuandika habari/ makala zenye kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani
Afisa Habari shirika la WoteSawa akizungumza kwenye mafunzo hayo
Mwanahabari Moses Mathew kutoka gazeti Daily News akichangia mada kwenye mafunzo hayo

WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA 2017: WATEJA NA WANACHAMA WA PSPF WAPATIWA HUDUMA ZA ZIADA

 Faiza Masoli, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
WATEJA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wanaofika kwenye ofisi za makao makuu jengo la Jubilee Tower jijini Dar es Salaam ili kujipatia huduma katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma Kwa Wateja Duniani, wamekuwa wakifaidika na huduma za ziada zinazotolewa na washirika wa Mfuko huo ambao wameweka kambi kwenye eneo hilo.
Washirika wa Mfuko  walioweka kambi kwenye ofisi hizo tangu Otoba 2, 2017, ili kuwahudumia wateja ambao ni pamoja na Wastaafu na Wanachama wa PSPF ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), Benki ya CRDB, Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Benki ya NMB na  Mwalimu Commercial Bank Plc (MCB), Menenja wa Huduma kwa Wateja wa PSFP, Bi. Laila Maghimbi amesema.
“Kama mnavyoona, mwaka huu tumeamua kuongeza huduma za ziada kwa wateja wetu, yaani wastaafu na wanachama wanaofika kupatiwa huduma ofisini kwetu, ambapo Mteja baada ya kuhudumiwa pia anaweza kuonana na washirika wetu, ambapo NHIF wanafanya uchunguzi wa afya bure, mabenki nayo yapo hapa kuwaelimisha kuhusu jinsi wanavyoweza kuweka fedha zao na kupatiwa mikopo nafuu ili kuendesha miradi  mbalimbali na hivyo kujiongezea kipato.” Alifafanua Bi. Maghimbi.
Alisema, nia ya Mfuko ni kuhakikisha wanafurahia huduma zitolewazo lakini pia kuonyesha kuwajali wateja wao kwa kuwasogezea karibu huduma muhimu za afya na kibenki.
Wateja wamekuwa wakifurika kwenye ofisi hizo tangu Wiki ya Huduma kwa Wateja ianze Oktoba 2, 2017 na miongoni mwa huduma zitolewazo ni pamoja na wastaafu kufuatilia taarifa za michango yao, kuhakikiwa, kulipwa mafao na kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS).
Aidha wanachama wanaofika kwenye ofisi hizo wamekuwa wakipatiwa maelezo ya namna wanavyoweza kupatiwa mikopo ya viwanja na nyumba za makazi ambapo kampuni mshirika ya PSPF, Ardhi Plan Limited kupitia afisa wake, Bi.Anna Lukindo imekuwa ikifanya kazi hiyo.

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa pspf, Bw, Andrew Mkangaa, (wapili kulia), Meneja wa Huduma kwa Wateja, Bi. Laila Maghimbi, (watatu kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward(kulia), wakimsikiliza Daktari kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), kuhusu huduma wazitoazo kwa Wateja na wanachama wa PSPF kwenye ofisi za Mkao makuu ya Mfuko katika kipindi hiki cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
 Maafisa wa Benki ya CRDB, Afisa Uendelezaji Biashara, Bw. Peter Christopher, (wapili kulia), na Afisa Mikopo kwa watumishi, Bi.Diana Jekela, (kushoto), wakiwahudumia wateja.
 Afisa wa Benki ya NMB GTawi la Sinza jijini Dar es Salaam, Bi. Nadina Mpasha, (kulia0, akimpatia maelezo mteja aliyefika kwenye banda la benki hiyo kwenye ofisi za PSPF.
Dkt. Jason B.B Bagonza, (kushoto), ambaye ni Mchumi Mkuu kutoka Idara ya uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha na Mipango, akihudumiwa na maafisa wa benki ya Posta Tanzania, (TPB), Maafisa Masoko,  Bi. Heavenlight A.Uiso na Bw.Nelson Mwakilasa
 Maafisa wa Mwalimu Commercial Bank, (MCB), Plc, Mwajuma Gilbert, (kulia) na Michael Kachala, ambao ni maafisa wan huduma kwa wateja, wakitoa huduma.
 Faiza Masoli, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
 Bi.Valley Malinga, Afisa kitengo cha simu (Call Centre), cha PSPF, akiwa kazini.
 Afisa Huduma kwa wateja, PSPF, Bi.Elizabeth Shayo.
 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akipitia taarifa za Mteja aliyefika kuhudumiwa
 Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Ndani wa PSPF, Bi. Costantina Martin, akizungumza na mteja huku akimuonyesha taarifa yake.
  Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akiwaeleza wateja hawa wa Mfuko huo, kuhusu huduma za ziada zinazopatikana kweye eneo hilo.
 Afisa wa PSPF(kulia), akimpatia nyaraka Mwanachama huyu aliyefika kuhudumiwa kwenye ofisi hizo.
 Anna Lukindo, (kulia), kutoka kampuni ya Ardhi Plan Limited, akimpatia maelezo Mwanachama wa PSPF aliyetaka kujua ni jinsi gani anaweza kupatiwa mkopo wa kiwanja.
 Wanachama kushoto, wakihudumiwa na maafisa wa PSPF ambao wako makini katika kuwahudumia wateja wanaofika kwenye ofisi hizo.
 Maafisa waandamizi wa PSPF, Bw. Gabriel P.Maro, (kushoto) na Bw. Abdul Njaidi wakifurahia jambo