Friday, February 26, 2016

TIGO YAFIKISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA 4G LTE MOSHI

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (katikati)  akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma ya 4G LTE jijini Dodoma, kushoto ni Meneja wa huduma ya 4G LTE, Benedict Mponzi na kulia kwake ni Meneja Masoko wa kanda ya kaskazini  Kephar Kileo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo mjini Moshi.

SDL KUMALIZIKA WIKIENDI HII


Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajiwa kumalizika wikiendi hii kwa michezo 12 kuchezwa katika makundi ya A, B, C & D katika viwanja mbalimbali nchini, huku kila kundi likitoa timu moja ya juu itakayocheza fainali za kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Kesho Ijumaa, michezo mitatu ya kundi C itachezwa katika raundi hiyo ya mwisho, Villa Squad watacheza dhidi ya Mshikamano (Mabatini, Mlandizi), Abajalo Dar v Karikaoo FC (Karume) na Changanyikeni watakuwa wenyeji wa Cosmopolitan katika uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha.
Kundi A, Jumamosi Green Warriors watawakaribisha Abajaro Tabora katika uwanja wa Mabatini Mlandizi, Transit Camp watakua wenyeji wa Mvuvumwa uwanja wa Kambarage Shinyanga, huku siku ya Alhamis Singida United watacheza dhidi ya Mirambo uwanja wa Namfua mjini Singida.
Jumamosi Kundi C, Alliance Schools watakua wneyeji wa Bulyankulu katika uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watacheza dhidi ya  Pamba FC uwanja wa Karume Musoma, na Madini FC watakua wenyeji wa AFC Arusha uwanja wa Mbulu.
Kundi D, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Wenda FC uwanja wa CCM Mkamba, Sabasaba watakua wenyeji wa The Mighty Elephant uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, huku Mbeya Warriors wakicheza dhidi ya African Wanderes katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Timu moja ya kwanza kutoka katika kila kundi zitacheza hatua ya Fainali Machi 7-14, 2015 uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, ili kupata timu tatu za juu zitakazopanda moja kwa moja ligi daraja la kwanza (StarTimes League) msimu ujao.

Habari24 Blog yapaa kimataifa--HEINEKEN waonyesha kuguswa nayo

Meneja Mkuu wa Bia ya HEINENEKEN Tanzania Michael Mbungu (kulia) akimkabidhi mkurugenzi na mmiliki wa mtandao wa habari24 blog EXAUD MTEI maarufu kama Msaka Habari moja kati ya zawadi nyingi ikiwa ni shukrunani ya ushirikiano wa makampuni hayo mawili kibiashara kwa mwaka jana,katika hafla ambayo iliandaliwa maalum kwa ajili ya kushukuru na kufungua mwaka mpya wa kibiashara zaidi kwa makampuni hayo mawili

MAJALIWA AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNHCR NCHINI


majil1

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR), Bi. Joyce Mends- Cole, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 26, 2016. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
majil2

KAMPUNI YA MAWASILIANO YA TIGO YATOA MSAADA WA FEDHA ,KIASI CHA SHILINGI MIL TANO NA VIFAA VYA MICHEZO KWA WATOTO WA KITUO CHA AMANI CENTER CHA MJINI MOSHI.



Meneja wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 5 afisa uhusiano wa kituo cha kulea watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Amani Center ,Kampuni ya Tigo imetoa kiasi hicho cha fedha pamoja na vifaa vya michezo kwa ajili ya maandalizi ya mbio za Kilimanjaro Marathoni.
Meneja wa kampuni ya Tigo Kanda ya Kaskazini,Henry Kinabo akikabidhi fulana kwa watoto waishio katika mazingira magumu ya Kituo cha Aman Center cha mjini Moshi.
Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini ,Henry Kinabo akifurahia jambo na afisa uhusiano wa kituo cha kulelea watoto waishio katika mazingira magumu cha Amani Center ,Salma Khatibu,wengine ni watoto waishio katika kituo hicho.
………………………………………………………………………………………………………..

Wednesday, February 24, 2016

CUF Watoa Tamko Zito Kuhusiana Na Kukamatwa Kwa Mwanamkakati wa Maalim Seif

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wiki iliopita, mnamo tarehe 16 Februari, 2016, aliyekuwa mjumbe wa Timu ya Kampeni ya Chama Cha Wananchi (CUF), Ndugu Mohamed Ahmed Sultan Al-Mugheiry (maarufu kwa jina la Eddy Riyami), alipokea barua ya wito kutoka kwa Jeshi la Polisi Zanzibar ikimtaka kufika Makao Makuu ya Polisi, Ziwani, Zanzibar siku inayofuata, yaani tarehe 17 Februari, 2016, saa 2 asubuhi kwa kile kilichoelezwa kwamba “kuna mambo muhimu yanayomhusu” ambayo walitaka kuzungumza naye.

Mgambo wasio waadilifu kushughulikiwa


675  mashujaa Mgambo
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Kutokana na tabia ya baadhi ya mgambo katika Halmashauri za Jijini la Dar es Salaam kujipatia fedha kwa njia zisizo za halali, serikali kupitia Halmashauri zake imejipanga kuwachukulia hatua za kisheria migambo wote watakaobainika kujishirikisha na vitendo vya rushwa.

Akitoa ufafanuzi juu ya madai ya wanachi juu ya mgambo wanaochukua rushwa nje ya faini halali zinazistahili kutozwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala, Afisa Habari wa Manispaa ya Ilala Tabu Shabibu amesema kuwa zipo baadhi ya taarifa wamepewa na watawachukulia hatua kwa kuwasitishia mikataba wale wote watakaobainika kukiuka sheria na taratibu za kazi.

Tuesday, February 23, 2016

WAKULIMA WILAYANI RORYA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPATA HUDUMA ZA UGANI KWA NJIA YA SIMU



Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Rorya, Dominick Ndentabura akizungumza na wakulima hao kabla ya kuanza kwa semina hiyo.
Wakulima wa Rorya wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mkulima Sophia Charles kutoka Kijiji cha Roche akizungumzia changamoto ya ukosefu wa soko la zao la mhogo ambapo wanategemea zaidi soko nchini Kenya.
Mkulima Charles Ruola akizungumzia changamoto ya kilimo cha mahindi.

TFF, KTA ZAZINDUA PROGRAMU YA MAENDELEO YA SOKA KWA WANAWAKE


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Taasisi binafasi ya Karibu Tanzania Association (KTA) kwa pamoja wamezindua programu ya maendeleo ya soka kwa wanawake vijana ili kuhamasisha usawa wa kijinsia, uwezeshaji kijamii na kiuchumi kwa wanawake nchini itakayofadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka nchini Sweden.

Monday, February 22, 2016

Meya wa kinondoni na DC MAKONDA kuna kitu kinaendelea,Soma kauli ya meya huyo hapa


Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amemuonya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuacha tabia ya kuingilia majukumu ya Halmashauri, badala yake afanye kazi zinazomuhusu.

KATIBU MKUU BAWACHA AZINDUA RASMI OFISI MPYA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOANI MWANZA.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake
Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.
 
Akizungumza katika Uzinduzi huo, Tendega alipongeza uwepo wa ofisi hiyo ambayo itakuwa ikisikiliza kero za wananchi bila kujalisha itikadi zao za kisiasa kwa ajili ya kupokea hoja za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo kuzisemea bungeni.
 
“…Kazi ya Mbunge siyo kugawa hela. Kazi ya Mbunge ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Na mimi niseme nitakuwa mwakilishi bora na hapa tumeanza tu ambapo katika ofisi hii nitakuwa napokea na kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuzisemea bungeni… Alisema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele.
Ofisi hiyo inapatikana Mtaa wa Ghana Green View, Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza. Ndani yake pia kuna Ofisi ya BAWACHA Mkoa wa Mwanza.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele. Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akiwa pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).

DK SHEIN AZUNGUMZA NA UVCCM MKOA WA MJINI

ccm1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Jumuiya ya Umoja wa Vijana UVCCM Mkoa wa Mjini kichama leo katika ukumbi wa CCM Amani Mjini Unguja na kuwataka Vijana kulinda Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar,ikiwa ni katika hatua za uimarishaji wa Chama cha Mapinduzi,[Picha na Ikulu.]

KIKWETE AZINDUA OFISI YA CCM WILAYA YA KIBAHA MJINI LEO

kib1
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akizindua Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha mjini mkoani Pwani leo. Ofisi hiyo imejengwa na familia ya Mbunge wa Kibaha mjini Slyvester Koka (kulia). (Picha na Bashir Nkoromo).