Thursday, November 6, 2014
HAWA NDIO WATANGAZAJI WALIOTAJWA KUTAKA KUTUMIWA NA IKULU KUURUBUNI MCHAKATO WA KATIBA
KATIBU mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa amefanikiwa kupata waraka kutoka ndani ya Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete ambapo Waraka huo umetenga kiasi cha Sh Bilioni 2.5 kwa ajiri ya kuvionga vyombo vya Habari na waandishi na watangazaji ili kuipigia Kampeni Katiba ilyopendekezwa,
Waraka huo ambao mtandao huu unao unawaonyesha watangazaji kutoka Tv mbalimbali nchini, ambao ikulu ya Rais Jakaya kikwete imepanga kuwanunu ili kufanya kazi ya kuongoza vipindi mbalimbali nyenye lengo la kuwafosi wananchi waipigie kura ya ndio wakati wakuipigia kura katiba iliyopendezwa.
Dokta Slaa aliufichua waraka huo juzi Jijini Dar Es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam ambapo Kwa mujibu wa Waraka huo kila mtangazaji wa kituo cha TV ambaye ataongoza kipindi kimoja atapewa kiasi cha sh laki mbili (200000) kwa kila kipindi ndani ya wiki 22 yaani katika wiki moja kipindi kitaruka mara mbili kwa wiki na wananchi wataruhusiwa kupiga simu.
Waraka huo umewataja watangazaji wa vituo vya TV ambao watanunuliwa,Natha Chingu ambaye ni Msimamizi wa Vipindi wa redio ya East Afrika ambayo yeye atakuwa mtangazaji wakipindi cha Katiba ndani ya Runinga ya EATV pamoja Samson Charlses kutoka kituo cha Tv EATV,
Kwa upande wa kituo cha Runinga cha ITV ni watangazaji hao ni Abdallah Mwipaya,Fatuma Shangasa,Ramphedi Mwasako.Wote hao kutoka ITV,
Waraka huo uliwataja watangazaji wengine walionunuliwa kutoka Kituo cha Tv cha Chanel Ten ni David Ramadhani na katika Shirika la Utangazaji la Serika TBC ni Shabani Kissu.
Pia Kituo cha Tv cha Star Tv ni Mzee Angalieni Mpendu na Francic Mawalla na waraka huo umeshindwa kuwataja watangazaji wa vituo vya ZBC pamoja Clauds Tv ambao wamenunuliwa ili kuipigia kampeni katiba iliyopendekezwa,
MAKUBWA YAANZA KUIBULIWA SAKATA LA MAKONDA,ELIMU YAKE KUMBE NI----SOMA HAPA
Na Karoli Vinsent
HUKU ikiwa bado wasomi,wanasiasa na wanaharaki pamoja na taasisi mbalimbali zikiwa zinalaani vikali kitendo cha wahuni waliokodiwa na aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Paul monda kuvuruga na kupigwa aliyekuwa
Mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji Maoni ya Katiba mpya Jaji Joseph Warioba wakati mdahalo wa kutoa
elimu kuhusu katiba iliyopendekezwa na Bunge maalum la katiba,sasa Mapya yaibuka kuhusu Fujo hizo,Mtandao huu unariboti
Taarifa za kuaminika ambazo Mwandishi wa Mtandao huu amezipata zinasema Chama cha Mapinduzi CCM kilikuwa nyuma za vurugu hizo zilizoibuka wakati wa mdahalo huo wa kutoa elimu kuhusu katiba,na kiongozi wa vurugu hizo ametajwa kuwa ni Paul makonda katibu wa uhamisishaji wa umoja wa Vijana (UV-CCM),
Wednesday, November 5, 2014
HABARI KUBWA--MATOKEO YA DARASA LA SABA YAPO HAPA,WENGI WAFAULU

DK. CHARLES E. MSONDE
AKITANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA MAPEMA HII LEO OFISINI
KWAKE,MSONDA AMESEMA MATOKEO YA MWAKA HUU UFAURU WAKE NI MKUBWA
UKILINGANISHA NA YA MWAKA JANA
Matokeo ya Darasa la 7 kwa mwaka 2014 yametangazwa na Baraza la Mitihani Tanzania Necta ambapo katika matokeo hayo ya mwaka huu yanaonyesha Kiwango cha ufaulu kupanda kwa asilimia 56.99 Tofauti na ufaulu wa mwaka jana ambao ulikuwa Asilimia 51.6 Huku mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza.
HAYA HAPA NDO MATOKEO YENYEWE:
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS
KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHOIVAA SWAZILAND HIKI HAPA
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza
kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la
Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16
mwaka huu jijini Mbabane.
Akizungumza Dar es Salaam, leo (Novemba
5 mwaka huu), Nooij alisema kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 10 mwaka huu
saa 6 mchana kwenye hoteli ya Accomondia, na siku hiyo hiyo jioni kitafanya
mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA MITAJI HISA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO.
![]() |
| Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo waliohudhuri ufunguzi huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia. Picha na OMR |
![]() |
| - Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. |
KUTOKA CHADEMA LEO
Tuesday, November 4, 2014
VURUGU MDAHALO WA WARIOBA--WANAHARAKATI WACHARUKA,SOMA KILICHOZUNGUMZWA MUDA HUU JIJINI DAR ES SALAAM
Ikiwa ni siku kadhaa kupita tangu tukio la kufanyiwa fujo
kwa mdahalo ulikuwa unafanyka jijini Dar es salaam chini ya mwenyekii wa tume
ya mabadiko ya katiba Tanzania
jaji JOSEPH SINDE WARIOBA, asasi mbalimbali za kiraia wameibuka na kauli nzito ya kulaani
kitendo hicho ambacho wamedai kuwa kinafedhehesha taifa.
Wakizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam
wanaharakati hao wakIongozwa na mkurugnzi wa kituo cha sheria na haki za
binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA wamesema kuwa kitendo cha kuvuruga mdahalo huo
ni kitendo cha kulaaniwa na kila mtanzania mpenda haki na si kitendo kizuri
katika mchakato wa kupata katiba ya Tanzania.
| Wanahabari wakiwa wanafwatilia kwa umakini |
“ndugu
wanahabari kitendo cha kufanya vurugu katika mdahalo wa juzi kinapaswa kulaaniwa
na kukemewa na kila mwananchi mwenye mapenzi mema na taifa la Tanzania na
hasa viongozi wananchi wenye dhamana yakulinda na kutetea democrasia na amani
tuliyo nayo.amesema bi HELLEN.
Aidha amesema
kuwa vurugu hizo zimeonyesha kuwa zina lengo la kuwatisha wanachi wasijadili
katiba waitakayo kwa muskatabali wan chi yao ,ambapo
amesema kuwa ni lazima kitendo hiki kikemewe na kila mtanzania ili kuweza
kuweka dmocrasia ya kweli katia kutoa maoni ya katiba ya Tanzania .
Katika hatua
nyingine wanaharakati hao wamvitaka vyombo vya
sheria kuhakikisha kuwa wanawatia mbaroni vijana wote walioonekana
kuanzisha vurugu hizo juzi katika mdahalo huo kwani kuna njia nyingi za
kuwakamata ikiwa ni pamoja na kutiza mikanda ya video ambayo imerekodiwa aidha
na uongozi wa ukumbi huo au wanahabari.
| mkurugenzi mstaafu wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA bi ANANILEA NKYA akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam |
Monday, November 3, 2014
HABARI ILIYOTIKISA JIJI--PAUL MAKONDA AIBUKA ,AJIBU TUHUMA ZA KUDAIWA KUMPIGA JAJI WARIOBA--SOMA HAPA
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita Baada ya aliyekuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Paul Makonda kumrushia Chupa aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya ukusanyaji Maoni ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakati wa mdahalo wa kutoa elimu kuhusu Katiba iliyopendekezwa na bunge Maalum la Katiba
TAMASHA LA TIGO WELCOME PACK LAFUNIKA MJINI MOSHI--PICHA ZOTE ZIKO HAPA
![]() |
Sehemu ya umati uliofurika kwenyeTamash la Tigo welcome pack
uwanja wa Ushirika Mjini Moshi.
|
![]() |
| . Msanii Emmanuel Mgaya Maarufu Masanja Mkandamizaji akiwapa raha wa kazi wa Moshi waliofurika kwenye uwanja wa Ushirika wakati wa onesho la Tigo welcome pack |
![]() |
Msanii Ibrahim Mussa maarufu Roma Mkatoliki akipiga shoo
kwenye tamasha la Tigo welcome pack uwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa
wiki.
|
![]() |
Sunday, November 2, 2014
HAYA NDIYO YALIYOJIRI UBUNGO KWENYE MDAHALO,MAKONDA AMTWANGA WARIOBA MCHANA KWEUPE

Jaji Warioba.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
VURUGU zilizoambatana na ngumi kurushwa zimetokea hivi punde katika Ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba alipokuwa akitoa mada kwenye mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuielewa kwa kina Katiba inayopendekezwa kama ilivyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba.
Vurugu hizo zimezuka baada ya watu waliokuwa na mabango kuvamia ukumbuni hapo na kusababisha baadhi ya watu waliokuwa wanafuatilia mdahalo huo kuwakabili na kuwapa kichapo.
Baada ya vurugu hizo, mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na kurushwa moja kwa moja na ITV umesimamishwa kwa muda.
![]() |
Kwa upande wake Gwiji La masuala ya habari nchini na Mhariri wa Gazeti la Tanzania Daima Edson Kamukara alichukizwa na kitendo cha Makonda haya ndio aliyoyasema kwenye ukrasa wake facebook |

SOMA ZAIDI WALICHOKISEMA WADAU JUU YA YUKIO HILO LA TUHUMA ZA MAKONDA KUMPIGA WARIOBA NA CHUPA
Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)











.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)


