Chama cha
walimu tanzania (CWT)
kimewataka wabunge kuwa makini wakati wa kujadili bajeti ya wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi , na kutambua kuwa mgogoro kati ya walimu na serikali kuhusu madai ya nyongeza za
mishahara waliyokuwa wanayadai bado haujamalizika.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini dar es salaam raisi wa chama hicho GRATIAN MUKOBA amesema ikumbukwe kuwa mgogoro
huo uliotangazwa na chama cha walimu mnamo mwaka jana haukufikia suluhu badala
yake serikali ilikimbilia mahakamani kusitisha mgomo huo na kuruhusu mazungumzo
ambayo amesema hadi sasa mazungumzo hayo bado hayajaonyesha mafanikio
Bw MUKOBA Amesema kuwa kumekuwa na
maneno mengi ambayo yamekuwa yakisemwa na serikali kuwa mgogoro huo umemalizika
jambo ambalo amesema sio kweli na kuwataka wanachama wa CWT kuendelea kuvuta subira wakati
majadiliano yanaendelea na kama hayatafikia muafaka watatoa tamko rasmi
Aidha
ameyataja baadhi ya madai ambayo walimu wamekuwa wakiyadai kutoka kwa serikali
kuwa ni ongezeko la mishahara asilimia 100,kurudishwa kwa posho ya kufundishia
asiilimia 55 kwa walimu wa sayansi na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa,pamoja na
posho ya asilimia 30 kwa walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu.
picha na maktaba
No comments:
Post a Comment