Wananchi eneo la Miyomboni wakiwa wamembana omba omba huyu tapeli kuonyesha mikono yake yote
Hapa ni kipigo kikiendelea
Tapeli huyo akitaka kujinasua kutoka mikono ya wananchi wenye hasira kali
Hapa baada ya kupata upenyo akivaa nguo zake
Hapa akiwa ameachiwa na kuanza kutimua mbio
Baada ya kuchezea kichapo tapeli huyo sasa anajaribu kuficha aibu
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO KWENYE TUKIO LA KWANZA
Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo
AMA Kweli mwisho wa utapeli ni aibu kubwa na wahenga walinena kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wamepata kushuhudia kituko cha mwaka baada ya watu waliochoka kuvumilia vitendo vya kitapeli vinavyofanywa mzee mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli huyo mbali ya kuumbuliwa kwa kutakiwa kuonyesha miguu yake yote pamoja na mikono yake yote bado amepata kuchezea kichapo kiasi cha kunusurika kuuwawa na wananchi hao wenye hasira kali.
Tukio la mzee huyo kubainika kama ni tapeli kwa mara ya kwanza mtandao wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ndio ulipata kufichua siri hiyo ya omba omba huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano wa mlemavu .
Kutokana na kufichuliwa kwa siri hiyo ya kujiigiza kuwa ni omba omba mlemavu wananchi wamekuwa wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na kumtimua mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua kumkimbiza kutoka eneo la Hazina Ndogo hadi miyomboni na kuanza kumpa kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo vyote kuwa si mlemavu
Tapeli huyo mbali ya kujifanya ni mlemavu wa viungo wakati mwingine huwa anajifanya ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu mmoja na kuwaomba watu fedha za matibabu .
Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu).
Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo kutokana na kichapo alichokipata na kuumizwa vibaya usoni .
Hata hivyo inasemekana mzee huyo amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali mbali kutokana na mbinu yake ya kufuru anayoifanya kuwa ni mlemavu wakati si mlemavu na kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya kiuchumi kuliko kuwaigiza walemavu na kuwa iwapo atarudia na kukutwa akifanya hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya hivyo.
Aidha anadaiwa chanzo cha kichapo cha leo kwa mzee huyo tapeli ni mmoja kati ya mpenzi wake ambae alikuwa amemsusa na kuhamia kwa mpenzi mwingine kuueleza umma kuwa huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea wananchi kufanya udadisi.
Kabla kufukuzwa na kuchezea kichapo tapeli huyo alifukuzwa eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya vijana wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.
CHANZO: FRANCIS GODWIN WA MATUKIO DAIMA
CHANZO: FRANCIS GODWIN WA MATUKIO DAIMA
No comments:
Post a Comment