Inadaiwa kuwa Waasi wa M23 jana wamemkamata askari wa Tanzania anayefahamika kwa jina Christopher George Yohana katika maeneo ya Kinyandonyi huko kivu ya kaskazini, Waasi hao wa M23 wameweka picha ya passport ya mateka huyo kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Habari zilizoandikwa na mtandao wa chimpreports.com, zimeeleza kuwa Waasi waM23 wameripoti kumkamata askari huyo akiwa na bunduki aina ya AK47 yenye serial number 1372. Hapa chini ni kauli waliyoandika Waasi wa M23 kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook ......“leo Fdlr zikiongozwa na askari toka Tanzania zilivamiya Positions zetu pale Kinyadonyi Na Nkwenda huko Rutshuru. Zilikuta Vijana wanazisubiri, walizicapa na kuzikimbiza alafu zikaaca Askari wa Tanzania Nyuma tukamunasa, ivi tuko naye tuko na mupa cayi na mukate anywe.
Serikali ya tanzania isiwe na hofu hatutamufanya kitu, tutamucunga muzuri. sisi hatuko kama wale wa criminals wa FARDC ambao wanatukanaka hata maiti, na wenye Wanabakaka watoto wa myaka sita, sisi ni jeshi la Mungu. Kesho mutaona Video yake, Cliquer apa uone passport ya ule askari ya tanzania ambaye tulikamata”
HABARI KWA NIABA YA CHINGA ONE BLOG
No comments:
Post a Comment