Wednesday, August 28, 2013

POLISI DAR YACHARUKA,MAJAMBAZI 9 WAKAMATWA YUMO ASKARI POLISI,WENGINE WANATUMIA SARE ZA JESHI

PICHA NA MAKTABA
Jeshi la polisi kanda maalumu limefankiwa kukamata majambazi wanne akiwemo askari wa polisi wa kituo cha polisi kimara katika mkoa wa kipolisi kinondoni ambaye jina lake ni NO F 1205 PC MUHIDINI MHINA          Akizungumza na wanahabari leo jjini dar es salaam kamishna wa kanda hiyo SULEMAN KOVA amesema kuwa mnamo tarehe 26 ya mwezi huu wa nane majira ya saa tatu usiku huko maeneo ya club ya wazee amana ilala nyumbani kwa MOHAMED SAISI MOHAMED  ambaye ni msukuma mfanya biashara alisikia watu wakigonga hodi alipofungua akijua ni wageni ghafla mmoja akatoa bastola na kuanza kuwatisha kuwa watoe hela zote zilizopo nyumbani ambapo walifanikiwa kupora kiasi cha dolla 20,000 na kutoka nazo,

           Amesema kuwa wakati wakitoka alitokea mwananchi wa kawaida aliyekutana nao mlanhgoni ndipo alifanikiwa kumzuia mmoja na nipo wnanchi walipofika na kutaka kumpiga,ghafla alijitokea askari mohidin ambaye alikuwa likio na kudai wamwachie aondoke naye kani yeye ni askari lakini wananchi wale walipinga kitendo kile na ndipo walipowaita askari wa ukweli na kuwakamata wote wawili.
wengine waliokamatwa ni FARUK OMARI,OMGBA KHERI,PAMOJA NA GHALIBU IBRAHIMU

              Aidha katika tukio lingine jeshi la polisi limeakamata majambazi watano huko temeke ambao wlikuwa wanatumia sare za jeshi la wananchi tanzania pamja na za jeshi la polisi na vifaa kama pingi,na silaha katika kufanya uhalifu wao

          Aidha kova ameomba kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kuwafichua wahalifu kama hao katika mitaa huko akitamba kuwa sasa wameanza kazi ya kuwafuta majambazi ama hao jijini dar es salaam


No comments: