Club ya yanga leo imetengaza kumwajiri rasmi mkenye PATRICK NAGGI ambaye hapo awali alizua taharuki baada ya wazee wa club hiyo kumpinga, na watu wengine wawili huku ikisema kuwa LAURENCE MWALUSAKO ataendelea kukaimu nafasi ya katibu mkuu katibu huyo mpya
Akizungumza na wanahabari leo jijini dar es salaam makam mwenyekiti ndg CLEMENT SANGA amesema kuwa maambuzi hayo yalifikiwa na kikao cha kamati ya utendaji jana jijini dar es salaam.
Wengine walioajiriwa ni BENO NJOVU ambaye ni mshauri wa maswala ya utawala na fedha pamoja na GEORGE SIMBA MAGANI atakeyefanya shughuli za masoko
Sanga amesema kuwa waajiriwa wote hao nafasi zao zitatangazwa rasmi baada ya miezi miwili huku akisisitiza kuwa mwalusako anaendelea kukaimu nafasi ya katibu
No comments:
Post a Comment