Shindano la kuimba la Epiq BSS limeingia hatua za mwisho
wiki hii likiwa limebakiza washiriki kumi na mbili, kuelekea kumpata mshindi wa
shilingi milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Washiriki waliochaguliwa kwa usaili wa simu, nao waliungana na wenzao waliongia kumi bora wiki hii na konyesha uwezo mkubwa, hali inayoashiria kutakuwa na kazi kubwa kumchagua mshindi.
Washiriki waliobaki mpaka sasa na namba zao za ushiriki ni Amina Chibaba (03), Elizabeth Mwakijambile (08), Emmanuel Msuya (21), First Godfrey (11), Francis Flavian (09), Furaha Charles (14), Furaha Mkwama (06), Joshua Kahoza (02), Maina Thadei (5), Mandela Nicholas (10), Melisa John (22) na Raymond John (23).
Akizungumzia hatua ambayo shindano limefikia, jaji mkuu wa shidano hilo, Ritha Paulsen, aliwataka wananchi watumie vema nafasi ya kupiga kura kwa kuchagua washiriki wenye vipaji vikubwa.
‘Hatua hii ni muhimu sana, hasa kwa kuwa inalirudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao, hivyo nawaomba wawapigie kura kwa wingi’ alisema Ritha.
Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amewataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri na watafanya vizuri kwenye soko.
‘Maana ya kufungua laini za watu kupiga kura mapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wanayempenda’ alisema Khan.
Kampuni ya Zantel pia imerahisisha namna ya upigaji kura kwa kutoa namba maalumu ya kupiga kura kwa kupiga simu namba 0901551000, na kwa njia ya ujumbe mfupi mashabiki wa Epiq BSS wataweza kuwapigia washiriki wanaowapenda kwa kuandika neno KURA, halafu waache nafasi, namba ya mshiriki halafu watume kwenda 15530.

Akizungumzia
ubora wa washiriki wa mwaka huu, Ritha alisema wamepata washiriki bora zaidi,
na pia mafunzo wanayoyapata ndani ya jumba la Epiq BSS ni makubwa hivyo
mashabiki watarajie mchuano mkubwa zaidi katika kuwania milioni hamsini.
Kwa upande wake Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amewataka wananchi wawapigie kura washiriki wanaoamini ni wazuri na watafanya vizuri kwenye soko.
‘Maana ya kufungua laini za watu kupiga kura mapema ni kuwapa nafasi ya kuchagua mshindi wanayempenda’ alisema Khan.
Kampuni ya Zantel pia imerahisisha namna ya upigaji kura kwa kutoa namba maalumu ya kupiga kura kwa kupiga simu namba 0901551000, na kwa njia ya ujumbe mfupi mashabiki wa Epiq BSS wataweza kuwapigia washiriki wanaowapenda kwa kuandika neno KURA, halafu waache nafasi, namba ya mshiriki halafu watume kwenda 15530.
Mshiriki Elizabeth Mwaakijambile
akitoa burudani kwa waandishi wa habari leo. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa
Huduma za Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha
Paulsen.
|
Mshiriki First Godfrey akiimba mbele
ya waandishi wa habari. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za Ziada wa
Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen, mwisho ni Haji
Yussuf, Meneja Huduma za Ziada.
|
Jaji Mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen,
akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maenedeleo ya kipindi hicho.
Kulia kwake ni Haji Yussuf, Meneja Huduma za ziada, na kushoto ni Mtaalamu wa
huduma za ziada, Cecil Muhina.
|
Mshiriki Joshua Kahoza akiimba wakati
wa mkutano na waandishi wa habari. Anayetazama kushoto ni Mtaalamu wa Huduma za
Ziada wa Zantel, Cecil Muhina, na jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen.
|
No comments:
Post a Comment