JOHN MNYIKA AKITOA UFAFANUZI KWA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM |
Na Karoli Vinsent
SIKU
chache baada ya aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kikushutumu
chadema kwa uamuzi wa kumvua uongozi aliokuwa nao ndani ya chama hicho.Chama
cha Demokrasia na Maendeleo “chadema” kimeibuka na kumpa ukweli wake.
Ukweli wa chama
hicho ulitolewa na Mwanasheria wa Chama hicho,ambaye ni Mbunge wa Singida
Mashariki TUNDU LISU pamoja Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Chama hicho ambaye pia ni mbunge wa jimbo la ubungu JOHN
MNYIKA,leo makao makuu ya chama hicho jijini dar es salaam wakati
wakizungumza na wahariri pamoja na wandishi wa habari
Kuhusu sababu ya kumvua uongozi
ndani ya chadema ENDELEA HAPO CHINI---------
Kuhusu hoja ya kumfukuza chadema
mwanasheria wa chama hicho Tundu lissu alisema uamuzi waliofanya ulikuwa sahihi
na wamefuata kanuni zote za chama kwa mwanachama au kiongozi yeyote anayeenda
kinyume na taratibu za chama
“Sheria zipo wazi na sheria hizi sijatunga mimi wala
zitto,sheria hizi ni Chama,kwa kiongozi yeyote au mwanachama akifanya mambo
kinyume, kamati kuu ya chadema inanguvu ya kumvua uongozi na ikwezekana hata
kumfuta uanachama na kamati kuu ya chadema haijavunja katiba”alisema Lissu
Vilevile mwanasheria huyo akafafanua kuhusu hatua ambazo
chama kinachofanya kwa mda huu baada ya kumati kuu ya chadema kuvua uongozi wa
chadema zitto kabwe pamoja na mjumbe wa kamati kuu wa chama hicho Dk kitilo
Mkumbo
“Kwa sasa chama tayari kimekamilisha utaribu wa kuwapa
barua kwa maandishi kama katiba ya chama inavyosema na vilevile chama kimewapa
fursa ya siku kumi ili waje kujitetea kwenye tena kwa maandishi juu ya tuhuma
zinazowakabili kwenye kamati kuu ya chama na chama kitasikiliza na kutoa
maamuzi”alizidi kufafanua LISU
Aidha Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chama hicho ambaye
pia ni mbunge wa jimbo la ubungu JOHN MNYIKA alisema kama watuhumiwa hawo
watadharau maamuzi ya chama kuhusu kuja kujitetea baada ya siku kumi na nne
basi chama hicho kitafanya maamuzi magumu
“kama siku kumi na nne zikipita watuhumiwa hao
hawatafanya busara kuja kujitetea kwenye kamati kuu ya chadema kwa maandishi
kama katiba ya chama inavyosema, basi chadema itafanya maamuzi magumu kwa sasa
sitaweza kuzungumzia hatua tutakazochukua”alisema John Mnyika
Suala la waraka wa siri
Kuhusu
walaka wa siri ambao chadema waliunasa kutoka kwenye kompyuta ya Watuhumiwa hao,
ukionyesha mikakati ya kukihujuma chama hicho pamoja viongozi wa chama hicho
Mwanasheria wa chadema alifafanua na kukanusha ule walaka uliosambazwa kwenye
vyombo vya habari amabapo Zitto kabwe aliusambaza wakati akizungumza na
waandishi wa habari juzi jumapili kwenye hoteri ya serena jijini Dar es salaama
na kusema walaka huo ni tofauti na tulio tumia kumuhukumu kwenye kamati kuu ya
chadema,
“Kuhusu walaka unaosambazwa na yeye Zitto Kabwe
kwenye vyombo vya habari ni tofauti na ule tuliotumia kumuhukumu kwenye kamati
kuu ya chama, na mwenyewe Zitto anafanya uwongo wa hali ya juu ili kupotosha
uma umwamini juu ya kile anachokisema”alisema Lissu
Vilevile,Tundu Lissu alisema ukisoma walaka ambao unasambazwa
kwenye vyombo vya habari unaonyesha upungufu wa kiongozi huyo na kusema sababu
za uwongo za sisi kumuengua chadema
“Zitto kabwe amewadanganya watanzania kwa kupia
walaka ule nataka niwambie watanzania walaka ule anausambaza nakuonyesha kamati
kuu kuwa tumemuengua chadema kutokana na Hesabu za Vyama vya kisiasa”,
“kutokana nayeye kuwania nafasi ya mwenyekiti pamoja na
ufisadi anausema yeye.Nataka niwambie wanachadema pamoja na watanzania walaka
ambao kamati kuu tumetumia kumuhuku hajazungumzia hivyo vitu na wala havipo
kwenye walaka amabao tumemuhuku na sisi tutahuto walaka huo mala baada ya siku
kumi na nne kupita”alifafanua Lissu
Kuhusu hoja ya ukuguzi wa fedha ndani ya chadema
Kwa upande waukaguzi wa matumizi ya fedha ndani ya chadema,Mwanasheria
wa chama hicho alisema anayosema mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto kabwe ni
dariri ya uongo anaofanya hivyo kwa makusudi na akatoa ushahidi kwa waandishi
wa habari juu ya ukaguzi wa fedha ndani chama
“ Mwaka 2010 mkaguzi aliniaviandika vyama vyote
kisiasa vilipie garama ya ukaguzi wa atakaofanya kwenye vyama vya siasa”
Barua hiyo ilisomeka kama ifuatavyo “mimi sijapewa
ruksa ya kukagua ila sijapewa pesa ya kukagu vyama vya kisias”barua hiyo
ilitoka na kwa mkaguzi mkuu wa serikali kwenda kwa vyama vya siasa
Aidha,Mwanashera huyo wa chadema aliongeza na kusema
mwaka jana mwezi semptemba vilipereka hesabu kwa mkaguzi mkuu wa serikali
pamoja na msajili wa vyama vya kisiasa
“Mwaka jana mwezi semptemba vyama vitatu vilipereka hesabu
kwa msajili wa vyama vya siasa ilonyesha Chama cha wananchi Cuf walipereka
hesabu zao”
“Na chama cha Nccr mageuzi pia walipeleka pamoja na sisi
Chadema,katika ukaguzi ulionyesha vyama viwili tu ndivyo vilivyofanyiwa ukaguzi
ambapo na sisi chadema na Nccr nashamshangaa zito kabwe anasema chadema
haijakaguliwa sijui ananini huyu mtu”alijoji Lissu
Katika hatua nyingine Mwanasheria huyo wa Chadema
alimshutumu aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kuwa Hajawai
kufika kwenye ofisi za chadema tangu achaguliwe kuwa mbunge mwaka 2010 hajawai
kufika kwenye ofisi za chama hicho
MWANASHERIA MKUU WA CHAMA HICHO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI JJINI DAR ES SALAAM LEO |
No comments:
Post a Comment