Na Karoli Vinsent
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa
Monduli, Edward Lowassa (CCM), amewaomba wanachama wa chama hicho kuhakikisha
wanaweka ushawishi katika suala la elimu bure na bora ili iwe ajenda ya kwanza
katika ilani ijayo ya uchaguzi wa chama hicho.
Akiwahutubia
wananchi wa Kata ya Kigamboni alipokwenda kukabidhi madawati shule za msingi za
kata hiyo, Lowassa alisema kutokana na kuhitaji kuona Watanzania wanapata elimu
bora ni muhimu ajenda hiyo ikapendekezwa na kila mwanachama wa CCM.
ENDELEA KUSOMAHAPO CHINI-------
Lowassa
alisema kuwa anaamini kuna siku elimu nchini itatolewa bure kwa kila Mtanzania
kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kujenga usawa wa matabaka kwa taifa.
“Wana
CCM wenzangu naomba tushawishi suala la elimu bure kwa wanafunzi wote wa shule,
tena elimu bora liwe la kwanza katika ilani ijayo ya uchaguzi,” alisema.
Lowassa
alisema kuwa hali ya uchumi kwa sasa imeimarika kutokana na uongozi thabiti wa
Rais Jakaya Kikwete ambao umeimarisha miumbombinu.
“Wakati
Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa anaingia madarakani, alikuta madeni mengi,
serikali yake ikafanya juhudi kulipa na kuanza kukopesheka, Rais Kikwete yeye
ameunyanyua uchumi kwa kuimarisha miundombinu na sasa hali ni nzuri kabisa,
sasa tuelekeze nguvu katika elimu,” alisema.
Alisema
kuwa kwa wale wanaokubaliana na fikra zake za kutaka elimu bure na bora
wanapaswa kujenga hoja katika mitandao na sio kupinga tu.
“Najua
wako watakaobisha na kusema sana katika mitandao, lakini mimi nawaomba wabishe
kwa hoja na iwe ni mjadala katika mitandao na sio kupinga tu, hiyo haisaidii,”
alisema.
Lowassa
alisema kuwa hafurahii kuona wanafunzi wanakaa chini wakati uwezo wa kuboresha
hali hiyo pamoja na maslahi ya walimu inawezekana.
Aidha,
Lowassa alichangia madawati 100 na kutoa changamoto kwa wadau wengine wa elimu
kusaidia zaidi huku akiahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa kikundi cha
Vicoba cha kinamama wa Kigamboni.
Huu, si mwanzo kwa Lowassa kuendeleo kuipinga elimu
inayotolewa hapa nchini,amekuwa akifanya hivyo tu pindi anapopewa nafasi ya
kuchangia kuhusu elimu,
Wachambuzi, ya masula ya elimu nchini wanaitazama kauli ya
Lowasa kuhusu elimu inatija,kutokana na elimu inayotolewa nchini kutomwandaa
mwanafunzi kujiajiri mwenyewe,huku wachambuzi hao wakionyesha kuna kila aina ya
dariri vijana wakawa bomu mbeleni kutokana na vyuo vikuu vingi kuzalisha wasomi
wengi huku wasomi hao wakingojea kuajiriwa na serikali kuliko kujiajiri
mwenyewe,huku uchumi wa Tanzania
kutakaa kutoa ajira,
Mbali na suala la elimu,wachambuzi hawo wakailahumu
serikali ya Ccm kwa kuviua viwanda vya ndani, ambavyo vilikuwa vinatoa ajira
kwa vijana wengi ambao wanamaliza shure na kutoka vyuo vikuu mbalimbali,
“Mji wa mrogoro ulikuwa na viwanda vingi sana miaka ya
nyuma na viwanda hivi vilikuwa vinachukuwa watu wote kutoka kwenye mikoa
mbalimbali kwa mfano hapa Dar miaka ya nyuma ulikuwa umkuti mtu katikati ya
wiki yuko nyumbani au vijiweni maana watu wote wanakuwa wanafanya kazi
viwandani,lakini leo viwanda vile vyote vimekufa na walioviuwa wanajulikana na
wapo kwann hawachukuliwi hatua?”walihoji wachambuzi hawo
No comments:
Post a Comment