Na Karoli Vinsent
SIKU chache baada ya Waziri wa zamani
na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka na
kutishia kumuua binti mdogo wa miaka 16, kiongozi huyo ameibuka na kutoa
utetezi wa kujikanganya.
endelea hapa chini-------
Akizungumza kupitia kwa wakili wake,
Yasin Memba, mbunge huyo alitishia kuliburuza gazeti hilo mahakamani endapo halitamwomba msamaha
ndani ya siku saba.
Pamoja na kukataa kwake kumfahamu binti
huyo, Kapuya amekiri kumiliki simu namba0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana
naye ikiwemo kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.
Hata hivyo, katika namna ya kushangaza,
Kapuya alidai kwamba simu hiyo aliishaigawa miezi sita iliyopita, na hivyo
hausiki kwa namna moja ama nyingine na tuhuma alizopewa.
Lakini wakati Kapuya akikwepa mtego huo,
Novemba 9, mwaka huu, gazeti hilo
liliwasiliana naye kupitia namba hiyo hiyo anayodai kwamba alishaigawa miezi
sita iliyopita.
Tarehe hiyo, gazeti hili liliwasiliana na
mbunge huyo ili kuthibitisha tuhuma zilizokuwa zikimkabili wilayani Kaliua za
kumpiga makofi kiongozi mmoja wa CCM.
Kapuya kupitia namba hiyo, alitoa utetezi
wake ambapo gazeti hili lina sauti yake.
Utetezi wake pia unaongeza utata kwani
hakufafanua ilikuwaje akagawa namba ya simu iliyosajiliwa kwa jina lake kwa mtu
mwingine, huku ikiendelea kutuma fedha na vitisho kwa binti huyo.
Katika
utetezi wake jana, Kapuya alikana kutomjua binti huyo wala dada yake, na kwamba
yeye si mwathirika wa ugonjwa wa ukimwi.
Alilishutumu
gazeti hili kuwa lilijifanya hakimu kwa kuchapisha tuhuma zake bila kumpa
nafasi ya kujitetea kama ilivyo kawaida kwenye
tasnia ya habari.
Hata
hiyo, ukweli ni kwamba nafasi hiyo aliipata, lakini hakuitumia kwani
alipopigiwa, simu yake ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake
na kutaka aelezwe sababu za kutafutwa bosi wake.
Hata
alipoelezwa kuwa anayehitajika ni bosi wake, alisita kisha alitoa namba
nyingine ya simu akitaka atafutwe kupitia namba hiyo.
Lakini
muda wote namba hiyo haikupokelewa na hata alipopigwa tena namba ya awali, nayo
iliita bila kupokelewa.
Wakili
Memba alidai kuwa mteja wake, alimweleza kuwa habari ile imemletea madhara na
usumbufu mkubwa katika familia yake, jamii na kumvunjia heshima yake.
“Kwa
sababu hiyo, amenielekeza niwapatie siku saba gazeti la Tanzania Daima,
mitandao ya kijamii ukiwemo wa Jamii Forum, Justina John na Vituko Mtaani ambao
walichapisha habari hiyo, waombe radhi kwa uzito ule ule la sivyo
atavishitaki mahakamani.
“Kama
hawataomba radhi, basi atafungua kesi mbili, moja ni kwa ajili ya gazeti la
Tanzania Daima na hiyo mitandao ya kijamii, na kesi ya pili ni ya kuhusu huyo
mtoto anayedaiwa kubakwa na kuambukizwa ukimwi,” alisema.
Aliongeza
kuwa wanataka mtoto huyo aje mahakamani athibitishe aliambukizwaje ukimwi na
alete ushahidi unaoonyesha Kapuya ana ukimwi.
Memba
aliuomba umma kuelewa kuwa habari hiyo iliyochapishwa na Tanzania Daima
haiusiani na chama chake wala serikali.
Kwa siku
mbili mfululizo gazeti hilo lilifichua tuhuma za Kapuya kudaiwa kumbaka mtoto
huyo, na hata baada ya kubaini siri hiyo imevuja, alimpigia simu mtoto huyo, na
baadaye kutuma meseji kadhaa za vitisho.
Juzi
alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake alituma ujumbe kwa mtoto huyo: “Chagueni
kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?”
Baadaye
saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa
mtoto huyo, ukisema: “Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi.
Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama
wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.”
Baadhi
ya mashirika yanayotetea makundi kadhaa yakiwamo Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC) na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) yalijitokeza kuwasaidia
watoto hao, ambao ni yatima.
Mtoto
huyo na dada yake, wakizungumza na gazeti hili kwa hofu mafichoni, walisema kwa
sasa hawana imani tena kama kuna serikali nchini Tanzania kwa kuwa
wamedhalilishwa, wametembezwa hadi bungeni na wabunge bila hatua kuchukuliwa,
licha ya kutoa taarifa katika Kituo Cha polisi Oysterbay tangu mwaka jana.
Hata
hivyo, kabla ya tukio la watoto hao kuripotiwa ofisi za gazeti hili, juzi usiku
kulikuwa na watu waliokuja wakiwatafuta watoto hao, huku wakiwatisha kwa simu
na kuwatolea maneno ya kejeli, wakidai watawamwagia tindikali.
Juzi
gazeti hilo lilichapisha habari kuhusu mwanafunzi huyo aliyesema kuwa
waziri huyo alimbaka kwenye hoteli moja ya kitalii iliyoko jijini Dar es
Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo hicho katika Jengo la Biashara
Complex lililoko Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa
mara ya pili.
Wachambuzi wa masuala ya mambo wanaona kauli ya Mbunge
huyo ni yakutapatapa na kuvinyima fulsa vyombo vya habari kuandika ukweli na
maovu wanayofanya tabaka tawala, kwakuwa maelezo yake anayoyatoa hayaendani na
usomi wa elimu yake ya Profesa ,
Vilevile wameshangaa
kitendo cha Jeshi la Polisi nchini hususani kituo cha polisi Ostabei kushindwa
kumchukulia hatua Mwanasiasa huyo kwa kitendo hicho cha kinyama .
No comments:
Post a Comment