Na Karoli Vinsent
MBUNGE wa kigoma Kaskazini Zitto Kabwe
ameibuka na kujibu mapigo na kusema haondoki Chadema.
ENDELEA HAPO CHINI---------
Hayo aliyasema jana jijini Dar es salaam wakati akizungumza na
Waandishi wa Habari pamoja na Wahariri Zitto alisema kwa sasa hanampango wa
kuondoka chadema kama watu wanavyosema na kusema kuwa yeye atakuwa mtu wa
mwisho kuondoka
“Nawahakikishia siwezi kuondoka
chadema na kama kuondoka mimi nitakuwa mtu wa mwisho kukihama chadema,siwezi
nikahama Chadema akati nimejiunga tangu na miaka 16 mimi nimepanda miti ya hiki
chama mpaka leo kimestawi harafu nikihame haitowezekana”alisema Kabwe
Kuhusu kufukuzwa uongozi wa Chadema,Zitto
Kabwe alisema mpaka sasa hajapata barua kutoka kwa Viongozi wa Chama kuhusu
kufukuzwa kwake katika uongozi na kuongeze kuwa yeye anachosubilia ni barua
hiyo
“Mimi nichosubili ni barua kutoka
kwa viongozi wa Chadema wananiambie wameniengua katika Uongozi na Sababu
waziweke hadharani,na mimi nitachukua hatua ya kukata rufaa sehemu
zengine”alisema zitto
Vilevile Kabwe alimtaka Mwanasheria
Mkuu wa Chadema Tundu Lissu ambae pia ni Mbunge wa singida Mashariki, atoe
ushahidi kama Zitto kabwe anahusika katika Ripoti hiyo ya siri,
Zitto aliongeza na kusema Lissu amevunja
kanuni za Chama katika kutoa hukumu hiyo
“Ukisoma vipengere mbalimbali vya
katiba ya Chadema inasema wazi kuhusu kumuengua kiongozi pamoja na kumfukuza
mwanachama,ni pamoja na kumpa mda wa kujitetea pamoja na kuonyesha ushahidi wa
kosa lenyewe lakini leo Chadema hawajafanya hivyo wametoa mahamuzi ambayo yako
nje ya Katiba ya chadema”alisema Kabwe
Kwa upande mwingine Zitto Kabwe
amefadhaishwa sana hari ya kisiasa ndani ya chama cha Chadema na kusema kuwa
hali hiyo haitasaida kujenga chama bali ndio itakuwa inakishusha chama hicho
“Siasa za Majungu ndani ya Chadema
haita kisaidia Chama na hari hii Chadema inapitia katika sehemu ngumu sana
Chadema si chama Cha kwanza kupitia hali hii ni vyama vingi sana vinapitia
katika hali hii,na hali hii ni ishara tosha kabisa kuwa ni kukomaa kwa
Demokrasia na kikipa nguvu chama’”alisema kabwe
KUHUSU DK KITILA MKUMBO KUENGULIWA
NAFASI YA UONGOZI
Kwa upande wake kitila mkumbo yeye
alisema amefadhaishwa na maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu na kusema
hawajafuata haki
“mimi sijakubalina na maamuzi ya
wajumbe kwani hawajafuhata haki katika maamuzi haya kwani katiba ya chama hiko
wazi katika kuwaengua viongozi lakini leo chadema hawajafata vipengere kama
kumpa mwanachama au kiongozi kujitetea pamoja na ushahidi wa kile anachokifanya
na huo walaka ambao tunahukumiwa uko sahihi”alisema Mkumbo
Vilevile kuhusu hoja ya kukihama Chama
Mkumbo alisema kwa sasa hatokiahama chama cha chadema na hataendeleo
kupigania hati ya watanzania na hatua chama hicho kinapitia ni hatua ya
kukijenga chama na chama chochote duniani cha kisiasa kinapita sehemu
hiyo
KUHUSU WALAKA WA SIRI KUHUSU MABADILIKO
YA CHADEMA
Kuhusu hoja ya
walaka mbunge Zitto Kabwe pamoja na Mhadhiri mwandamizi kutoka chuo kikuu
cha mrimani Dokta Kitila Mkumbo wote kwa pamoja waliunga mkono yale
yalioandikwa ndani walaka huo na kuongeza kuwa kama mtu anayependa mabadariko
lazima haukubali walaka huo
“Mimi sikuwaikusoma walaka huo
niliuona mala ya kwanza kwenye mkutano mkuu wa chama juzi na nilipousoma
nikaukubari walaka huo na kuvikubali vipengere vyote vilivyoandikwa katika
walaka huo”Alisema Zitto Kabwe
Kwa upnde wa Dk Mkumbo alisema
walaka huo umeandikwa mahasusi kwa ajiri ya kukijenga chama cha Chadema
“Walaka huu unaonyesha taswira
ya kukijenga chama chetu kukitoa katika mfumo wa kidikteta na kukifanya kiwe
chama cha nchi nzima”alesema Mkumbo
Katika hali ya kushangaza Waandishi
wa habari walimbana Dk Mkumbo hawataje watu waliohusika katika kuandaa walaka
huo lakini Dk huyo aligoma kuwataja wenzake na kusema kuwa kila mtu ajitangaze
mwenyewe kwa wakati wake
Mwandishi wa Blogs hii aliushuhudi walaka
huo ikiwa pamoja na kuusoma walaka huo huku walaka huo ukionyesha udhaifu
mkubwa katika Chama hicho cha siasa chadema na katika suala la uongozi na
kuonyesha chama hicho akina uwazi wa mapato na mtumizi ya pesa pamoja na
viongozi wa juu wachadema katika kuchezea katiba ya Chama hicho ili waendelee
kubaki daima
Taarifa ya chamaAkitangaza uamuzi wa Kamati Kuu jana
Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto, Dk Mkumbo na Mwenyekiti wa
Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walikuwa na mtandao wa kukiua
chama hicho, huku wakitengeneza tuhuma za kuwachafua Mwenyekiti wa chama
hicho, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk Willbroad Slaa.
Alisema kuwa kamati kuu ilibaini
kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika
waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi
kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
“Kikundi hicho vinara wake wapo
wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na
mtu mwingine wa nne hatujamtambua kwa sasa yeye anatumia jina la M2” alisema
Lissu.
Alisema wakati wa kuhojiwa na Kamati
Kuu Dk Mkumbo alikiri kuwa mhusika mkuu wa mtandao huo ni Zitto, lakini Zitto
alikana kuutambua waraka huo licha ya kueleza unamhusu kwa kuwa umetaja jina
lake, kauli ambayo alidai Kamati Kuu haikutaka kuiamini.
Huku akieleza jinsi watu hao
walivyokuwa wakiwasiliana na kupanga mikakati ya kuimaliza Chadema kwa siri
chini ya ufadhili wa fedha kutoka kwa Zitto, Lissu alisema Naibu Katibu Mkuu
huyo wa zamani alikuwa akitumiwa na Chama Tawala (CCM) kuimaliza Chadema.
“Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni
mpango haramu na ambao unaichanachana katiba ya chama chetu. Ni mkakati wa vita
dhidi ya chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba.
Alisema Kamati Kuu itakutana kwa
dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya watuhumiwa hao
KUHUSU
RIPOTI YA SIRI KUHUSU ZITTO KABWE
KWA upande wa ripoti ilyosambazwa kwenye mitandao ya kijamiii kuhusu Zitto
Kabwe kushirikiana na Viongozi wa Juu wa Usalama wa Taifa katika kukihujuma
Chadema Ripoto hiyo iliyojulikana kama “Ripiti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Zitti Kabwe alisema yeye
alipousoma walaka huo aliwasiriana na viongozi wa chama na kuwauliza wao kama
wana utambua walaka huo na wao wakakanusha kile kilichoandikwa kwenye walaka
huo
“Mimi nilipousoma ripoti hiyo
nikawasiliana na viongozi wachama na kutaka kuja kama wao wanahusika katiaka
ripoti hiyo ila wao kwa pamoja wakakanusha kama chama kinahusika kuuandaa
walaka huo na kusema ni hila zinazofanywa na CCM pamoja na jkushirikiana na
usalama wa Taifa”alisema Zitto Kabwe
Vilevile Zitto kabwe aliongeza
na kusema kuwa kwa sasa anatawachukulia hatua viongozi wote wa chadema
waliohusika katiaka kusambaza walaka huo,ikumbukwe mwandishi wa blog hii
aliripoti kuwa walaka huo unasambazwa kwenye blogs ya kiongozi wa Chadema na
jina tumeliifadhi
KUHUSU POSHO
KUHUSU posho Kabwe alisema apokei posho toka mwaka 2008 na anafanya hivyo ili kupinga
posho zinazotolewa bungeni kwenye vikao vyake pamoja na Shuguli za Kamati na
kufafanua kuwa posho hizo zingeenda kwasaidia wa mama wajane wanaojifungulia
vichakani kwa kukosa hospitari na zingeelekezwa kwenye kujenga shure.
Kwa zaidi ya wiki mbili Zitto
amekuwa akilumbana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na
masuala ya posho.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika
kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa
posho.
Alimtuhumu mbunge huyo wa Kigoma
Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi
kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye
Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama
kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani
hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Zitto alijibu kuwa tangu siku nyingi
alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)
kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku
posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa
(Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
Zitto pia alipata msukosuko
mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’
iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama
wa Taifa kuihujumu Chadema.
Pia, Zitto aliingia katika malumbano
na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi
na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye
vyama hivyo isimamishwe.
Chadema ilipinga vikali madai hayo
na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo. Vyama
vinavyopata ruzuku ya Serikali ni vile vyenye wabunge Chadema, CCM, UDP, TLP,
CUF na NCCR-Mageuzi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment