Na Karoli Vinsent
SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo
Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), kudaiwa kutoweka nchini kukwepa mkono wa
sheria dhidi ya tuhuma za kutishia kumuua binti anayedaiwa kumbaka, vigogo wa polisi
wanadaiwa kuhusika kumsaidia kutimkia nje, Habari24 limedokezwa.
Habari24 limezipata, zinaeleza kuwa
siku mbunge huyo akikamilisha taratibu za kusafiri, ndiyo siku ambayo Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kinondoni lilikuwa limekamilisha kufungua jalada la tuhuma zake
na liliweka mtego wa kumnasa.
SOMA ZAID HAPO CHINI---------
“Wakati Polisi Kinondoni wakiweka mtego wa kumnasa, baadhi ya polisi
walimjulisha na hata kumsaidia kuhakikisha anasafiri nje ya nchi,” alisema
mmoja wa maofisa wa juu wa polisi nchini.
Hata hivyo, kuna utata na kauli
zinazopingana kuhusu mbunge huyo. Taarifa nyingine zinasema kuwa mbunge huyo
ambaye amepata kuwa waziri, anadaiwa kusafiri kwenda nchini Sweden kwa masuala
ya kikazi, na kwamba atakuwepo huko kwa muda usiopungua mwezi mmoja.
Chanzo kingine kimedokeza kuwa mbunge
huyo alidai ametumwa kazi na kigogo mmoja serikalini na atakuwepo nchini humo
miezi miwili hadi mitatu.
Hata hivyo, haijajulikana kazi anayokwenda kuifanya Kapuya ingawa kuna
taarifa safari hiyo imelenga kutuliza upepo mbaya wa kuandamwa na tuhuma za
ubakaji ambazo zipo polisi hivi sasa.
Tayari Profesa Kapuya alishafunguliwa
jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es
Salaam juzi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa linamsaka mbunge huyo ndani
na nje ya nchi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alikaririwa juzi
kuwa watamtafuta Kapuya nchi yoyote atakayokwenda iwapo tuhuma dhidi yake
zitathibitika.
Alisema mtandao wa polisi ni mkubwa,
hivyo si rahisi kwa mtuhumiwa yeyote kuukwepa mkono wa sheria endapo
itahitajika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
“Sisi tunashirikiana na polisi wa nchi mbalimbali duniani, ndiyo maana
inakuwa rahisi kwa mtuhumiwa aliyetoroka nchi fulani kukamatwa nyingine na
kurejeshwa kwao.
“Nataka niwaondoe hofu wale wote wanaodhani polisi haiwezi kumkamata mtu
akikimbia nchini, tuna mkono mrefu sana, na hatufanyi kazi kinyume na taratibu
zetu,” alisema.
Kamanda Wambura pia alikiri polisi kufungua jalada la Kapuya, huku
akiweka wazi kuwa kinachofanyika hivi sasa ni uchunguzi wa tuhuma zake.
Alisema miongoni mwa maeneo wanayoyafanyia uchunguzi ni kubaini kama
ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka
katika simu ya mbunge huyo.
“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni
nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema
Wambura.
Gazeti la Tanzania Daima limekuwa likiandika namba ya simu ya Prof.
Kapuya ambayo huwa anaitumia kutuma ujumbe wa vitisho kwa binti huyo, ingawa
kuna vyombo vingine vya habari viliamua kuandika kwa mtazamo tofauti na
kumtuhumu dada wa binti aliyebakwa kuwa ni mtu mzima na kuwa ana uhusiano na
Kapuya, na wana watoto.
Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa
kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya
kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao
kwenda kwa binti huyo.
Tangu gazeti hilo na Blogs hii vianze kuandika tuhuma hizi nzito,
kumekuwapo na kusuasua kwa mtuhumiwa huyo kutiwa hatiani na Jeshi la Polisi.
Harakati za kufungua jalada dhidi ya
Kapuya zilizoanza wiki iliyopita ziliendelea hadi juzi ambapo polisi walitumia
zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa
sakata hilo.
Akiwa polisi, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi
ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi
hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa
mashitaka.
Wachambuzi wa masuala ya kijamii
waliotoa maoni yao kuhusu sakata hili na mwandishi wa blogs hii wote kwa pamoja
wameonyesha hali ya kushangaza kwa Jeshi la polisi nchini limeshindwa
kumchukulia hatua Profesa huyu kwa vitendo vya kinyama alivyofanya huku wengine
wakiinyoshea kidore Wizara ya Jinsia na Watoto kwa kushindwa kumchulia hatua
profesa huyo.
Katika hali ya kushangaza waziri wa
Jinsia na Watoto Sophia Simba mala kwa mala amekuwa akikinyoshea kidole chama
cha Demokrasia Chadema kuwa kinavuruga amani ya nchi . huku akishindwa hatu
kumsaidia mototo huyo aliyebakwa na Kuongozi huyo wa Ccm akati ndio jukumu lake
kwenye wizara kuliko mambo haya ya vyama vya siasa ambavyo haviko kwenye wizara
yake,
No comments:
Post a Comment