Thursday, November 14, 2013

KIKONGWE CHANUSURIKA KUUAWA AKITUHUMA KUJIHUSISHA NA UCHAWI, CHATIMUA MBIO NA KUKIMBILIA KANISANI ILI KUOKOA MAISHA YAKE.


        Bibi Salima ambaye amenusurika kuuawa baada ya kuanza kupigwa na baadhi ya watu waliokuwa wakimtuhumu kujihusisha na vitendo vya ushirikina ambapo mchungaji Elias Mbagata aliamua kusalimisha maisha ya bibi huyo kwa kumhifadhi ofisini kwake.

         Baadhi ya wakazi wa Kata ya Tambukareli ambao walikusanyika Kanisa la Injili Afrika kumshuhudia Kikongwe huyo anayetuhumiwa kwa Uchawi,Bimkubwa huyo alinusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na baadhi ya watu hao na hatimaye kupelekwa kanisani kwa ajili ya usalama wake.

No comments: