TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
11/12/2013
ALERT
MSANDO
Baada ya kupokea
barua yake ya mashtaka 11 tarehe 01/12/2013 ambayo anashitakiwa nayo na
iliyomtaka ajitetee kwa maandishi,
Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe (MB) jana tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Uendeshaji za Chama
Pia Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Chama kumueleza nia
yake kukata rufaa Baraza Kuu la Chama kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu
dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.
Kuna
sababu mbili za msingi za kukata rufaa;
1. Utaratibu wa
kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.
2. Sababu za
kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.
Utaratibu ambao
unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu
wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji ni kama ifuatavyo;
Kanuni
ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
Kiongozi yeyote hatachukuliwa
hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka
husika na kupewa
nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
Pia tunapenda
ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2 (a), (b), (c) na (d) kama
ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa mujibu wa
ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama yeyote hatachukuliwa hatua za
kinidhamu ama kuonywa ama kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza;
a) Kujulishwa
makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki
mbili.
b) Kupewa nafasi
ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama
atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao mnamo wiki mbili baada ya
kusikilizwa.
d) Kamati Kuu
inaweza kuchukua hatua za dharura bila kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu
kama itaona maslahi ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa mwanachama
au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika kuitwa kwenye kikao husika.
Naomba nichukue
fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama ulifanya mkutano na waandishi mnamo
tarehe 26/11/2013 na kusema kwamba marekebisho haya ya Kanuni ya mwaka 2013 ambayo
nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu waliofuata.
Pia walieleza
kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni ilishabadilishwa.
Mabadiliko haya
ambayo ni katika kipengele (d) kuhusu hatua ya dharura iliyochukuliwa na Kamati
Kuu haikugusa kipengele (a) cha Kanuni. Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu
itachukua hatua ya dharura kwa mujibu wa kipengele (d), bado kipengele (a) ni
lazima ifuatwe na inatamka wazi sharti la kiongozi kupewa mashtaka kwa
maandishi na kupewa nafasi ya kujibu kwa maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa
kila utawala au uongozi.
Mheshimiwa Zitto
Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta ndani ya kikao baada ya kupewa taarifa
kwa ujumbe wa simu (text message au sms).
Kwa uzito wa
makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na kwa kuangalia athari zake kwake
yeye binafsi na chama kwa
ujumla, Kamati
Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.
Hili linaendana
na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba
kuvuliwa
nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa. Yeye hakuitwa kabisa kwenye kikao hicho na
ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji
Taarifa kwa
Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 4 6.5.6(d) niliyoisoma hapo juu
kwamba lazima kiongozi huyo aitwe kwenye kikao.
Sababu
zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi kwa mujibu wa Kanuni
za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki kwenye kuandaa na kusambaza waraka ambao
unasemekana ni mkakati wa ushindi wenye lengo la kupindua uongozi uliopo.
Waraka huo
haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama muandaaji au msambazaji.
Waliouandaa hawajaukana na badala
yake wamesema
waziwazi kabisa kwa maneno na maandishi kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
HAHUSIKI. Sio sawa kumuadhibu Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa
sababu ya urafiki wake na watu fulani.
Haya ni
mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za Uendeshaji zinatoa nafasi
ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya kukata rufaa. Na utaratibu ni huu hapa;
Kwa ufupi, Ibara
6.3.6(d) ya Katiba ya Chama; “Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na
mamlaka yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya ile mamlaka
yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo utakuwa wa mwisho”.
Ibara
6.3.6(e) ya Katiba ya Chama;
“Rufaa yoyote
lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupokea rasmi
kwa maandishi maamuzi ya mamlaka iliyotoa adhabu”.
Kanuni za
Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa
aweze kutumia HAKI yake ya kukata rufani kwa maneno haya;
Kanuni
ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Kiongozi
aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili
kumuwezesha kuamua kukata rufani au la”
Kanuni
ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Mwadhibiwa
atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku
thelathini baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu”
Kanuni
ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Baada ya kutoa
uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa
taarifa kamili
ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya
juu. Taarifa
hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne
baada ya kikao
cha mamuzi”
Mpaka hivi sasa
hatujapokea taarifa kamili ya mwenendo wa shauri tokea kikao cha Kamati Kuu cha
tarehe 20-21/11/2013 Huo ndio utaratibu ambao Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ameamua
kufuata kwa kuheshimu maamuzi ya Kamati Kuu lakini kukatia rufaa maamuzi hayo.
Kuheshimu maamuzi sio kuyakubali uhalali wake.
Kumekuwa na
matukio ya kusikitisha ambayo mengine yamefikia mahali kuwa fujo na vurugu
ikiwa ni pamoja na kurushiwa mawe Katibu Mkuu wa Chama. Vurugu hizo baadhi zimehusishwa
na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe na baadhi ya watu.
Mheshimiwa
Zitto Zuberi Kabwe hahusiki kwa njia yoyote na hayo
yanayoendelea na anayakemea na kuwashauri
wanachama wote kuwa watulivu na kuendelea kuwaheshimu viongozi wa kitaifa. Hatua zimeshachukuliwa kukata rufaa na ni imani yake kwamba Baraza Kuu la Chama
litatenda haki kwa kupitia rufaa
yake na kutoa uamuzi.
Nawashukuru
wote.
ALBERT MSANDO,
Mwanasheria
11/12/2013
No comments:
Post a Comment