MUDA mfupi uliopita klabu ya soka ya Yanga imetangaza
kusitisha mkataba na kocha wake Ernest Brandts baada ya kutoridhishwa na
mwenendo wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga,
Baraka Kizuguto, mkataba wa Brandts ambaye ni raia wa Uholanzi
umesitishwa rasmi leo hii asubuhi na ameshakabidhiwa barua ya kumtaarifu
juu ya hali hiyo.
“Tumesitisha mkataba na kocha wetu na
ameshakabidhiwa barua yake, huo ni uamuzi wa uongozi mzima wa Yanga,
kila kitu kimeenda sawa katika kuachana naye,” alisema Kizuguto.
Tetesi
za Brandts kutimuliwa zilizagaa jijini Dar es Salaam tangu jana muda
mfupi baada ya Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji kwamba hata kama klabu
itaamua kuachana na kocha huyo itafuata taratibu zote.
Uamuzi
huo wa Yanga unaonekana pia kuchagizwa zaidi na kipigo cha mabao 3-1
dhidi ya Simba katika mchezo maalum wa kirafiki maarufu kama Nani Mtani
Jembe uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
|
No comments:
Post a Comment