Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.
‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’
Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini..
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
PRESS RELEASE
07/01/2014
MWENYEKITI
WA CHADEMA WILAYA YA TEMEKE ATEKWA
NYARA, ASHAMBULIWA NA KUTUPWA VICHAKANI
SOMA YOTE HAPOP CHINI---------------
Jeshi
la Polisi kanda maalum Dsm, linafanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio la kutekwa
nyara, kupigwa na kujeruhiwa na hatimae kutupwa vichakani dhidi ya mtu
aitwaye JOSEPH YONA miaka 32 mkazi wa
Temeke Mtoni kwa Azizi Ally.
Imegundulika kwamba mtu huyo ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke
ambaye pia ni Mtaalam wa Maabara Chuo Kikuu cha Elimu (DUCE) kilichopo
Chang’ombe.
Mnamo
tarehe 7/1/2014 saa 5.00 usiku eneo la Ununio, mlalamikaji aitwaye Joseph Yona
alienda kuomba msaada kwa mlinzi binafsi aitwaye ISMAIL SWALEHE ili aende Kituo
cha Polisi kuripoti. Mlinzi alimuona
Joseph Yona akiwa katika hali mbaya ya kujeruhiwa. Aliamua kwanza ampeleke kwa
mwenyekiti wa serikali za mitaa Ununio.
Mwenyekiti wa Ununio alipopatikana aliwasiliana na Mkuu wa Polisi Kawe ambaye alifika eneo la tukio akifuatana
na RPC Kinondoni ACP. Camilius Wambura na kundi la wapelelezi. Maofisa wa Polisi walimhoji mlalamikaji
kuhusu majeraha aliyonayo usoni na sehemu mbali mbali za mwili wake. Mlalamikaji aliweza kujieleza vizuri kwamba
yeye ni mkazi Mtoni kwa Azizi Ally wilaya Temeke na kwamba ilipofika saa 5.oo
ya tarehe 6/1/2014 alikuwa akipata vinywaji katika grocery ya Mgumbini eneo la
Mtoni kwa Azizi Ali akiwa na wenzake watatu walikuwa wakimalizia vinywaji. Ghafla walijitokeza watu sita ambao
walijitambulisha kuwa ni Maafisa wa Polisi na walimtaka aende nao Kituo cha
Polisi cha Kati. Hata hivyo kati ya watu hao sita aliweza kumtambua mmoja wapo
kwa sura na jina (limehifadhiwa) kwamba ni mwanachama mwenzake wa Chadema na
alipojaribu kuulizia kuhusu huyo mtu
aliyemtambua, haraka walimwingiza ndani ya gari Land Cruiser na kumfunga
kitambaa usoni na kuondoka naye.
Kutokana
na maelezo ya mlalamikaji waliomteka nyara walianza kumhoji ni kwa nini
anaendelea kumshabikia Zito Kabwe wakati ni mtu anayeharibu chama chao? pili
walimtaka akawaonyeshe rafiki yake ambaye anajulikana kwa jina HABIBU
MCHANGE. Mlalamikaji JOSEPH YONA alianza
kushambuliwa baada ya kudai kwamba ni kwa nini
hapelekwi Polisi Kati (central) kama ilivyodaiwa
awali. Aliendelea kuhojiwa na kupigwa
hadi alipopoteza fahamu. Hatimaye usiku wa manane alipozinduka alijikuta yupo
vichakani sehemu asiyoifahamu na ndipo alipoanza kutangatanga na kutafuta msaada
huku akiwa katika hali ya maumivu makali katika mwili wake. Baada ya muda alifanikiwa kumpata mlinzi,
mwenyekiti wa serikali za mitaa na hatimaye kuhojiwa na Maafisa wa Jeshi la
Polisi.
Uchunguzi
wa awali unaonyesha wazi kuwa tukio hili lina uhusiano wa moja kwa moja na mgogoro
unaoendelea katika Chama cha Siasa Chadema.
Aidha kabla ya tukio hili, mlalamikaji amekuwa katika hali ya hofu
kutokana na kupokea simu nyingi na
ujumbe mfupi (sms) wa vitisho kutoka kwa viongozi wa ngazi mbali mbali wa
Chadema ambao anadai anawafahamu. Pia
jana ofisi ya Chadema Wilaya wa Temeke ilifungwa saa 10.00 jioni kwa kile
kilichodaiwa kuwa ni maagizo kutoka katika ngazi za juu katika chama cha
Chadema. Kutokana na tukio hili nimeunda
jopo la wapelelezi waliobobea wa fani
mbali mbali wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ACP. Jaffari Mohamed ili kuwabaini na kuwakamata watuhumiwa na
kuwachulia hatua kali za kisheria. Wakati huo huo natoa onyo kali kuwa vitendo vya utekaji nyara pamoja na madhara yanayofuata
baada ya hapo hayavumiliki katika jamii ya Kitanzania. Yeyote atakayegundulika
kujihusisha na matukio kama haya ajue
wazi kwamba atachukuliwa hatua kali za kisheria bila ajizi na bila kujali
nafasi yake katika jamii. Ni vizuri
kila mtu au kundi lolote lenye matatizo au mgogoro lifuate taratibu za kisheria
katika kutanzua migogoro badala ya kutumia vitisho, nguvu au utekaji nyara kama
huu.
Natoa
wito kwa mtu yeyote ambaye ni raia mwema mwenye taarifa sahihi kuhusu tukio
hili awasiliane nasi ili tusaidiane kukomesha vitendo kama hivi visirudie tena
popote nchini Tanzania.
(S. H. KOVA – CP)
KAMISHNA WA POLISI
KANDA
MAALUM
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment