TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABAR
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa
mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa
CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick.
Chama kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano
na Uhusiano, mbali ya kukemea kwa nguvu zote tukio hilo la kihuni na mengine ya
namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya binadamu, katika hatua ya sasa
kinapenda kusema yafuatayo juu ya tukio hilo ovu
ISOME YOTE HAPA=
1. Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la
kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili ukweli
ujulikane na haki itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.
2.
Chama kinawataka
wanachama na Watanzania kwa ujumla kutulia, hasa pale ambapo watu wenye hila na
malengo yao, wanaanza kukihusisha chama na tukio hilo. Watambue kuwa pamoja na
mtu yeyote kuwa kiongozi wa chama, bado anayo maisha yake na uhusiano na watu
wengine katika jamii.
3.
Jeshi la Polisi
linapaswa kuyachukulia uzito mkubwa na unaostahili matukio ya namna hii ambayo
yanaanza kuota mizizi kutokana na watu waovu wanayoyatekeleza kutochukuliwa
hatua za kisheria ambazo zingesaidia kuzuia yasitokee tena.
4.
Watanzania bado wanakumbuka kwamba hadi sasa Jeshi la Polisi
limeshindwa kutoa taarifa za kina na kuchukua hatua za kisheria ambazo
zingesaidia ukweli kujulikana na haki kutendeka katika matukio ya kutekwa na
kuteswa kwa kiongozi wa madaktari Dk. Steven Ulimboka na Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri, Absalom Kibanda. Hivyo ingesaidia kuzuia matukio mengine kutokea.
5.
Ni kutokana na jeshi hilo kushindwa kuwajibika ipasavyo
katika matukio mengine ya namna hiyo, watu waovu wanaweza kutumia mwanya wa
kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa chama kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya
wanachama wasio waadilifu, kufanya matukio ya namna hiyo ili kujenga taswira ya
kukihusisha chama na uhuni huo unaobeba kila sifa ya kuitwa ukatili dhidi ya
binadamu.
6.
Aidha kushindwa kwa
Jeshi la Polisi kuwajibika ipasavyo katika kufanya uchunguzi wa matukio hayo
(yaliyotolewa kama mfano hapo juu) na mengine ya namna hiyo, jeshi hilo
linazidi kujiweka katika wakati mgumu wa kukwepa tuhuma za baadhi ya watendaji
wake kujua na kushiriki masuala haya, hususan kwa kurejea tukio la kutekwa kwa
Dkt. Ulimboka.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano na Uhusiano
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
No comments:
Post a Comment