Na Karoli Vinsent
MIEZI michache
kupita tangu Serikali itangaze urejeshwaji wa ada ya leseni za kibiashara nchi
nzima,Chama cha Wafanya biahara wenye viwanda na Kilimo wameitaka
serikali kusitisha mpango huo.
Hayo yalisemwa
leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho Dk Piter Chasawilo
wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake,ambapo
alisema utaratibu ulio tangazwa na
Serikali juu ya urejeshwaji wa ada ya leseni na kulipia kila mwaka
utaratibu huo unaenda kinyume na sheria.
ENDELEA HAPA----------
“Utaratibu
huu mpya unaenda na kinyume na sheria ya Leseni ya mwaka 1972 na hasa
marekebisho yake ya mwaka 2004 ambayo yaliwezesha leseni za biashara
kutolewa bure na maramoja tu kwa kipindi cha maisha yote ya biashara”alisema Dk
Chasawilo
Dk
Chasawilo,alizidi kuongeza kuwa tayali kumekuwepo na malalamiko mengi kwa
jumuiya ya wafanyabiashara juu ya urejeshwaji wa ada ya leseni na sekta binafsi
inailalamika Serikali kwa kutoishirikisha katika urejeshwaji wa utaratibu
huu ambao unaiathiri sekta hii moja kwa moja na sekta binafsi inaamini kuwa
serikali imelenga kuongeza mapato bila kuzingatia nia ya urasimishaji wa sekta
isiyo lasmi ilikuarakisha maedereo ya uchumi kwa ujumla.
Aidha,Dk
Chasawilo alisemahakuna muongozo uliotolewa na serikali kuelekeza namna maombi
ya leseni yatakavyo shugulikiwa.na kusema hii inatoa mwanya kwa
maofisa husika kuongeza usumbufu kwa wafanyabiashara watakapotaka leseni hizo.na
vilevile kuongeza urasimu kufanya Biashara kwani mfanyabiashara
atalazimika kupia mlolongo wa utaratibu kila mwaka
Katika hatua nyingine chama hicho
kimezindua utaratibu mpya ambao utakuwa ni wa ujumbe mfupi yaani
(SMS MOBILE SYSTEM) ambapo lengo kubwa ni kuwashirikisha wadau ili kuweza
kuishawishi serikali kwa kutumia takwimu sahihi juu ya madhara
yanayotokana na urejeshwaji wa ada hii ya leseni
No comments:
Post a Comment