Kamishna wa polisi kanda maalum
ya dar es es salaam suleman kova amesema
kuwa ni jukumu la viongozi wote wa dare s salaam kuhakikiksha kuwa jiji hilo
linakuwa huru na salama ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa amani ya uhakika.
Kamishna kova ameyasema hayo eo katika
senmina iliyoandaliwa na manispaa ya ilala kwa viongozi wote wa ngazi za chini
kuanzia ngazi za vitongoji yenye lengo la kuboresha maswala ya usalama jijini dare
s salaam.
Kova amesema kuwa ni lazima ifike mahala
jiji la dare s salaam liwe na amani na uhuru ili ifike mahala dare s salaam iwe
mfano wa kuigwa na majiji mengine tanznia na nje ya Tanzania.
Anasema kwa kilamtaa lazima uwe huru na
mbinu pekee ya kuwa huru nikushirikiana na viongozi wa mtaa na wa ngazi za
chini.
Akizungumzia
swala la vijana wahalifu wanaojiita MBWA MWITU kamishna kova amesema kuwa
tayari ametoa agizo kwa viongozi wa mitaa hiyo kuhakikisha vijana hao
wanakamatwa mara moja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Katika semina hiyo ya viongozi
mbalimbali wa mtaa mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya ilala mh RAYMOND MUSHI
ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watanzania kushirikiana kwa pamoja
katika kuwafichua wahalifu kwani wananchi ndio walionao karibu zaidi
No comments:
Post a Comment