TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
KAMATI
KUU YA CHADEMA KUKUTANA KWA DHARURA
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itakutana kwa ajili ya kikao cha dharura, Februari 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu itajadili
na kufanya uteuzi wa mwisho wa jina la mgombea ubunge wa CHADEMA katika
uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa, unaotarajiwa kufanyika Machi
16, mwaka huu.
Kikao hicho kitafanya uteuzi wa mwisho,
baada ya mchakato wa ndani wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa
tiketi ya CHADEMA, kuwa umepitia hatua za awali, ambazo ni pamoja na watu wote
wenye nia ya kugombea, kuchukua fomu za uteuzi wa ndani tangu Februari 5-10,
mwaka huu.
Kama
ilivyoelezwa kwa umma kupitia vyombo vya habari, Februari 6, mwaka huu, fomu
hizo zilitolewa katika maeneo matatu, Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es
Salaam, Ofisi za Jimbo la Kalenga na kwenye tovuti ya chama, ambayo ni; www.chadema.or.tz.
Jumla
ya watu 16 waliweza kuchukua fomu za kuwania uteuzi huo, ambapo hadi siku ya
mwisho, watu 13 waliweza kurejesha fomu zao na kupita kwenye mchakato wa kura
za maoni, zilizofanyika Februari 12, mwaka huu.
Imetolewa
leo Februari 13, 2014, Dar es Salaam na;
Tumaini
Makene
Ofisa
Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
No comments:
Post a Comment