Na Karoli Vinsent.
IKIWA
imepita siku moja kupita Baada ya Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na Baraza la
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, kumtia hatiani Mbunge wa Bahi, Omar
Badwel (CCM), akidaiwa kutumia vibaya fedha za Mfuko wa Jimbo.
Chama
cha Mpinduzi CCM,kimesema kinasubili ripoti ya Baraza la Madiwani wa
halmashauli hiyo ili kiweze kumchukulia hatua Mbunge huyo.
Hayo,aliyasema
leo na Katibu wa Itikadi na ueneze wa Chama cha Mapinduzi CCM Nape
Nnauya,wakati wa Mahojiana kati ya mwandishi wa Mtandao huu na kiongozi
huyo,ambapo Nape alisema kwa sasa bado hajapata taharifa nzima inayomuhusu
Mbunge huyo zaidi ya kusika kwenye Vyombo vya Habari.
ENDELEA HAPA------------
“Mimi
taarifa hiyo nimeiona kwenye Vyombo vya habari ila sisi kama chama tunasubili
ripoti nzima ya Baraza la Madiwani na tujilizishe juu ya Tuhuma zinazomkabili
na ili tuweze kumchukulia hatua,sisi kama chama”alisema Nape
Mbunge
huyo ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa katika halmashauri
moja mkoani Pwani, anadaiwa kutumia fedha za mfuko huo kinyume na malengo, huku
pia taratibu za manunuzi zikiwa zimekiukwa.
Mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kujua ni hatua Gani chama
kitamchukulia mbunge huyo,Nape alisema kwa sasa hawezi kusema ni hatua gani
chama hicho kitamchukulia mpaka watakapopata taarifa nzima juu ya tuhumu
zinazomkabili mbunge huyo.
Ikumbukwe Hoja binafsi ya kuundwa kwa kamati
hiyo ilitolewa mwishoni mwa mwaka jana na Diwani wa Kata ya Lamaiti, Donald
Mejitii (CCM), akitaka matumizi ya fedha hizo za Mfuko wa Jimbo la Bahi
yachunguzwe.
Baada ya kamati hiyo kuundwa na kufanya kazi,
juzi ilirejesha taarifa yake ikibainisha kuwa fedha hizo zimetumika vibaya
tofauti na lengo la mfuko.
Mejitii katika hoja yake alidai kuwa Badwel
alitumia vibaya fedha za mfuko huo ambazo zilitolewa kwa vikundi, ununuzi na
usambazaji wa majembe ya kukokotwa na ng’ombe kwa kipindi cha Agosti mwaka
jana.
Akisoma taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Kamati,
Julius Chitojo, ambaye ni Diwani wa Kata ya Zanka, alisema kuwa walibaini
kwamba wananchi walidanganywa kwa kuuziwa majembe hayo wakielezwa ni chapa
Zimbabwe wakati ni chapa ya Jogoo.
Kamati pia ilibaini kuwa majembe hayo yaliuzwa
kwa bei ya juu kuliko ilivyokubaliwa na Kamati ya Mfuko wa Jimbo.
“Pia tumebaini kuwa makusanyo ya fedha
kutokana na mauzo ya majembe hayo hayajarudi halmashauri ili wananchi wengine
waweze kunufaika na mfuko huu wa jimbo.
“Badala yake fedha hizi zimechukuliwa na Said
Kayumbo kwa maelekezo kuwa anampelekea mbunge Badwel,” alisema Chitojo.
Hata hivyo, aliongeza kuwa baadhi ya wananchi
wamepata mgawo wa majembe ya bure wakati wengine wameuziwa, na pia fedha za
vikundi ziliingizwa katika akaunti ya Jumuiya ya Akiba na Maendeleo Bahi
(Basada) kinyume cha utaratibu.
Kwamba, hadi kufikia Oktoba 30 mwaka jana,
fedha za vikundi tisa zilikuwa bado hazijawafikia walengwa.
“Fedha za mchango wa kusafisha kisima cha maji
katika Kijiji cha Chibelela zilichukuliwa na mbunge Januari na Februari 2013 na
hazikuwa zimerejeshwa mpaka kufikia Oktoba 30 wakati baraza lilipounda kamati
ya uhakiki.
“Aidha, mbunge aliendelea kukaa na fedha hizo
huku akijua wazi kuwa halmashauri imekwishalipa fedha zote,” alisema Chitojo.
Katika mradi wa maji Chibelela, alisema zaidi
ya sh milioni 1.7 zilikusanywa kwa wananchi na alikabidhiwa mbunge.
Alisema kuwa halmashauri ilitoa fedha zote sh
milioni nne ambazo zilikuwa gharama za mradi huo na ziliingizwa katika akaunti
ya Kijiji cha
Chibelela namba 50502300434.
Chibelela namba 50502300434.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa wananchi
walidanganywa kwa kupewa risiti za ada ya kujiunga na Basada badala ya zile za
ununuzi wa majembe na kudai kuwa hiyo inaashiria kuwaibia.
“Mbunge ndiye aliyewapa kazi Basada ya
kukusanya fedha za majembe na alikuwa akiongozana nao kwenye mikutano
mbalimbali ya kukabidhi majembe.
“Wananchi waliuziwa majembe kwa nusu bei ya
sokoni yaani sh 110,000 kwa jembe wakati huo, kumbe yalinunuliwa na halmashauri
kwa sh 170,000 hivyo walipaswa kutoa sh 85,000 na sio 110,000,” alisema.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kamati hiyo
ilibaini kuwa majembe yaliyosambazwa ni 85 yenye thamani ya zaidi ya sh milioni
14.4 kati ya 78 yaliyouzwa kwa sh 110,000 ambapo ni sawa na sh milioni 8.5.
“Kutokana na uhakiki huu, kamati imebaini ya
kuwa ni kweli matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo hayapo sawa sawa. Kamati hii
inatoa maoni kuwa baraza lichukue hatua stahiki dhidi ya mbunge pamoja na kurejesha
fedha sh 2,750,000 alizozipokea msaidizi wake.
“Pia arejeshe sh 1,950,000 ambazo ni ziada ya
bei iliyokubaliwa, sh 5,440,000 za majembe 32 hayajawafikia walengwa na milioni
4.3 hazijapelekwa kwa vikundi,” alisema mwenyekiti huyo.
Kamati hiyo iliitaka Basada kurejesha fedha za
halmashauri ambazo walikusanya na kuzitumia kiasi cha sh 4,180,000 pamoja na
kuwachukulia hatua za kisheria kwa kutoa risiti ambazo sio za ununuzi wa
majembe. Vile vile fedha za Mfuko wa Jimbo zitolewe kama ruzuku na sio mkopo.
Ripoti hiyo ina viambatanisho mbalimbali
ambavyo vinadhihirisha fedha hizo kupokelewa na mbunge pamoja na msaidizi wake
Kayumbo zikiwa zimesainiwa na kuandikwa kwa mkono.
Katika utetezi wake, Badwel alisema kuwa
inawezekana kuwa kuna tatizo katika mfuko huo na kudai kuwa yaliyopo katika
ripoti hiyo mengine ni ya kweli, lakini mengine sio ya kweli.
“Katika ripoti hii sijaona sehemu ambayo mimi
nilitoa majembe ambapo katika mzunguko huu na mimi nilipeleka majembe 58 kwa
ajili ya wananchi wangu.
“Nadhani mnyonge mnyongeni, lakini haki yake
mpeni… mbona nimetoa orodha ya vijiji ambavyo nimetoa majembe yaliyotolewa kwa
Mfuko wa Jimbo na mengine ambayo sio ya mfuko?” alihoji.
Alisema kuwa lazima atendewe haki kwani yeye
hakushinikiza aina ya majembe na kudai kuwa huu ni mwaka wa tatu majembe ya
Mfuko wa Jimbo yanatolewa kwa sh laki moja.
“Sasa mimi nitasema nini, kuna vikundi vitatu
kweli hatujavipa fedha kwa sababu vilikuwa na milioni moja kila kimoja kutoka
maendeleo ya jamii.
“Hii taarifa haijanitendea haki, imejaa siasa,
imenidhalilisha ili nijiuzulu, lakini leo nasema hajiuzulu mtu na hii
haijafanywa leo, imeanza tangu nikiwa mwenyekiti wa halmashauri na
nilijiuzulu,” alisema.
No comments:
Post a Comment