Fomu za wagombea kwa ajili ya uchaguzi
wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
(TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam zimeanza kutolewa leo
(Februari 24 mwaka huu).
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu
hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi (Februari 27 mwaka huu)
saa 9 alasiri.
Ada kwa wagombea wa nafasi za
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhazini na Mhazini
Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu
zinapatikana kwa sh. 20,000.
Kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(i), sifa ya
elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi Katibu Msaidizi ni diploma au
digrii ya uandishi wa habari. Kwa nafasi nyingine kwa mujibu wa Ibara ya
21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa habari.
Tunawahimiza wanachama wa TASWA
kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi hizo.
Boniface
Wambura
MWENYEKITI
KAMATI YA UCHAGUZI TASWA
No comments:
Post a Comment