MAMBO YA TIGO |
Kampuni ya mawasiliano ya TIGO TANZANIA leo imeweka historia nyingine ya dunia baada ya kuzindua huduma yake mpya ambayo sasa unaweza kutuma na kupokea pesa ukiwa nchini Rwanda na Tanzania kwa kutumia tigo pesa kwa Tanzania na tigo cash kwa Rwanda
Huduma
hiyo ambayo imezinduliwa leo katika tafrija mbili tofauti moja ikiwa Tanzania na
nyingine ikiwa Rwanda inatajwa kuwa ya kwanza kufanyika duniani kwani katika
huduma hiyo unaweza kupokea pesa za nchi
husika kama zilivyotumwa
Huduma
hiyo ilishuhudiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania bw BEN RUGANGAZA pamoja
na balozi wa Tanzania nchini Rwanda,ambapo wote kwa pamoja wameipongeza kampuni
ya tigo kwa kufanikisha huduma hiyo ambayo inatajwa kuwa ya kwanza kutokea Tanzania
na duniani kwa ujumla.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi wa tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa baada ya
mteja kupokea pesa ikitokea baina ya nchi hizo mbili mteja anaweza kuitumia
kulipia huduma zote za tigo zinazopatikana katika tigo pesa au tigo cash kwa Rwanda.
Amesema
kuwa huduma hii itaokoa muda mwingi sana ambao wateja wake wanchi hizo mbli
walikuwa wanaupoteza katika kutuma pesa huku akitaja jinsi ya kuipata huduma
hiyo kuwa ni *150*90# ka Tanzania huku
wale walioko Rwanda wakipiga *200*7#.
MKURUGENZI WA TIGOTANZANIA BW DIEGO GUTIERREZ AAKIZUNGUMZA KATIKA HAFLA HIYO LEO |
No comments:
Post a Comment