WAFANYAKAZI WAKIFUATILIA KWA MAKINI
MKUTANO HUO, WOTE KWA UMMOJA WAO WAMEAZIMIA KUTOFANYA KAZI MPAKA
FEDHA YAO YA MWEZI WA KWANZA MPAKA WA TATU ILIPWE TENA KATIKA ONGEZEKO
WALILOAHIDIWA KATIKA VIKAO MBALIMBALI.
WAFANYAKAZI
WA SHIRIKA LA RELI HAPA NCHINI MAPEMA HII LEO WAMEWEKA VIFAA VYAO VYA KAZI
CHINI NA KUISHINIKIZA UONGOZI WA SHIRIKA HILO KUWALIPA STAHILI ZAO KAMA
ILIVYOKUBALIWA NA WAZIRI MKUU,
WAFANYAKAZI HAO AMBAO WAMEKUWA WAKIHITAJI MALIPO YAO KUONGEZWA KUTOKA
200000 HADI LAKI 400000 WAMESEMA HAWATATOKA KATIKA VIWANJA HIVYO WALIVYOFANYIA
MKUTANO HADI HAPO KATIBU MKUU WA WIZARA ATAKAPOTATUA TATIZO LAO,
INADAIWA KUWA WAZIRI MKUU ALISHAKAA NAO NA KUWAAHIDI MATATIZO YAO KUPATIWA
SULUHU LAKINI MPAKA SASA, HAKUNA CHOCHOTE KIPYA KILICHOFANYIKA, HATUA AMBAO
INATAFSIRIWA NA WAFANYAKAZI HAO KUWA NI UBABAISHAJI WA HALI YA JUUU
KATIKA HATUA NYINGINE WAFANYAKAZI HAO WAMEMTAKA MKURUGENZI WAO KUACHIA NGAZI
ILI KUPISHA KUVU KAZI MPYA KUINGIA KULETA MABADILIKO KATIKA TAASISI HIYO YENYE
MIGOGORO MINGI NA YA KILA SAAA
KINACHOONEKANA MKURUGENZI AMESHACHOKA HANA JIPYA CHA KUFANYA ILI KUTATUA TATIZO
HILI HIVYO NI VYEMA BASI AKAPATIKANA MKURUGENZI MPYA ATAKAYELETAMABADILIKO
KATIKA TAASISI HII YA UMMA.
|
No comments:
Post a Comment