Chama
cha Demokrasiana Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Chalinze kimeanza mchakato wa ndani
wa kupata mgombea ubunge kwa ajili ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika
mapema mwezi Aprili, mwaka huu, ambapo fomu za uteuzi zimeanza kutolewa kwenye Ofisi
Jimbo, kuanzia tarehe 4 Machi na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu hizo itakuwa
tarehe 7 Machi 2014, saa 10.00, jioni.
Kura
za maoni ndani ya chama, zitafanyika tarehe 8 Machi katika Mji wa Chalinze na kufuatiwa
na kikao cha kamati ya utendaji ya jimbo ili kufanya uteuzi wa awali kwa mujibu
wa Katiba ya chama na hatimaye kikao cha Kamati Kuu kufanya uteuzi wa mwisho ili
kupata mgombea atakayeshindana na wagombea wa vyama vingine.
Mpaka
sasa wagombea waliochukua fomu kwenye ofisi ya jimbo ni watatu (3) na wagombea wengine
watatu (3) wamechukulia fomu Ofisi za Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam,
hivyo hadi sasa idadi ya wagombea waliotambuliwa rasmi ni sita.
Tunatumia
nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania, hususan wanachama wa CHADEMA, kuwa fomu
za kuwania uteuzi wa ndani zinaendelea kupatikana sehemu tatu, Makao Makuu ya
Chama, Ofisi ya Jimbo la Chalinze na kwenye tovuti ya chama www.chadema.or.tz
No comments:
Post a Comment