Saturday, March 1, 2014

HAYA NDIO MATOKEO YA MWISHO YA MCHEZO WA YANGA NA WAARABU WA MISRI.CHEKI NA PICHA ZA MCHEZO WOTE HAPA

MCHEZO KATI YA YANGA NA ALAHAL ULIOKUWA UNAFANYIKA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM UMEMALIZIKA HAPA UWANJANI NA YANGA IMEIBUKA KIDEDEA KWA KUWAZIBUA WAMISRI HAO KWA BAO MOJA KWA BILA BAO LILILOTIWA KIMYANI NA MCHEZAJI WA YANGA NADIR HAROUB KANAVARO KATIKA DKIKA YA 82 YA MCHEZO HUO.TIMU HIZO ZITAREJEANA HUKO CAIRO WIKI IJAYO AMBAPO YANGA WANATAKIWA KUJIPANGA UPYA KABISA KWANI GOLI MOJA HALITOSHI KUWAHAKIKISHIA USHINDI.

HIVI SASA

 Kikosi cha Yanga 
 Kikosi cha Al Ahly
 Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Mrisho Ngassa akiondoka na mpira huku Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri akitafuta namna ya kumzuia katika Mchezo unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika na hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akitafuta namna ya kuwatoka mabeki wa Timu ya Al Ahly ya Misri katika Mchezo unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika na hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
 Kiungo mchezeshaji wa Yanga,Haroun Niyonzima akizuiwa na Beki wa Timu ya Al Ahly ya Misri,Ramy Abdel Aziz katika Mchezo unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam hivi sasa.Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika na hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Kipa wa timu ya Al Ahly ya Misri,Sherif Ekramy Ahmed akida moja ya hatari iliyokuwa ikielekeshwa langoni kwake na Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza.


No comments: