Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yenye jukumu la kusimamia sekta
ya Vijana nchini imeandaa Kongamano la Vijana kutoka Vyuo vya Elimu ya
Juu kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano Wetu Miaka 50
tangu kuzaliwa kwake.
Kongamano
hili la Vijana kuhusu Muungano linafanyika Jumapili Machi 30, 2014
kuanzia Saa 5:00 Asubuhi katika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam
na litarushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa, TBC One na TBC
Taifa.
Kongamano
hili ni sehemu ya sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar tangu kuasisiwa kwake na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Mzee Abeid Aman Karume aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar Aprili 26, 1964.
Kauli mbiu ya sherehe za Miaka 50 ya Muungano ni “UTANZANIA WETU NI MUUNGANO
WETU, TUULINDE, TUUIMARISHE NA KUUDUMISHA”.
Lengo la Kongamano hili ni kuzungumzia Wajibu wa Vijana katika kuimarisha Muungano ambao mwezi ujao unafikisha miaka 50.
Washiriki wa Kongamano hili ni vijana 300 kutoka Vyuo vya Elimu ya Juu vilivyopo Tanzania Bara na Zanzibar.
Washiriki
wa Kongamano hili watapata fursa ya kuwasikia watoa mada ambao ni
Wahadhiri wa Vyuo Vikuu Prof. Gaudens Mpangala atakayewasilisha mada
kuhusu Wajibu wa Vijana katika Kuimarisha Muungano, Miaka 50 tangu
kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Aidha mada kuhusu
Mapendekezo ya Katiba Mpya kwa Mustakabali wa Muungano wetu
itawasilishwa na Prof. Issa Shivji.
Waandishi
wa Habari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari nchini wanakaribishwa
kushiriki kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu kongamano hili.
Imetolewa na Idara ya Habari – MAELEZO
29 Machi 2014
No comments:
Post a Comment