Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili
tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la
Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu
Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu April 10
20014 baada ya Waziri wa Fedha kupata safari ya kikazi nchini
Marekani,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato huo wa Katiba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza Benki
zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo
zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge
ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30.
No comments:
Post a Comment