Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto)
akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan
nchini Masaki Okada (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na
Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam.
Balozi wa Japan nchini Masaki Okada (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam.
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za
Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali
ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) . Kauli
hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt.
Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada
huo ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini
nchini. Katibu Mkuu Dkt.Likwelile
alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili kuongeza
tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo
wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.
Katibu Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo
serikali inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo
inawaajiri watanzania takribani asilimia 74 nchini. Aidha, Katibu Mkuu
aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa
Japan nchini Mh.Masaki Okada kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaki Okada alisema kuwa msaada
uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya
kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo
ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa
mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria
ulianzishwa tangu mwaka 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa
unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.
Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini Okada,
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu
Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na
ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo
chenye tija nchini.
Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia
kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na
utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao
bora na hivyo kupunguza umasikini nchini.
No comments:
Post a Comment