RATIBA KAMILI YA MAZIKO YA MZEE GURUMO IKO HAPA(R.I.P)
Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo na mtoto wa kwanza wa Marehemu Mzee
Gurumo Ndg Abdallah Gurumo amesema kuwa leo saa 10 jioni kutakuwa na
kisomo hapa nyumbani kwa Marehemu eneo la Tabata Kisukulu ambapo
Watanzania wote wanakaribishwa.
Baada ya kisomo saa 3 ya asubuhi kesho April 15 mwili wa Marehemu
utaletwa nyumbani kwa ajili ya swala kisha saa 4 asubuhi safari ya
kuelekea kijiji cha Masaki wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani itaanza kwa
ajili ya maziko ya Mzee Gurumo.
Kwa mtu usiyepafamu nyumbani kwa Mzee Gurumo ukiwa unatokea Ubungo kabla
ya Mwananchi kuna kituo kinaitwa Garage shukia hapo kisha ulizia mtu
yoyote atakuelekeza pia kwa wewe unaetokea Tabata,Buguruni au Tazara
shukia hapo Garage kituo baada ya Mwananchi.
No comments:
Post a Comment