Kampuni ya Smile communications
Tanzania (Smile), inayoongoza kwa kutoa huduma za internent Dar es Salaam
na Arusha, leo imeendesha droo ya mwisho katika droo za wiki kuhitimisha
promosheni yao ya “Shinda iPad” ambapo wateja 13 wenye bahati wamejinyakulia
iPad kila mmoja.
Katika ofa hiyo, wateja wapya wa Smile walitakiwa kununua
kifaa cha Mi-Fi au Router kutoka katika maduka au vibanda vya Smile ndani ya
mwezi Machi ili kupata nafasi ya kushindania moja kati ya iPad 13
zilizokuwa zikishindaniwa.
Promosheni hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na Bodi ya Michezo
ya Kubahatisha (TGB) imewazawadia wateja tisa (9) kutoka Dar es salaam na (4)
kutoka Arusha. Droo ya mwisho imefanika leo makao makuu ya Smile Dar es
Salaam ambapo washindi wanne wa mwisho wamechaguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Masoko wa
kampuni hiyo Linda Chiza, amesema kampuni yake imetoa zawadi ya toleo jipya la
iPad lililowezeshwa katika tekinlojia ya 4GLTE zikiwa na vivurushi vya
GB5 za intaneti.
“ Tunawapongeza washindi na wote walioshiriki na
kutembelea kwenye sehemu tunazotolea huduma” alise Chiza na kuongeza kuwa “
kila mwezi tunakuwa na kitu cha kuwafanya watabasamu tutawajulisha nini
kinafuata.
No comments:
Post a Comment