Wednesday, April 2, 2014

EXCLUSIVE---MAMA KANUMBA AJITOKEZA MBELE YA WANAHARI MUDA HUU,ATOA UTARATIBU MZIMA WA KUMWAZIMISHA MWANAE

Raisi wa shirikisho la filamu tanzania SAIMON MWAKIFAMBA akizungumza na wanahabari jijini dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya kanumba day yatakayoadhimishwa jijini dar es salaam wiki ijayo,pembani ni mama mzazi wa zSTEVEN KANUMBA marehemu
shirikisho la filamu tanzania kwa kushirikiana na familia ya marehemu KANUMBA imetangaza utaratibu kamili wa kumuenzi marehemu kanumba leo ambapo utaratibu utakuwa hivi.siku ya jumapili ya tarehe sita wasanii wa filamu na familia yake watakuwa katika kituo cha watoto yatima huko sinza ambapo watatoa msaada mbalimbali kama ishara ya kumkumbuka kwani na yeye alikuwa akipenda sana kukisaidia kituo hiko.siku ya jumatatu ambayo ndiyo tarehe yenyewe ya kifo chake ibad ya kumwombea itafanyika katika kanisa lililopo huko kimara suka na baadae kuelekea makaburini kuweka mashada ya maua kama ishara ya kumkumbuka,jioni sasa burudani itahamia dar live ambapo burudani mbalimbali zitakuwepo kutoka kwa wasanii mbalimbali,utaratibu huo umetolewa muda huu na mama kanumba na shirikisho la filamu tanzania Aidha katika maadhimisho hayo pia yatatumika katika kuzindua kanumba foundation
steve nyerere alikuwepo katika mkutano huo na wanahabari
Cloud na steve wasanii wa filamu tanzania pembeni ni mdogo wa steve kanumba seth bosco

No comments: