
Sehemu ya muhtasari wao inasema hivi
kama nilivyoinukuu kwenye Taarifa ya TWAWEZA kwa Vyombo vya Habari: ----
Sauti za Wananchi imebaini kuwa, uungwaji mkono ni mkubwa sana miongoni
mwa wananchi wa Tanzania Bara kwenye vifungu vingi vilivyowasilishwa katika
rasimu ya kwanza ya katiba na vimebaki katika rasimu ya pili.
Vifungu hivyo ni vile vinavyohusu kuwepo
kwa uwajibikaji zaidi kwa watumishi wa umma, kuimarisha utaratibu wa dola ili
kudhibiti na kuwajibisha wabunge, hasa wabunge kuwajibika kwa wapiga kura wao,
na kuongeza ushindani zaidi wa kisiasa. Utafiti pia unaonesha kuwa Watanzania
wangeipitisha rasimu ya katiba bila shida ikiwa Watanzania sita kati ya kumi
wameonesha kuwa wangeipigia kura ya Ndiyo.
Tanzania Bara ni wananchi asilimia 65
na Zanzibar ni wananchi asilimia 62 wanaoikubali rasimu ya sasa. Hata hivyo,
suala la muundo wa serikali bado ni tata. Idadi kubwa ya Wazanzibari (80%)
walisema wanataka muundo wa serikali tatu, ikilinganishwa na chini kidogo ya
nusu (43%) ya wahojiwa kutoka Tanzania Bara.
Aidha, zaidi ya nusu ya wahojiwa kutoka
Zanzibar (53%) walisema kuwa uungaji mkono wa rasimu ya sasa ya katiba
utategemea muundo wa serikali tatu. Sauti za Wananchi na Wasemavyo Wazanzibari
pia ziligundua kuwa wananchi kutoka Tanzania Bara wamepata fursa kufuatilia midahalo
na mijadala ya katiba mpya.
Wananchi sita kati ya kumi (62%) kutoka
Bara wamekuwa wakifuatilia kwenye radio, luninga au mijadala ya wazi, wakati
wenzao wa Zanzibar, ni wananchi watatu tu kati ya kumi (30%) ndiyo wamefanya
hivyo.
No comments:
Post a Comment