(Picha zote na Frank Mvungi )
Na Georgina Misama-MAELEZO
MFUKO wa Kuhifadhi Wanyamapori
Tanzania (TWPF) umebuni miradi ya maendeleo kama vyanzo vya mapato ili
kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa bajeti katika kutekeleza majukumu
yake.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji
Mkuu wa mfuko huo Bw John Muya wakati wa mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo.
Alisema kwamba mfuko umebuni
miradi ya maendeleo ili kujiendeleza kwa kuongeza mapato ambapo alitaja
miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Jengo la Kakakuona na Pori la akiba la
Pande.
Miradi mingine ni Bustani ya
Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila-Songea na kambi
ya Utalii katika Pori la akiba Selous.
Muya alisema TWPF husimamia
ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa uwindaji wa kitalii na wa wenyeji,
utalii wa picha, biashara ya wanyamapori hai na mazao yatokanayo na
wanyamapori, mashamba na bustani za ufugaji wa wanyamapori.
Kwa upande wake Kaimu Katibu
Tawala wa TWPF Bi. Antonia Raphael alisema mfuko hugharamia shughuli
mbalimbali za usimamizi wa wanyamapori ikiwa ni pamoja na usimamizi wa
maeneo ya jumuia za hifadhi za wanyamapori (WMAs), kutoa elimu ya
uhifadhi kwa jamii na uendelezaji wa miundombinu katika mapori ya akiba.
Mfuko hufanya malipo ya kifuta
machozi kwa wananchi ambao ndugu zao wameuawa au kujeruhiwa na
wanyamapori ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu Januari –Machi 2014,
kiasi cha shilingi milioni 9 kililipwa kwa ajili waliouwawa.
No comments:
Post a Comment