Sunday, June 15, 2014

EXCLUSIVE---TASNIA YA HABARI KWISHA HABARI YAKE-SAID KUBENEA KUMBE NA YEYE NI MWANACHAMA HALALI WA CHAMA HICHI CHA SIASA,AKITETEA WAZIWAZI LEO


SAID KUBENEA alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano wa vijana wa chadema CHASO leo jijini dar es salaam
             Tasnia ya uandishi wa habari Tanzania sasa imeanza kuporomoka kimaadili ikiwa ni pamoja na wanahabari kujikita katika siasa chafu na kuacha Jukumu lao la kuwaelimisha na kuwahabarisha watanzania na badala yake baadhi ya wanahabari wameanza kuonyesha dhahiri kuwa wao ni wanachama wa vyama vya siasa huku wakivitetea hadharani kinyume na maadili ya uandishi wa habari yanavyotaka.
           
         Hayo yamejidhihirisha leo katika mkutano wa jumuiya ya wanafunzi wa elimu ya juu toka CHADEMA (CHASO) ambapo mmoja wa waandishi wa habari maarufu nchini Tanzania SAID KUBENEA alikuwa mzungumzaji katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine ameonekana kuikacha taaluma yake na kujikita katika kuzungumza siasa kitu ambacho ni hatari sana katika tasnia ya habari Tanzania,
       
       Mwandishi wa mtandao huu  ambaye alikuwa eneo la tukio ameshughudia mwenyewe mwandishi huyo akionyesha wazi kuwa yeye ni adui namba moja wa chama kilichoko madarakani huku akionekana wazi kuwa yeye ni mpenzi wa chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA,
       
     “Nani kasema kuwa ccm haiwezi kuondoka madarakani,unadhani kukiondoa madarakani imeshindikana au,ccm lazima itaondoka tu haina ujanja tena,nachokisema ni kuwa lazima chadema tujipange na tuhakikishe tunawashika ccm kila upande na uwezo wa kushinda upo kwa asilimia kubwa sana”alisema KUBENEA maneno ambayo yameonyesha dhahiri kuwa yeye ni mwanachama mtiifu wa chama cha CHADEMA na sera zake.
       
        Mwandishi huyo ameendelea kusema nchi ya Tanzania imefika sehemu mbaya sana kiuuchumi,kijamii na kila kitu na sababu kubwa ya kufika hapo ni kwa sababu ya uwepo wa serikali ya ccm madarakani
        
         “Mimi nasema hivi ndugu zangu,nchi ya Tanzania imefika mahali pabaya sana,umaskini unaongezeka kadiri siku zinapokwenda,kila kitu hakieleweki na yote hii ni kwa sababu ya serikali ya CCM na viongozi wake,kuna kila haja ya kuhakikisha mwakani katika uchaguzi tunawangoa mara moja la sivyo tutateseka sana”alisema kubenea.
       
        Katika mkutano huo umehudhuriwa na  MABERE  MARANDO ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CHADEMA ambapo katika mazungumzo yake ametangaza rasmi kuwa hatogombea nafasi yoyote katika chaguzi zijazo ndani ya chama, jambo ambalo SAID  KUBENEA amewataka wanachadema kulipinga na kumuomba mzee MARANDO agombee katika nafasi yoyote .
      
      “Wanachadema jamani naomba maneno ya MARANDO kuwa hatogombea uongozi ndani ya chama muyapinge kwa moyo mmoja kabisa lazima mzee huyu agombee uchaguzi ujao katika nafasi yoyote,jamani au mnasemaje wanachama”alisikika KUBENEA akisema.
Vijana wa CHADEMA wakimsikiliza kwa makini mwandishi huyo
              Wachambuzi wa maswala ya habari nchini Tanzania wameieleza HABARI24 kuwa kitendo cha mwandishi huyo ambaye ni mkurugenzi wa mwanahalisi forum kuanza kujikita katika siasa ni kibaya kwani sasa inaonekana wazi kuwa anatumika na wanasiasa kwa ajili ya maslahi ya vyama vyao.

      “Daah kama ni kweli KUBENEA  katamka maneno hayo mbele za watu sasa tasnia ya uandishi wa habari imeharibika,hawezi kuwatetea tena wananchi,wameshamnunua huyo”alisema mwanahabari mmoja ambaye hakutaka kuweka jina lake wazi kwa sababu za kiusalama.

      SAID KUBENEA  ni moja kati ya wanahabari nchini Tanzania waliowahi kufanya vizuri hadi kupatwa na matatizo likiwemo la kuwagiwa tindikali kutokana na kufichua maovu,lakini kwa sasa anaonekana wazi kuwa mwandishi huyo ambaye alikuwa tegemeo la wanyonge sasa ameamua kuingia rasmi katika siasa chafu jambo ambalo linatajwa kumshusha ufanisi wake katika kuwatetea wanyowe wanchi hii


No comments: