Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Wakimbizi, Jenita Ndone wakati alipokuwa anaeleza majukumu ya Idara hiyo ambayo inasimamia masuala ya wakimbizi nchini, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Manzi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) akimuuliza maswali Afisa wa Idara ya Uhamiaji, Mathew Ikomba kuhusu matatizo mbalimbali likiwemo baadhi ya wananchi wanailalamikia Idara hiyo kuhusu uombwaji wa rushwa wakati wanapoomba kupatiwa Hati ya Kusafiria (pasipoti). Malemi aliitaka idara hiyo ifuate haki wakati wananchi wanapoomba pasipoti. Wizara na Idara zake inashiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NCHI
WIZARA YA MAMBO YA NCHI
No comments:
Post a Comment