ONYO KUHUSU CLUB ZINAZOCHEZESHA
NGOMA AINA YA BUNYEROBUNYERO KINYUME CHA SHERIA
Jeshi
la Polisi Kanda Maaluum ya Dar es salaam limetoa onyo kali kuhusu ngoma mpya
ilyoibuka hivi karibuni katika club za usiku ambazo ngoma hizo ni za aibu na
kinyume cha maadili.Hakuna tofauti kubwa kati ya ngoma ya Bunyerobunyero na
vigodoro ila tofauti yake ni maeneo.
KAMISHNA KOVA |
Vigodoro hufanyika mitaani sehemu ambazo ni makazi ya watu wa hali ya
kawaida wakati hufanyika katika club maarufu za usiku ambazo huhudhuriwa na
watu wenye kipato cha kati na cha juu. Onyo
hili linatolewa kwa sababu huu ni mtindo ulioko sehemu mbali mbali za jiji la
D’Salaam.
MFANO HUU HAPA |
Uchunguzi unafanyika na endapo
itabainika ngoma hizo kuendelea kuchezwa basi Jeshi la Polisi pamoja na
halmashauri za miji itakuchukua hatua mbali mbali za kisheria ikiwa ni pamoja
na kuzifungia club hizo.
No comments:
Post a Comment