Friday, July 4, 2014
STORY YA SHEIKH ALIYELIPULIWA NA BOMU AKILA DAKU HUKO ARUSHA IKO HAPA
Sheikh wa msikiti wa Qiblatan ,Sood Ally Sood (37)uliopo
eneo la Kilombero jijini Arusha, amelipuliwa na bomu la kurushwa kwa mkono nyumbani kwake wakati akila daku na kujeruhiwa vibaya.
Sheikh huyo amejeruhiwa miguu yake yote miwili na mapajani pia Kifuani na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote miwili.
Aidha mbali na Sheikh huyo,mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es salaam naye amejeruhiwa vibaya na wote wamelazwa katika bhospital ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya matibabu.
Akizungumza hospitalini hapo sheikh,Sood amesema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la majengo ya chini ,usiku wa kuamkia leo majira ya saa 5 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni .
Amesema alishangaa kusikia mlio mkubwa ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ,ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumbani katika nyumba hiyo .
Ameongeza kuwa wahusika wanafahamika maana walishawahi kumtishia kupitia waraka wa maandishi pamoja na kumfyatulia risasi.
Amesema kuwa siku tatu kabla ta tukio hilo alikoswakoswa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha polisi jijiji hapa juu ya tukio hilo,hata hivyo kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.
Sood ambaye ni kiongozi Alswasun kanda ya kaskazini amekuwa
akitofautiana na waamini wenzake kutokana na msimamo wake mkali wa kutokukubaliana na makundi ya kigaidi yanayojiita jihadi ,yanayotokana na vijana wenye msimamo mkali yaliyopo ndani ya msikiti huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment