Balozi wa palestina nchini Tanzania NASRI ABU JAISH akionyesha baadhi ya picha za mauaji yanayoendelea nchini kwao |
Ubalozi wa palestina nchini Tanzania umeliomba
baraza la usalama la umoja wa mataifa kutafuta suluhu ya mauaji yanayoendelea
nchini palestina yanayofanywa na taifa la Israel .
Akizungumza na wanahabari jijini dare s salaam
balozi wa palestina nchini Tanzania NASRI ABU JAISH Amesema kuwa viteno vya
mauaji vinavyoendelea nchini pallestina ni kinyume na haki za binadamu
ukuzingatia kuwa vinawalenga wanawake na watoto na vinafanywa kwenye ardhi ya
wapalestina.
Aidha balozi huyo ameongeza kuwa baraza la usalama
la usalama la umoja wa mataifa limekuwa halitendi haki katika mikutano
mbalimbali ya kuleta suluhu ya mgogoro huo kwani ni mgogoro wa muda mrefu na
umekuwa ukikuwa kadiri siku zinavyoizidi kwenda.
Balozi huyo Amesema kuwa ubalozi wao unaamini kuwa
nchi ya Tanzania ina nafasi kubwa katika kuwa suluhu ya mgogoro wao ikiwa ni
pamoja na kuyashawishi mataifa mengine ya Africa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro
wao.
Katika mauaji yanayoendelea katika ardhi ya
pelestina hasdi sasa wananchi 104 na wengine 600 wamejeruhiwa na wengi kati yao
wakiwa ni watoto na wanawake.
Katika hatua nyingine balozi huyo amevishutumu
vyombo vya habari vya magharibi kwa kuegemea upande mmoja wa Israel jambo
linalopelekea kutopatikana kwa suluhu ya kudumu ya mgogoro huo
No comments:
Post a Comment