Afisa habari wa NEW HOP FAMILY GROUP, FLORA METHEW akizungumza na wanahabari leo |
Kituo cha kulelea watoto yatima nchini Tanzania cha
NEW HOPE FAMILY GROUP kilichopo kigamboni jijini Dar es salaam kimeandaa futari
kwawatoto hao siku ya chungu cha 20 itakayofanyika katika fukwe za Islamic club
gezaulole kigamboni.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es salaam afisa habari wa kituo hicho FLORA METHEW
Amesema kuwa lengo la kuandaa futari hiyo ni kuendeleza mahusiano mema miongoni
mwa makundi mbalimbali ya kijamii pamoja na kuangalia namna ya kuwasaidia.
FLORA Amesema
kuwa futari hiyo itaongozwa na sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambapo
itafanyika siku ya mfungo wa 20 futari ambayo itawashirikisha watoto yatima
kutoka vituo mbali mbali pamoja na watu wenye ulemavu.
Kituo hicho kimewataka wadau mbalimbali
kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuangalia kwa pamoja jinsi ya kuwasaidia
watu wenye mahitaji mbalimbali wkiwemo watoto yatima na walemavu.
No comments:
Post a Comment