Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katiba Tanzania HEBRON MWAKAGENDA akizungumza na wanahabri leojijini Dar es salaam |
Na Karoli Vinsent na Exaudi Mtei
Wakati
mchakato wa katiba Tanzania ukiwa ni kama kitendawili kisicho na majibu sahihi
kutokana na mchakato huo kuvurugika na kukosa mwelekeo,nao jukwaa la katiba Tanzania JUKATA wazidi kumtupia lawama zote za
kuvurugika bunge hilo mwenyekiti wa bunge hilo mh SAMWEL SITTA na
kudai kuwa ndiye aneyeuvuruga mchakato huo baada ya kugeuza Bunge hilo kama
kikao cha Chama cha Mapinduzi CCM.
Akizungumza
na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam kaimu mwenyekiti wa jukwaa la
katiba Tanzania HEBRON MWAKAGENDA amesema kuwa JUKATA wamekuwa wakifwatilia
mchakato huu wa bunge ka katiba kwa wiki mbili hizi na kubaini mapungufu
makubwa sana ambayo yanatokea jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa mwenyeikiti wa
bunge hilo hana nia wala dhamira ya kulipatia taifa katiba mpya ya watanzania.
Wanahabari mbalimbali wakiwa wanamsikiliza kiongozi huyo wakati wa mkutano |
Bw
MWAKAGENDA amesema kuwa swala la mahudhurio ya wabunge wanaoshiriki katika
kamati mbalimbali za bunge hilo yamekuwa madogo sana na yasiyo ya kuridhisha
ikiwa ni pamoja na wabunge wengi kutokuhudhuria katika kamati hizo pamoja na
kusaini kulipwa posho za siku jambo ambalo amesema kuwa ni wizi mpya kwa
watanzania,
“Kwanza
bunge la katiba linaonyesha kuwa wajumbe 441 wamehidhuria lakini uchunguzi wetu
unaonyesha kuwa hawa ni wale wote ambao wamewahi kufika na kusaini kwenye
kitabu cha mahudhurio wengine wao takribani 100 tuligundua kuwa hawapo
bungeni wakiwemo mawaziri wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar pamoja na baadhi ya
viongozi wa kamati”amesema MWAKAGENDA.
Ameongeza kuwa mambo mengine ambayo yanalifanya
bunge hilo kuvurugika ni pamoja na
kukosekana kwa muafaka na maridhiano ya kitaifa,matumizi mabaya fedha ikiwa ni
pamoja na Wajumbe kulipwa bila kuhudhuria bungeni,kukosekana kwa theluthi mbili
toka Zanzibar ili kupitisha katiba,pamoja na uondoaji wa vifungu muhimu kwenye
rasimu mambo ambayo amesema kuwa mwenyekiti SAMWELI SITTA ameyafumbia macho na
kijifanya kama hayaoni huku akiwa anajua wazi kuwa anauzika mchakato huo.
“Huyu mzee hatujamwelewa kabisa,sisi tumekaa
tumezungumza naye tukamuuliza atueleze swala la theluthi mbili hawa wajumbe
watapatikana wapi hajatupa jibu la kuridhisha na ukimwona ni kama mtu ambaye
ameshachanganyikiwa,anapambana na kila anayekuja mbele yake,iwe
mwandishi,mwanaharakati,mbunge,yeye amekaa kujihami tu,sasa hali hii sio nzuri
kwa mchakato muhimu kama huu”alisema kiongozi huyo wa JUKATA.
Katika hatua nyingine JUKATA wamemwomba raisi
KIKWETE kiusimamisha mchakato huu wa katiba hadi kipindi kingine kutokana na
kuonekana wazi kuwa hauwezekani na kusema Tanzania imekuwa na michakato mingi
ambayo sisi kama taifa hatuwezi kuiendesha kwa wakati mmoja na kupata katiba
bora,
“Kusema ukweli taifa sasa lina michakati mingi sana mfano mchakato wa vitambulisho vya taifa,uchaguzi wa serikali
za mitaa,daftari la kudumu la kupiga kura na michakato mingine mikubwa,hii
haitaki usome sana ndo uelewe ni kutumia busara tu kwamba huu mchakato wa
katiba hautawezekana tena,sisi tunamwomba mh RAIS KIKWETE awasikilize
watanzania na kuusimamisha mchakato huu wa katiba ili tujipange upya kuanza
tena.
Mchakato wa katiba umekuwa ukiendelea jijini Dodoma
bila ya mariano na wajumbe waliotoka wa UKAWA huku kukiwa na taarifa kuwa rais
amekubali kukutana nao wiki hii kwa ajili ya mazungumzo ya kuunasua mchakato
huu.
No comments:
Post a Comment