Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano toka Mamlaka ya Elimu Tanzania Bi Sylvia Lupembe akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu jitihada wanazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu,wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakiwasikiliza wawasilishaji toka Mamlaka ya Elimu Tanzania, KCB, TOTAL, Social Action Trust Fund (SATF) leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Uhusiano toka benki ya KCB Bi. Christina Manyenye akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mipango waliyoiweka kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania katika kuendeleza na kuinua sekta ya Nchini.kushoto ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya. Afisa Rasilimali Fedha toka taasisi isiyo ya kiserikali ya Social Action Trust Fund (SATF) Bw. Timotheo Tenga akiwaeleza jambo waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Sheria na Uhusiano toka kampuni ya uuzaji na usambazaji wa mafuta ya TOTAL Bi. Masha Msuya
No comments:
Post a Comment