Tuesday, September 30, 2014
TAARIFA KWA WATANZANIA KUHUSU ZITTO KABWE NA CHAMA CHA ACT
ACT-TANZANIA.
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPERANCY.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Ndugu wanahabari kumekuwa na utaratibu wa habari zinazoupotosha umma wa watanzania kuhusu chama chetu cha ACT-Tanzania.
Katika gazeti la mwanahabari toleo na 117 la tarehe 29/09/2014 katika ukurasa wake wa mbele iliandikwa "MKAKATI WA KUKIPA NGUVU CHAMA CHA KIPYA CHA ZITTO KABWE WAVUJA".
ACT WAZIDI KUIANDAMA CHADEMA,VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA LEO WATANGAZA KUHAMIA ACT
CHAMA kipya cha Siasa cha Alliance for Change and Transparence-Tanzania ACT kiamezidi kukipasua chama cha Demokrsasia na Maendeleo CHADEMA kutokana wimbi la wanachama kukihama chama hicho na kujiunga na ACT.
Wanachama hao kutoka CHADEMA wamejiunga na ACT leo na kupokelewa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar Es Salaam wa chama hicho Hamisi Said Chambuso na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari,ambapo Aliyekuwa mwenezi wa baraza la Wanawake la Chadema ,Jimbo la Kawe Batuli Abdalah naye alijiunga na ACT ,
TIGO WASHIRIKI KIKAMILIFU KUSAIDIA KUINUA SOMO LA HESABU KWA WANAFUNZI WA TANZANIA
Wanafunzi nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vifaa vya
electronic mfano computer na simu za mkononi
kama njia moja wapo ya kujifunzia na kupata elimu badala ya kutumia kwa
nzia zisizofaa.
UPIGAJI KURA WA RASIMU INAYOPENDEKEZWA WAENDELEA LEO BUNGENI MJINI DODOMA.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia Hassan Suluhu akipiga kura yake kwa ajili ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Makamu wa Pili wa Zanzibar ambaye pia Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Seif Ali Idd akiipigia kura Rasimu ya Katiba inayopendekezwa Bungeni hapo leo 30 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
MICROSOFT LAUNCHES MOBILE MATHEMATICS IN TANZANIA
RIITA VANSK from Director general of Nokia mathematics project |
Microsoft, in partnership with the Ministry of
Communications, Science, Technology and TigoTanzania,have officially launched an
innovative mobile education service called Nokia Mobile Mathematics. This
service is now being managed by Microsoft, after the company acquired
substantially all of Nokia’s devices and services business.
Nokia Mobile Mathematics is aservice that enables learners across Tanzania
toaccess quality mathematics content in an engaging and interactive manner
directly from their mobile phones, completely free.
The Guest of honour hon JOHN MNGONDO deputy permenent secretary minister of communication science and Technology speak during the lounching of that services |
MAMBO SITA AMBAYO BARAZA LA WAZEE LA CHADEMA LIMEITAKA CCM KUWATIMIZIA WAZEE WA TANZANIA
Mwenyekiti wa Baraza la wazee CHADEMA mzee HASHIM JUMA ISSA (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam kushoto ni makamu wake SUZAN LYIMO na RODRIC LUTEMBEKA katibu wa baraza hilo |
Ikiwa kesho tarehe 1,mwezi wa kumi
dunia inaadhimisha siku ya wazee duniani
baraza la wazee la chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA limeibuka na mambo
sita ambayo wameitaka serikali ya CCM kuwajibu wazee kwani ndio kero za wazee
kwa muda mrefu.
Akizungumza na waandiishi wa habari
makao makuu ya chama hicho muda huu mwenyekiti wa baraza hilo mzee HASHIMJUMA
ISSA ametaja mambo hayo kuwa ni
KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS KILICHOTAJWA LEO KIPO HAPA
Wachezaji 26 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kwa ajili mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kocha Mart Nooij ambaye yuko Cairo, Misri kwenye kongamano la makocha la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kitaingia kambini Oktoba 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Monday, September 29, 2014
PICHA TATU ZA MAANDAMANO YA CHADEMA LEO MANZESE KUPINGA BUNGE LA KATIBA
NANI ANAJALI KWA UFISADI HUU WA WAKUBWA
Tanzania ni nchi ya ajabu kwa mwanadamu makini kuweza kuishi. Ni nchi inayoshangaza sana, ingawa raia wake hawaonyeshi kushangazwa na matukio kadhaa yanayotokea. Naizungumzia Tanzania nchi niliyoishi kwa miongo kadhaa tangu nizaliwe. Baada ya nyimbo nyingi za matatizo, dhiki, wizi, rushwa, tabu, magonjwa na kila aina ya shida ambayo mwanadamu wa kawaida anapitia, jawabu kubwa linapatika kwa swali; nani anajali?
HABARI NZURI TOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA LEO
MAMLAKA ya Hali hewa nchini(TMA) imezindua Jarida Maalum lenye kutoa taarifa za matukio ya hali ya hewa kwa mwaka husika ambalo litakuwa likiwapa nafasi wananchi kujua halli ya hewa ya mwaka mzima,
Uzinduzi wa jarida hilo umefanyika Leo Jijini Dar Es Salam na kushuhudiwa na Waandishi wa Habari pamoja na Wajumbe wa bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA),ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt.Agnes Kijaz alisema Jarida hilo linalengo la ekulezea umma hali ya hewa ilivyokuwa katika kipindi cha mwaka husika kwa ufipi,
Saturday, September 27, 2014
NAJUA WAJUA,NATAKA UJUE ZAIDI KUHUSU HILI
Friday, September 26, 2014
HAYA NDIO ALIYOSEMA JAJI WARIOBA JANA NA KUWAACHA WATANZANIA NA MSHANGAO MKUBWA
Akiyataja mambo hayo muhimu ambayo ni maadili ya viongozi wa umma, madaraka ya wananchi, mgawanyo wa madaraka na muungano. “Tutakutana mtaani. Tume tutaendelea kutetea rasimu yetu na wao wawaeleze wananchi kwa nini wameondoa maoni yao yaliyokuwa katika Rasimu ya Pili ya Katiba,” aliongeza kwa ufafanuzi Jaji Warioba.
RAIS KIKWETE ATINGA STUDIO ZA CNN -PICHA ZIKO HAPA
CNN is an American basic cable and satellite television channel that is owned by the Turner Broadcasting System division of Time Warner.
The 24-hour cable news channel was founded in 1980 by American media proprietor Ted Turner. Upon its launch, CNN was the first television channel to provide 24-hour news coverage, and was the first all-news television channel in the United States.
While the news channel has numerous affiliates, CNN primarily broadcasts from its headquarters at the CNN Center in Atlanta, theTime Warner Center in New York City, and studios in Washington, D.C. and Los Angeles.
CNN is sometimes referred to as CNN/U.S. to distinguish the American channel from its international sister network, CNN International.
FAIDI PICHA NANE ZA MAANDAMANO YA CHADEMA LEO JIMBO LA UBUNGO
Wananchi wa jimbo la UBUNGO kutoka chama cha CHADEMA leo wameamua kuandamana kwa kile wanachodai kuwa ni kupinga mchakato wa bunge maalum la katiba unaoendelea ambapo hilo ni tekelezo la agizo la mkutano mkuu wa chama hicho |
PICHA--WAZIRI MKUU PINDA BUNGENI LEO
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Peter Serukamba (kushoto) na Abdulkarim Shah kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Septemba 26, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
KUHUSU MAMBO MAKUBWA WALIYOZUNGUMZA UKAWA NA WANAHABARI LEO JIJINI DAR ES SALAAM USIKOSE HAPA
Mwanasheria wa chama cha democrasia na maendeleo chadema TUNDU LISSU (kushoto) pembeni ni mwenyekiti wa chama hicho mh FREMAN MBOWE pamoja na viongozi wa ukawa walivyokutana na wanahabari leo njijini dar es salaam |
Na Karoli
Vinsent
LICHA ya
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta kujinadi kwamba Theluthi 2 ya
wajumbe inapatikana wakati wa upigaji kura kuipitisha rasimu iliyopendekezwa na Bunge hilo, kwa madai
wajumbe Bungeni hapo wasiokuwepo watatumia hata njia ya Fax,simu pamoja na
“Internet” mtandao kupiga kura,
Nao Viongozi Umoja wa Kutetea Katiba
ya Wananchi UKAWA umemjia juu Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake cha
Kumwacha mwenyekiti wa Bunge hilo Samwel Sitta kwa kuendelea kufanya hujuma kwa
watanzania kwenye mchakato wa katiba,
Kwani Duniani kote hakuna kura
yeyote inayopigwa kwa njia ya simu wala Internet na anavyofanya hivyo samweli
sitta ni kutaka kufanya mambo pasipo kisheria,
Hayo yamesemwa mda huu Jijini Dar
es Salaam na Viongozi wa vyama vikuu vya
upinzani nchini wanaounda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA wakati wa
Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF
Profesa Ibrahim Lipumba alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuyakimbia matatizo
nchi na kwenda nje ya nchi na kushindwa kuliokoa taifa katika hujuma anayofanya Samwel sitta.
“Rais Kikwete amekuwa mtu wa kwenda
Marekani kila wakati yanapotokea Matatizo,na leo anamwacha Samwel Sitta anafanya
mambo ya ajabu, ambayo duniani hayajawai kutokea kura kwa njia ya simu,harafu
Rais Kikwete anashindwa kukemea uragai huu,hivi huyo ni kiongozi gani”Alihoji
Profesa Lipumba
Profesa Lipumba ambaye ni Gwiji la
masuala Uchumi kimataifa alizidi kuzungumza kwa Uchungu ambapo alimshangaa Rais
Jakaya Kikwete kuonyesha ugeugeu kwa watanzania kwani wakati wa Mkutano kati
yake na Vyama vya kisiasa nchini vilivyo chini ya Kituo cha Demokrasia nchini (
TCD).
Katika mkutano huo Rais Kikwete
alikubali wazi kwamba bunge Maalum la sasa aliwezi kuleta katiba cha kushangaza
leo ameshindwa hata kuingilia kati utoto
unaofanywa na Samwel Sitta kwa Watanzania.
Thursday, September 25, 2014
WANAFUNZI WA TAMBAZA WAPEWA SOMO NA TAASISI YA WAANDISI NCHINI
KATIKA kuonyesha imedhamiria kuhakikisha wanapatikana Waandisi bora nchini,Taasisi ya Waandisi Nchini(Istitution of Engineer Tanzania IET) imewataka wanafunzi kuacha kusomea masomo ya sanaa peke yake badala yake wajikite zaidi kwenye masomo ya sayansi ili kulisaidia Taifa liweze kupata waandisi wenye sifa,
TAIFA STARS, BENIN KUCHEZA DAR OKTOBA 12
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inashuka uwanjani Oktoba 12 mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. Programu ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager kwa ajili ya mechi hiyo itatangazwa baadaye na Kocha Mkuu Mart Nooij.
KAULI YA BAWACHA KUHUSU RASIMU ILIYOPENDEKEZWA JANA
HALIMA MDEE mwenyekiti wa BAWACHA akizungumza nna wanahabari Jijini Dar es salaam. |
Baraza la wanawake wa chama cha democrasia na maendeleo chadema BAWACHA wamekuwa wa kwanza kuipinga rasimu ya tatu iliyowasilishwa bungeni jana na kutangaza kuandamana hadi ikuliu ya jiji la dar es salaam kupeleka kilio chao kwa kile walichoitwa kushindwa kuwapa wanawake nafasi stahiki katika rasimu hiyo
Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa baraza hilo BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa kawe HALIMA MDEE amesema kuwa kuwapa wanawake nafasi za uongozi za hamsini kwa hamsini kama rasimu hiyo ilivyoelekeza bado sio kipaumbele cha wanawake wa Tanzania ila kinachofanyika ni kuendelea kuwalaghai wanawake wa Tanzania.
Aidha amesema kuwa rasimu hiyo bado haimjali mtanzania kwani kuna mambo mengi ambayo yameondolewa yalikuwepo kwenye rasimu ya WARIOBA.
Wanawake hao wametangaza kufanya maandamano wiki moja ijayo ambayo amekataa kutaja siku rasmi kwa kile alichokisema kuwa bado wanafanya maandalizi ambapo yatakuwa ya amani ambapo amewataka polisi kuwalinda kwani maandamano hayo yatakuwa ya amani na utulivu mkubwa yakiwa na lengo la kupeleka ujumbe kwa watanzania wote juu ya mchakato huo wa katiba.
HOT NEWZZ--CHUO CHA IMTU CHAFUNGIWA
Na karoli Vinsent
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Imekifungia kwa mda,Chuo kikuu cha tiba na Sayansi IMTU kutofanya udahili kwa Wanafunzi wapya wa Mwaka wa Masomo 2014-2015,kutokana na chuo hicho kukiuka sheria inayosimamia Vyuo Vikuu nchini.
Uamuzi huo wa kikifungia Chuo hicho Umetangazwa mda huu Jijini Dar Es Salaam na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) Profesa Magishi N Mgasa wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari ambapo alisema maamuzi hayo yamefikiwa baada kikao cha Dharura kilichoitishwa na (TCU) wiki iliyopita na kujadili taarifa ya timu iliyotathimini chuo hicho,
Ambapo kikao hicho kikabaini mapungufu makubwa katika chuo cha IMTU yakiwemo matatizo ya uongozi,kukosa wahadhiri wakutosha na wenye sifa,kutokuwepo na Vifaa pamoja na kudahili wanafunzi bila hata kuwa na taratibu zilizowekwa na tume,
Profesa Mgasa alisema kwa kufanya hivyo chuo cha IMTU imekiuka sheria ya namba 5(1),sura ya 346 ya sheria za Tanzania ambayo inakitaka chuo Kikuu chochote kufuata taratibu zilizowekwa na tume,
Vilevile Profesa Mgasa alizidi kusema baada ya Tume kubaini makosa hayo,ndipo wamefikia maamuzi ya kukifungia chuo cha IMTU kufanya udahili kwa wanafunzi wapya wa Mwaka 2014-2015,mpaka pale itakakaporekebisha mapungufu yaliyotajwa na Tcu,
Pia tume imetoa notisi ya miezi 3 kwa chuo cha IMTU,kuanzia tarehe 16 mwezi huu kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza na endapo chuo hicho kikikaidi basi TCU haitosita kuwachukulia hatua kali ikewemo hata kukifungia kabisa.
Aidha Profesa Mgasa aliwataka wanafunzi nchini wasijiunge na chuo Kikuu chochote bila ya kufuata maelekezo kutoka Tume ya vyuo Vikuu nchini (TCU).
Wednesday, September 24, 2014
HIKI NDICHO ALICHOKIFANYA BAKHRESA KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TANZANIA LEO
KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa Group Limited, leo imetoa kiasi cha Sh. Milioni 10 kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa ajili ya tuzo za Wanamichezo Bora nchini, zilizopangwa kufanyika Desemba 12, mwaka huu.
Akikabidhi fedha hizo, Meneja Mkuu wa SSB Limited, Sheikh Said Muhammad Said katika ukumbi wa City Sports Lounge, Mtaa wa Samora, Dar es Salaam, amesema kwamba wanatoa mchango huo ili kuwezesha zoezi hilo lifanikiwe.
“Kwanza nasema naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa niaba ya kampuni kwa TASWA kutufuata kutuomba tuchangie tuzo hizi. Sisi tupo mstari wa mbele katika kuunga mkono harakati zote za kimaendelea katika sekta ya michezo nchini,”amesema.Sheikh Said amesema kwamba SSB inajivunia kuwa sehemu ya shughuli hiyo na inawatakia kila la heri TASWA ili wafanikishe mchakato huo.
SIRI IMEFICHUKA--MAGAZETI YA NIPASHE,TANZANIA DAIMA NA MAWIO HATARINI KUFUNGIWA,SOMA CHANZO HAPA
Na karoli Vinsent
SERIKALI ya Tanzania imezidi kuuzika uhuru wa Habari nchini kutokana na sasa kuanza kuvifungia vyombo vya Habari hususani Magazeti,baada ya hivi sasa serikali kujiweka tayari kuyafungia magazeti ya Nipashe,Tanzania Daima pamoja Mawio,Mtandao huu unaripoti
Taarifa za kuaminika ambazo mtandao huu umezipata zinasema serikali imejipanga kuyafungia magazeti hayo kutokana na habari wanazoziandika ambazo serikali inaziita ni za uchochezi,
Kwa mujibu wa Vyanzo mbalimbali zinasema serikali imekasirishwa na Habari wanazoziandika magazeti hayo kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba ambazo wanadai habari hizo zinaleta mgongano kwa wananchi,
Mpashaji huyo wa Habari aliuambia mtandao huu kwamba kwasasa serikali imejipanga kuhakisha inayafungia magazeti hayo.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA MWAKA LA WAKAGUZI WA HESABU ZA NDANI JIJINI ARUSHA LEO.
Tuesday, September 23, 2014
BREAKING NEWZ--YAMETIMIA BUNGE LA KATIBA
MH. CHENGE AWASILISHA RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA MWENYEKITI WA BUNGE MAALUM LA KATIBA.
Hayawi hayawi yamekuwa sasa. Ile KATIBA INAYOPENDEKEZWA yatoka rasimi leo.
Imekabidhiwa kwa Mwenyekiti na kesho (24/09/2014) itawsilishwa rasmi kwenye Bunge zima la Katiba.
Pichani Mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba Mhe. Andrew Chenge akimkabidhi Mwenyekiti wa Bunge hilo Mhe. Samuel Sitta Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo leo (23/09/2014).
Kamati ya Uandishi imemaliza kazi ya kuandaa Rasimu hiyo na inatarajiwa kusomwa Bungeni kesho.
TAARIFA KWA UMMA KUKANUSHA UVUMI WA KUAJIRI VIJANA 500 NA KUWAPATIA MASOMO YA MAFUTA NA GESI-TPDC
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
Kuna taarifa zimeendelea kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na maelezo kuwa: ” Serikali kupitia Shirika la Elimu Tanzania, TPDC kwa ushirikiano na kampuni za oil and gas, wanatarajia kuajiri vijana wapatao 500 katika sekta hii mpya Tanzania kuanzia mwezi Januari na Machi 2015, hivyo
wameandaa crush program itakayoanza 6 Oktoba 2014. Walengwa ni vijana wenye elimu ya form 4 na form 6 ambao watasoma kwa miezi 6 na kupelekwa kwenye ajira moja kwa moja baada ya kuhitimu!..kwa wale wenye elimu kuanzia diploma watasoma kwa miezi 3, kozi ya oil and gas management!…Ada kwa kundi la kwanza ni tshs 1,150,000 na kundi la pili ni Tsh 550,000. Kwa yeyote mwenye kuhitaji fursa hii akachukue fomu Shirika la Elimu Tanzania, application form ni Tsh 20,000 na deadline ni tarehe 30 Septemba 2014″.
TPDC inapenda kuwaeleza Watanzania kuwa habari hizo si za kweli na kwamba TPDC haijafanya makubaliano yoyote na Shirika la Elimu kuhusu suala hilo. TPDC inawaasa Watanzania kuchukua tahadhari ya matangazo ya aina hiyo na inapotokea, tafadhali wasiliana nasi kwa namba za simu zilizooneshwa hapo nchini.
IMETOLEWA NA
KITENGO CHA MAWASILIANO,
SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA
BWMPensions Towers, TowerA,
Junctionof Azikiwe /JamhuriStreets
P. O. Box2774,
Tel: +255 22 2200103/4
Dar-es-Salaam, Tanzania
PRESIDENT KIKWETE IN DIFFERENT ACTIVITIES IN NEW YORK
President Jakaya Mrisho Kikwete greets Senator Chris Coons of Delaware who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly
President Jakaya Mrisho Kikwete invites Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of Perdue Farms Mr Jim Perdue who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly
President Jakaya Mrisho Kikwete in talks with Senator Chris Coons of Delaware and Chairman of Perdue Farms Mr Jim Perdue and their delegation who paid a courtesy call on him in New York in the sidelines of the UN General Assembly
Subscribe to:
Posts (Atom)